Merchant of Qadian

Bismillahir Rahmanir Rahiim

 

Mirza Ahmad: “Mtamani pesa wa Qadiani”

Mwasisi wa dini ya Ahmadiya

Aliogopa U*****ara

Aliwataka wafuasi wake wamtii Malkia Viktoria

Na. Dk. Rashid Ali

Historia inabainishia kwamba, mitume walikuja kuwakomboa watu  kutokana na utumwa wa aina zote tangu ule wa minyororo hadi  wa tamaa za nafsi, ili kuwafanya wawe huru wanaomtii na kumtumikia Allah, ambako kutawapelekea wafikie kilele cha amani katika ulimwengu huu na ujao.

Kwa ajili hiyo, Mitume hawakupigania kujilimbikizia mali wakilenga kuishi kwa wasaa na starehe, hawakufanya hivyo kwao binafsi wala kwa wafuasi wao. Kwa mfano, usiku wa siku ya aliyokufa mtume(s.a.w), hata taa nyumbani kwake haikuwa na mafuta.

Kinyume na uchaMungu huo waliokuwa nao Mitume, wapo wadanganyifu wanaowadanganya wanaadamu kwa jina la dini, wakilenga kujipatia mali ili waishi vizuri. Watu hawa hawauzi tu imani yao kwa starehe ndogo za ulimwengu huu bali kibaya wanachouzia nafsi zao ni kuwajibika kwao katika kuharibu imani za wale ambao kwa bahati mbaya wametumbukia katika hadaa zao za kidini.

Katika toleo hili la Fatwa, Mwandishi amelenga kufichua vipengele vyote ya maisha ya  mmoja wa Wadanganyifu(matapeli) wa kidini aitwaye Mirza Ghulam Ahmad Qadiani, Mwasisi wa Jamaat Ahmadiya ambaye kwa tamaa ya kujipatia pesa, amepoteza wengi, na tutaonesha pia ni kwa kiasi gani amejikhasirisha yeye mwenyewe.

Baada ya kuyasoma makala haya, tunatumai wafuasi wake wachache waliobaki hapa na pale, wataona jinsi walivyotekwa kwa laghai. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape busara ya kupambanua ukweli na uongo kisha awaongoze katika njia sahihi. Amiin.

   Ndugu wasomaji,

Waislamu wote tunaamini pasi na shaka kwamba wahyi(ufunuo) ulikomea kwa Mtume Muhammad(s.a.w). lakini hata tukijaalia ufunuo bado ungaliunaendelea(kama wanavyodai akina Mirza) na usiku mmoja ikatokea mmoja wetu kwa ghafla anazungumzishwa na Allah, hivi anaweza kujisikiaje kwamba licha ya kupata fursa hiyo ataendelea kuona ni kitu kidogo tu kisicho na maana sana kwake? Ni taathira gani atakayokuwa nayo mara baada ya tukio hilo? Tukiangalia tukio kama hilo na fursa hiyo ilipomfikia Mtume Musa(a.s) haraka sana aliomba amuone Allah. Kadhalika Mtume(s.a.w) alipopata fursa hiyo ya kwenda Miiraj na kutakiwa aombe atakacho, akawaombea maghfira wafuasi wake.

Lakini tunamshuhudia mdanganyifu Mirza akidai kusemeshwa na Allah, alichokiwaza akiwa katika “fursa” hiyo ni hofu yake ya kufikwa na u*****ara na tamaa ya kupata mali. Katika moja ya maandiko, Mirza amenukuliwa akisema:

“Nilipopokea Wahyi kuhusiana na kifo cha baba yangu, ubinaadamu ukanifanya nidhani kwamba tungeishi maisha ya dhiki kwa kuwa aliyekuwa akituhudumia sasa hayupo”, (imenukuliwa kutoka “The founder of the Ahmadiya Movement kilichondikwa na Muhammad Ali uk. 7; pia taz. Ruuhani Khazin juzuu ya 13 uk. 194).

Mirza alidai huu ndio  “Wahyi” wa kwanza alioshushiwa na Mwenyezi Mungu. Hata hivyo wakati anashushiwa wahyi huo kikubwa alichokiwaza ni ile dhiki itakayowafika mara baada ya kufa baba yao. Anafikiria pesa. Wakati Mwenyezi Mungu anamfahamisha juu ya kifo cha baba yake, haraka anachokichelea “Mtume” Mirza ni upungufu wa mali!

