AlFatwa 7

Bismillah Al-Rehman Al-Raheem Anti Ahmadiyya Movement in Islam

Kwa jina la mwingiwa wa Rehema, Mwenye kurehemu.

Maulidi ya Mtume yeye Furaha!

FATWA YA KIMATAIFA NAMBA 7

Mwanzilishi na Raisi: Syed Abdul Hafeez Shah Mhariri: Dk. Syed Rashid Ali

Wasomaji wapenzi!

Seyidna Muhammad (SAW) alikuwa mtume wa mwisho katika msururu wa mitume wa Allah ambaye ametuletea Quran Takatifu ikiwa ni ujumbe wa mwisho ambao muumba wetu ameuleta kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu kwa nyakati zote zijazo. Sisi umma wa Muhammad (Rehema na amani za kudumu zimshukie) tumetukuzwa kwa tuzo hili toka kwa Allah na tumepewa habari njema yafuatayo.

“Leo hii nimekamilisha dini yenu kwenu ninyi nimekamilisha mapenzi yangu kwenu, na nimeuchagua uislamu kama njia yenu ya maisha kwenu” (Quran 5:4).

Imani hii katika ujumbe na mtume wa mwisho na ukamilifu wa dini yao ndicho kitu kinachotofautisha taifa la kiislamu na dini nyingine na kitu hicho kinakuwa kama kizuizi dhidi ya harakati zote za uasi wa kidini na nguvu zote zinazochangukana au zinazotengana ambazo ulimwengu mpana wa kiislamu. Quran, vitabu vya Hadithi na sira, vitabu vya Taarikh (vitabu vya historia) na maandiko matakatifu mengine ya dini nyingine vimethibitisha kuwa Syedna Muhammad (SAW) ni mtume wa mwisho wa Allah (SW) na ni kisawe na imani ya ukamilifu wa dini na Quran ni ujumbe uliofunuliwa au ni ufunuo toka kwa Allah (SW) kwa ajili ya kuongoza viumbe wake.

Allah (SW) anasema katika Quran:

“Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume bali yeye ni mtume na mwisho wa Mungu na mwisho wa mitume, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu (Quran 33:40).

Mtume Mtakatifu Muhammad (SAW) alitangaza:

“Kwa hakika utume na unabii vimesiamishwa. Kwa hiyo hakutakujakuwa na mtume wala nabii baada yangu mimi”. (Tirmidhi, Juzuu ya 2 uk 51: Masnad ya Ahmed).

Mitume wote wametoa (wametangaza) habari njema za ujio wa nabii mpya, lakini mtume Muhammad alituonya kwamba:

“Katika umma wangu kutazaliwa (kutatokea) waongo thelathini (30) kila mmoja akidai kuwa ni mtume. LAKINI MIMI NI MTUME WA MWISHO (KHATAMUN – NABIYIIN) HAKUTAKUWA NA MTUME BAADA YANGU”. (Abu Dawood, Tirmidhi)

JAMAA YA AHMADIYYAH NA CHUKI YAO DHIDI YA UNABII WA SYEDNA MUHAMMAD (SAW)

Miongoni mwa vikundi mbali mbali dhidi ya harakati za kiislam ambavyo mara kwa mara vimejitokeza katika karne ya 14 ya historia ya kiislam, ukadiani u-ahmadiyyah hauna kifani.

Mirza Ghulam Ahmad Qadiani, muasisi wa harakati za Ahmadiyyah, ameshambulia ujumbe (Quran) na mtume akiupinga unabii wa Syedna Muhammad (SAW) pamoja na kubadilisha na kuvuruga ujumbe wa Quran. Wakijizuga na kujifanya kama wao ni mabingwa wa kiislamu, wanaeneza itikadi yao ya uwongo wakinufaika na ujinga walionao waislamu katika sehemu nyingi za ulimwengu.

Kwa ujumla waislamu wanajua misingi ya kiislam. Lakini hawajui udanganyifu mtakatifu wa Ahmadiyyah katika jina la uislam. Watu wachache wanaelewa kwamba mtu huyu ambaye alianza kama mhubiri na mlinzi wa uislamu, alifundishwa na bwana zake wa kikoloni (British Raj) kudhoofisha mapenzi kwa mtume Muhammad (SAW) katika mioyo ya waislamu kwa kuvuruga na kubadilisha mafunzo ya Quran na hivyo kujaribu kuugawa ummah wa kiislamu.

MIRZA GHULAM ALIDAI KUWA MTUME

“Wafu ni wale ambao hawakumkubali mtume mmoja. Aliyebarikiwa ni yule aliyenitambua mimi. Miongoni mwa njia za Allah mimi ni njia ya mwisho na katika taa zake zote mimi ndio taa ya mwisho Mkosefu wa bahati ni yule anayenitupa kwa kuwa bila mimi kuna giza totoro”. (Kishtee-e-Nooh, Roohani Khazain Juzuu ya 19.uk.61)

BAADAYE ALIDAI KUWA UJIO WA PILI WA MTUME MUHAMMAD (SAW)

"Muhammad mMume wa Allah na wale walioamini ni wakali kwa makafiri, wanarehemeana baina yao katika ufunuo huu (wahyi huu) Mungu ameniita mimi Muhammad na pia mtume” (Roohani Khazain Juzuu ya 18, uk. 207)

“Pindi ninapokuwa mfano au kiigizo cha mtume na utimilifu (mafanikio) wote wa Muhammad pamoja na utume vinaakisiwa katika kivuli cha kiza changu, baadaye ni mtu gani mwingine aliyedai utume?” (Ek Ghatti Ka Izala, uk 8 Roohani Khazain, Juzuu 18 uk 212)

“Ni mimi pekee niliyechaguliwa katika umma huu kupata jina la “Mtume” Hakuna mtu mwingine ambaye anastahili jina hili na imepangwa kutokea hivyo …ili kwamba kama ilivyotajwa katika hadithi iliyosahihi kwamba kutakuweko na mtu kama huyo ambaye anatimilizwa katika bishara” (Haqeeqatul wahi, Roohani Khazain Juzuu ya 22 uk. 407).

Kwa hiyo Mirza aliiba heshima ya Khatam-Un Nabiyeeni – Mtume wa mwisho kutoka kwa Mtume Muhammad (SAW) na akaitumia yeye mwenyewe. Baadaye Mirza anaweka msingi wa umma ambao ni sambamba kwa kuita taifa lote la kiislam makafiri na wanaharamu.

“Isipokuwa kwa watoto wanaozaliwa na MALAYA, ambao mioyo yao imepigwa muhuri na Allah, kila mtu ananiamini mimi na amekubali utume wangu. (Aina – e – Kamalat – Islam, Roohani Khazain Juzuu ya 5 uk 547).

“Mungu amenifunulia (kwa njia ya wahyi) kwamba mtu yeyote aliyefikiwa na ujumbe wangu na hakunikubali basi sio Muislam” (Barua ya Mirza iliyotumwa kwa Dkt Abdul Hakeem).

MATAMSHI YA MIRZA BASHIR, Mwanae Mirza:

“Yeyote anayemuamini Musa lakini hamwamini Yesu, au anamwamini Yesu lakini hamwamini Muhammad, au anmwamini Muhammad lakini hamwamini Masihi aliyeahidiwa sio kafiri tu lakini ni kafiri aliyethibitishwa na ametoka katika uislam”. (Kalimatul Fasl, uk 110, - Mirza Bashir Ahmad)

MABADILIKO KATIKA QURAN NA JAMAA YA AHMADIYYA

Jamaa ya Ahmadiyya inajivuna kwa kuchapisha misahafu ya Quran Takatifu katika lugha nyingi. Kitu watu wanashindwa kukijua ni kuwa Mirza Ghulam na wafuasi wake walijaribu kwa maksudi kabisa kupotosha ujumbe wa Quran. Mabadiliko hayo yanaweza kufanywa katika njia zifuatazo:

·          Mabadiliko katika matini ya Quran

·         Mabadiliko katika tafsiri na ufafanuzi wa matini

·         Matumizi mabaya ya aya za Quran

·         Utanguzi na ubatilishaji wa sheria za Quran.

Mirza Ghulam A. Qadiani ni mwenye hatia (mkosaji) katika makosa yote manne. Wakati msahafu kwa lugha ya kiarabu haijabadilishwa maana, ametoa mchango mkubwa katika kupotosha tafsiri, ufafanuzi na matumizi mabaya ya aya zake mbalimbali.

 

MABADILIKO KATIKA MATINI YA QURAN

Japokuwa matini ya kiarabu ya msahafu wa jumuia ya Ahmadiyya haukubadilishwa, lakini Mrza Ghulam amebadilisha matini ya aya mbalimbali za lugha ya kiarabu akivinukuu katika vitabu vyake. Mifano michache inaambatanishwa katika ukurasa huu.