Mtume asiyejua jukumu lake

Kwa mujibu wa Mirza wakati huo kama mtume hakujua jukumu lake lingekuwa lipi katika ulimwengu huu, katika hali hiyo anadai Mwenyezi Mungu(naudhubillahi) alimfanya kuwa ndiye Yesu aliyekuja kwa mara ya pili. Uzoefu huu uliwezaje kuyageuza maisha ya Mirza Ghulam. Kuhusiana na hili Mirza amenukuliwa akisema:

“Kwa kuzingatia ahadi ya kwamba mtu anayeitwa Maryam ameahidiwa kwamba atainuliwa daraja kwa Yesu kuzaliwa naye ambaye ataitwa mwana wa Maryamu; ambaye ni mimi. Ufunuo utamjia Maryamu na mimi kadhalika lakini tofauti itakuwa kwamba Maryamu atasumbuliwa na mateso ya kimwili mimi nitataabika kwa kukosa pesa”(Taz. Nazool ul-Masih).

Kwa mara nyingine tena, alichokificha nyuma ya madai yake kinadhihirika, kwamba anateuliwa na Mwenyezi Mungu kuwa Masihi aliyeahidiwa lakini kikubwa anachowaza ni namna atakavyosumbuka kipesa!

Ni vipi tutamtofautisha mtu huyu  anayedai utume na wale walaghai watafuta pesa.

Sababu za kudai kwake utume

Akielezea sababu ya kuteuliwa kwake kushika jukumu hilo, Mirza katika “ufunuo” wake anasema:

“Masihi aliyeahidiwa amepokea ufunuo ili kuifanya biashara hii kuwa yenye faida kwangu”(Taz. Riwayat sahaba. Juzuu ya 11 uk. 106, na juzuu ya 14, uk.40).

“Masihi aliyeahidiwa amepokea ufunuo: Nimewekeza mtaji wangu kwenu. Mnajua faida na hasara yake”.(Taz. Mansab Khilafat uk. 40).

Kuporomoka kwa familia yake

Katika wasifu wake, Mirza anaelezea kuporomoka kwa familia yake:

“Huko nyuma, babu yangu, Mirza Gul Mohammed alikuwa Chifu na mtu maarufu kwetu, baadaye karibu babu zangu wote waliteketezwa....baadaye katika utawala wa Ranjit Singh, marehemu baba yangu, Mirza Ghulam Murtza, alirejea kijijini Qadiani, na alivichukua vijiji 5 vilivyokuwa vikimilikiwa na baba yake...katika hali hiyo ya uzee, baba yangu Ghulam Murtaza aliendelea kuwa chifu maarufu eneo hili”. (Kitab ul Bariyah, Roohani Khazain juzuu ya 13 uk 175-176).

“Kwa kifupi, hali ya nyumbani kwetu iliendelea kuporomoka siku hadi siku, mwishowe tukafikia mahali ambapo familia yetu ikawa ya daraja la chini”.(Tohfa-e-Qaiseriya, (Roohani Khazain juzuu ya 12 uk. 271).

Baada ya hapo wakati Waingereza walipokuja, wakaitaifisha ardhi yetu, na wakawa wanatulipa kiinua mgongo cha Rupiya 700 kwa mwaka ambacho kiliendelea kupunguzwa hadi kufikia Rupiya 180 wakati alipokufa babu, na baada ya kufa mjomba malipo hayo yakasimamishwa”.(Taz. Seerat ul Mahdi sehemu ya kwanza riwaya na. 48, kilichoandikwa na Mirza Basheer Ahmad(Mirza Ghulam Qadian).

Mirza Ghulam alichanganyikiwa kutokana na kuporomoka kiuchumi kwa familia yake. Kuchanganyikiwa kwake kulimfanya asiwaze kingine ila namna takavyoweza kuishi katika mazingira hayo duni kiasi kwamba kama anavyodai mwenyewe Mungu alipomteua, muhimu alichoweza kukikumbuka  ni dhiki yake ya kipesa.

Mirza - mwana mfujaji

“ Mama(mke wake Mirza) aliniambia(mtoto wake Mirza) kwamba katika ujana wake Hazrat Masiih Mowood(Mirza Qadiani) alikwenda kuchukua kiinua mgongo cha babu yako, kisha Mirza Imamudin alikwenda mbele yake. Alipopokea ushuru ule, Imamdin akamshawishi(Mirza) badala ya kwenda Qadian wakenda sehemu ya mbali, na akawa anahangaika naye huku na kule. Baadaye Mirza akazifuja pesa zote, Imamdin akaachana naye na kumkimbia”, (Siiratul Mahdi sehemu ya kwanza riwaya na. 49, kilichoandikwa na Mirza Bashiir Ahmad, mtoto wa Mirza Qadian).