MABADILIKO KATIKA TAFSIRI NA UFAFANUZI:

Mifano ya mabadiliko ya maana za Quran ni mingi, mashuhuri zaidi ikiwa aya 33:40 “Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu bali yeye ni mtume wa Mungu na mwisho wa mitume. Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu”. Kutokana na aya hii na hadithi ya mtume kuhusiana kuwa kwake mwisho wa mitume wa Allah, karne zote waislamu wamekuwa wakiamini kwa pamoja kuwa mtume Muhammad (SAW) kuwa mtume wa Allah (SW) Khatam – Un-Nabiyiin. Lakini muulize Qadiyani au Ahmadiyya yeyote, mfuasi wa Mirza Ghulam, watasema hivyo hivyo. Hapana hapana! Huu mhuri (Khatan) siyo mhuri wa kuhitimisha, bali ni mhuri wa kuidhinisha ujio wa mitume wengine. Lakini hata hivyo baada ya kunyemelea katika huu mlango wa nyuma wa utume,

(Mirza Ghulam) anaufunga tena kwa kusema. “Atukuzwe yule ambaye amenitambua mimi. Miongoni mwa njia (ziendazo) kwa mwenyezi Mungu, mimi ni njia ya mwisho, na katika taa zake zote, mimi ni taa ya mwisho. Amekosa bahati yule ambaye ataacha kunifuata mimi, kwa sababu bila mimi vyote vitakuwa giza”  (Roohani Khazain, Juzuu ya 19, uk 61).

Lakini hawatakuwa na ibu kwa swali hili: unamuitaje mtu anayeiba cheo au (heshima) Khatam – Un-Nabiyiin kutoka kwa mtume mtakatifu? Watu hawa wamepigwa na bumbuwazi!

MATUMIZI MABAYA YA AYA ZA QURAN

Quran takatifu imejaa aya ambazo Allah anamsifu kipenzi mtume wake Muhammad (SAW). Kwa mfano Quran 9:33, 17,1, 3:31, 48: 1 – 2, 36:1 – 3, 108:1, 21: 107 n.k. zote ni aya mashuhuri ambazo ziliteremshwa hususan kumsifu (au kumtukuza) mtume wa kiislam.

Kwa hali yoyote ile fungua vitabu vya Mirza Ghulam, hususan Haqeeqatul wahi, Juzuu ya 22 Roohani Khazain, na utaona kuwa toka kurasa 77 hadi 111 wizi wa maandishi usiokuwa na haya wa matini ya Quran inayotajwa na Mirza kama kielelezo ufunuo au uzinduzi ulioletwa kumsifu Mirza kwa mfano:

·         “Ni yeye aliyemleta (aliyempeleka) mtume wake na mwongozo na dini ya haki, ili iweze kushinda dini zote” (As-Saff 61:9) (Tazkirah uk. 387 – 388 toleo la 4).

“Sema (ewe Muhammad, kwa wanaadamu):

 Kama mnampenda Mwenyezi Mungu, nifuataeni mimi, mwenyezi Munguatawapendeni” (Aal-Imran 3:31) Haqiqat-ul-wahi, uk 82). “Wala hasemi kwa matamanio yake (ya nafsi yake) hayakuwa haya (anayosema) ila ni wahyi (ufunuo) uliofunuliwa (kwake)” (An-Naju 53:3-4) (Tazkirah. uk 378). "Sema (ewe Muhammad) Enyi watu hakika mimi ni mtume wa Allah kwenu ninyi nyote” (Al-A’raf 7:158) (Tazkirah uk, 352 toleo la 4). “Bila shaka wale wanaofungamana nawe. (Muhammad) kwa hakika wanafungamana na Mwenyezi Mungu. Uwezo wa Allah uko juu ya uwezo wao” . (Sarat Fath 48:10) (Haqiqatul-wahi, 80). Sema mimi ni binaadamu kama ninyi, mola wangu ananifunulia (ananiletea wahyi) kwamba Mungu wenu ni Mungu mmoja” (surat Kahf 18:110) (Haqiqat-ul-wahi uk 81) “Bila shaka tumekupa (ewe Muhammad) kushinda kuliko dhahiri ili mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yanayokuja” (Surat Fath 48:1-2) (Haqiqat-ul-wahi uk. 94) “Hakika sisi tumekuleteeni mtume aliyeshahidi juu yenu, kama tulivyompeleka mtume kwa Firauni”. (Surat Muzammil 73:15) (Haqiqat-ul-wahi, uk 101). “Hakika tumekupa kheri nyingi” (Suratul Kauthar 108:1) (Haqiqat-ul-wahi, uk 102). “Yaa Syn, Naapa kwa hii Quran yenye kutengenezwa vizuri (iliyojaa hekima) kuwa hakika ya wewe ni miongoni mwa mitume (wa mwenyezi Mungu) waliotumwa juu ya njia iliyonyooka” (Suratul-Yasin 36:1-4) (Haqiqat-ul-wahi uk. 107, Tazkirah uk. 479). “Na (wewe Muhammad), hukutupa wewe ule mchanga katika gao lako la mkono ulipotupa, lakini Allah ndiye aliyeutupa (Suratul-Anfal 8:17) (Haqiqatul wahi uk. 70). “Aya ya Quran Takatifu (17:1) Subhana ladhi asra be’abdihi lailan min al-masjid al haram ila almasjid alaqsa… “Utukufu ni wake yeye ambaye alimpeleka mja wake usiku (mmoja tu) kutoka msikiti mtukufu (wa Makka) mpaka msikiti wa mbali (wa Baitul Muqaddas) – Masjid Aqsa… matumizi yake halisi ni ule msikiti ambao umejengwa na baba yake Mirza na ambao upanuzi wake umefanywa na Mirza”. (Makusanyo ya matangazo, juzuu ya 3 uk 286)

Hebu fikiri kwa karne nyingi waislamu walikuwa wapumbavu kupigania umiliki wa mji mtakatifu wa Jerusalem. Kutokana na Mirza Ghulam, Masjid Aqsa (msikiti wa Jerusalem) uko Qadian na mtume mtakatifu alienda Qadian na sio Jerusalem usiku wa Miiraj. Huduma ilioje kwa Mayahudi!!

 

UBATILISHAJI WA SHERIA ZA QURAN

Dhana ya Jihad katika uislam ni vita ya halali iliyo na malengo na makusudi yaliyowazi: Kukomesha uonevu (au udhalimu) ili kuihifadhi haki ya mtu katika makazi yake na uhuru katika Taifa lake, kuzuia mateso katika dini na kuhakikisha kuwepo uhuru wa imani (ya dini) kwa watu wote.

Allah anasema:

“Na piganeni nao mpaka kusiwe na mateso, na dini iwe ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa madhalimu. (Quran 2:193)

“Na waueni popote muwakutapo, na muwatoe popote walipokutoweni…” (Quran 2:191)

“Na nyote piganeni na makafiri kama wao (wote) waanvyopigana nanyi; na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaomuogopa. (Quran 9:36)

Licha ya makatazo au amri hizi za wazi toka kwa Mwenyezi Mungu, kutokana na amri za wakubwa wake, Mirza Ghulam alitangua (alifuta) au kubatilisha wazo la Jihad. Aliandika:

“Kutokana na umri wangu mdogo hadi sasa nikiwa na umri wa miaka 65, nimejishughulisha na kalamu na ulimi, katika shughuli muhimu ya kugeuza mioyo ya waislamu na kuelekea mapenzi ya kweli na urafiki na upole kwa ajili ya serikali ya kiingereza na kuondosha kabisa (kufitilia mbali) wazo la Jihad kutoka katika mioyo ya waislamu wasio na akili (wapumbavu)”. (Kitabu-ul-bariyah, roohani Khazoin Juzuu ya 13 uk 350).

“Kwa ajili ya serikali ya kiingereza, nimechapisha na kusambaza kurasa zenye matangazo 50,000 katika nchi hii na nchi nyingine za kiislamu (dhidi ya Jihad)… matokeo ni kwamba mamia ya maelfu ya watu wametupilia mawazo yao machafu kuhusu Jihad” . (Roohani Khazain, Juzuu ya 15 uk. 114).

Ni matusi kama haya dhidi ya Mtume mtakatifu wa kiislamu na majaribio ya kugeuza au kubadili ujumbe wa Qurani uliopelekea au kuufanya umma mzima wa kiislamu kutamka au kutangaza kuwa Mirza Ghulam na Jamaa ya Ahmadiyyah kuwa ni makafiri na kuwa wametoka nje ya uislamu. Lakini wanaendelea kujigamba kama wao ni mabingwa wa uislamu wakiwashawishi waislamu wajinga na wasio na hatia hasa wale waliopo Afrika tokana na uislamu aliokuwa nao Mtume Muhammad (SAW) kuelekea katika kanuni ( au itikadi) ya udanganyifu ya Mirza Ghulam, iitwayo Ahmadi Islami (uislamu wa Ahmad).

(Tunamuomba) Allah, awaepushe waislamu wote na udanganyifu huu katika jina la uislamu na kuwaonyesha wafuasi wa Ahmadiyyah walio wajinga, sura halisi ya Mirza Ghulam Qadiani, kwa kuwa (itikadi zake) haziafikiani na maandiko yake ya asili. Amin.

Rehema na Amani kwa wale wote wanaofuata mwongozo.

Dkt. Syed Rashid Ali

P.O. Box 11560

Dibba Fujairah U.A.E

rasyed@emirates.net.ae

http://alhafeez.org.rashid/

 

تاريخ الاضافة: 26-11-2009
طباعة