Mirza Imamdin alikuwa mpwa wa Mirza Qadiani wakati tukio hili linatokea yeye alikuwa na umri unaopata miaka 30 hivi. Kiinua mgongo hiki cha Rupiya 700 kwa kulinganisha na pesa ya hivi leo inaweza kuwa sawa na laki kadhaa za Rupiya. Wapi Mirza na mpwawe walikwenda kufuja pesa nyingi kiasi hiki kwa muda wa siku chache, kila mmoja anaweza kuhisi vyake. Lakini kubwa ni vile mtu anavyoweza kupima akili ya mtu huyu ambaye baadaye amekuja kudai  anapokea ufunuo kama mtu aliyekuja kuuhuisha upya Uislamu. Kwa hiyo hakuja kuupigania Uislamu bali alichokuwa akikipigania ni m*****o na tumbo lake akikusanya mapesa kutoka kwa  wajinga ndio waliwao.

Mirza ataraji kupata riziki kimiujiza

“Awali, Mirza Saheb alikwenda Amratsir, akakutana na mtakatifu Maulvi Abdullah Ghaznawi. Mirza akamuomba: “Niliajiriwa(Mirza) kama karani wa mahakama ya Sialkot kwa mshara mdogo sana. Kwa kuwa ilikuwa vigumu kuishi kwa kajimshahara haka, nikajaribu kufanya mitihani ya kozi ya sheria, nikafeli. Moulvi Saheb alimuuliza, sasa ndio unatakuniambia nini, unakusudia nini sasa? Mirza Saheb alisema: Sasa sikusudii kufanya kazi, nataka kuishi kwa Tawakkul(kwa kumtegemea Mungu bila ya kufanya kazi), kwa hiyo nakuomba uniombee dua ya Rajuu’at na Futuhaat( Rajuu’at ni neno litumikalo kwa mtu mwenye kutaraji kuwa na mvuto kwa watu, na Futuhaat ni neno lenye maana ya watu watakaovutiwa naye watampa vitu mbali pamoja na pesa). Tafadhali niombee dua”,(Masih wa karne ya 14 uk. 48).

Mirza adai kapata ufunuo afunge ndoa, lakini ahofia ulofa

"Alama ya 27 ya utume, ni hii bishara kuhusu ndoa yangu ambayo ilifanyika mjini Delhi. Mwenyezi Mungu aliniteremshia ufunuo usemao: “Ametukuka Mwenyezi  Mungu aliyekuinua daraja kinasaba na kindoa, huyo ni Mungu aliyeifanya nasaba yako kuwa tukufu na mke pia atatokana na familia tukufu”.  Ufunuo huu ulikuwa bishara ya wazi, kwa sababu hiyo ule wasi wasi wangu uliongezeka nilikuwa nikihofia ni namna gani nitakavyomudu gharama za ndoa hii”.(Roohani Khazain juzuu ya 22 uk. 2470).

Mirza anadai kupewa bishara na Allah kuwa ataoa, anachohofia atapata wapi pesa ya kufunga ndoa na atamlisha nini mke huyo!

Mirza aomba michango kuchapisha

Njia rahisi na ya haraka ambayo Mirza alidhani ingemuwezesha kutatua dhiki yake ya pesa ni kuwanyonya watu kwa kutumia ujinga wao kuvuna mapesa yao. Bara hindi kama linavyofahamika limegubikwa na imani nyingi za kishirikina zinazonasibishwa na dini, hivyo tangu awali Mirza aliona mwanya mzuri wa kueneza mawazo yake ya kijinga ni kuchapisha vitabu atakavyovinasibisha na Uislamu.

Kitu cha awali alichofanya ilikuwa kutangaza azma yake ya kuandika kitabu chenye juzuu 50 kuthibitisha ukweli wa Uislamu. Kwa ajili hiyo akawataka Waislamu wachangie gharama za uchapishaji. Hiki kilikuwa kipindi ambacho Waislamu wa India walikuwa katika hali ngumu sana. Waingereza waliua kabisa nguvu za Waislamu ambao walitawala bara hilo kwa zaidi ya miaka 1000 badala yake walizipa nguvu jumuiya za Wamishenari wa kikristo na Wahindu kueneza itikadi zao huku wakiukejeli na kuupotosha Uislamu. Hivyo Mirza kwa tangazo lake ilionekana ni uamsho mkubwa kwa Waumini wa dini ya kiislamu ambao hawakujua kuwa ilikuwa ni katika njama zile zile za wakoloni wa kiingereza kuupiga vita Uislamu. Ilikuwa katika mazingira haya Mirza akatangaza mradi wake wa kuchapisha juzuu 50. Kwa kauli yake Mirza anasema:

“Ni vigumu kuweza kuchapisha kitabu kikubwa kiasi hicho bila ya msaada wa ndugu  Waislamu. Na kila mtu anajua thawabu atakazopata kwa kusaidia mradi huu muhimu. Kwa hiyo shime kila mwenye imani yake, achangie kazi hii nzuri ili asaidie uchapishaji wa kitabu hiki. Wale walio matajiri wakichangia gharama ya maakuli yao ya japo siku moja, itarahisisha zaidi kuchapishwa  kitabu hiki , vinginevyo mwanga huu utabaki mafichoni. Au wale watakaoweza  kutanguliza pesa zao kununua kitabu hiki kabla ya kuchapishwa, wanitumie rupiya 5 wakimbatanisha na maombi yao, pindi kitabu kitakapochapishwa watatumiwa” (Majmoo-Istihaarat, Collection of Advertisement, juzuu ya 1 uk 11-12).

Waislamu walichangia kwa ari kubwa mradi huo huku wengi wakitanguliza pesa kusubiri nakala za kitabu hicho baada ya kuchapishwa. Mirza hakuweza kutimiza ahadi yake licha ya mapesa mengi aliyopokea kutoka kwa Waislamu badala yake kwa muda wa miaka minne(1880-1884) akaandika juzuu 4 tu akielezea Uislamu na kuwatumia watu, baada ya hapo akadhamiria kwa  kipindi cha miaka 50 baadaye awe anaandika juzuu baada ya juzuu alizoziita Braheen Ahmadiya akielezea dini yake hiyo mpya na kuzigawa bure baada ya kutangulia kupokea mapesa ya watu. Alisimama kuandika Braheen Ahmadiya baada ya kutoa juzuu nne tu. Licha ya kupata upinzani mkali kutoka kwa wanunuzi, kwa kipindi cha robo karne alichapisha na kuuza vitabu vingine vipatavyo 80. Miaka 25 baadaye akachapisha juzuu ya tano ya Braheen Ahmadiya. Katika neno la awali la juzuu hiyo amendika:

“Awali nilifikiria kuandika juzuu 50, lakini sasa nimeamua kuzinya juzuu 5 badala ya 50 na kwa vile tofauti ya tano na hamsini ni sifuri(dot)(sifuri inatamkwa kama dot katika numerali za kiarabu /kiurdu) kwa hiyo kwa juzuu hizi 5 nimekamilisha ule mradi wa juzuu 50”.(Preface to Braheem Ahmadiya, Roohani Khazain vol.21 uk.9)

Laghai huyu ndiye anayedai utume.

Funuo 50,000 zinazungumzia masuala ya pesa

Ukisoma maisha ya Mirza Ghulam, ukisoma vitabu vyake, na ukitazama harakati zake zote utagundua yote yanahusisha masuala ya pesa:

“Kumbukeni kwamba Mwenyezi Mungu amejenga desturi kwangu mara nyingi ninapoelekea kuata pesa au vitu vingine kama zawadi, Hunifahamisha mapema ama kwa njia ya wahyi au ndoto; na alama hizo zimenifunukia si chini ya mara 50,000”. (Haqeeqat ul-Wahyi, Roohan Khazain Vol. 22 uk. 346).

Mifano mingine ya funuo zinazoelekea kwenye pesa

“Ndoto nilimsikia mtu mmoja akitaja: Noti, kisha nikapewa kitabu kana kwamba kina noti ndani yake na wahyi ukaanza kutiririka kutoka katika ulimi wangu):Tazameni rafiki zangu, habari mpya imechapishwa”.(Al-Hakam, Vol.X, Na. 6, February 17, 1906, uk.1).

“Niliona karatasi ndotoni, mistari michache iliandikwa kwa herufi za Kipeshia na iliyosalia iliandikwa kwa kingereza. Niliielewa kana kwamba mtu aliniita jina langu na kuniambia angenipa rupiya 25.(Review of Raligions, Vol.IV, No.2 Februari 1905

“Ndotoni, nilimuona mke wa Qudratullah akinipa rupiya”(Al-Hakam, Vol.IX, Vol. IX, Na. 36, oct.17, 1905, uk. 10)

“Niliona ndotoni alfajiri moja mtu mmoja akinipa kifurushi kilichojaa rupiya ambacho nilizikipokea na kuzivingirisha kwaa kitambaa cheupe”(Diary of the promised Mesiah, uk 23).

Mara moja nilipokea Wahyi kwamba ningepata rupiya 21. Kwa hiyo Wahyi huu uliwataja vile vile Aryas(Wahindu wanaoishi Qadiani)...ziada ilikuwa kuwafanya Waarya washuhudie, utamu uanaogharimu rupiya 1 utakaogaiwa kwao...kama si hivyo, huenda wakakumbuka alama hii baada ya kuonja tamu tamu hiyo.(Roohani Khazain Vol. 22 uk. 318.

Mpaka hapo msomaji ameona unaodaiwa kuwa ni wahyi  aliopokea Mirza ulivyojihusisha na mambo ya pesa. Zaidi ya hivyo inaonekana alikuwa makini sana na  ndoto au wahyi zake zilizohusu pesa.

Mipango ya kuvuna mapesa

Ili kuijpatia mapesa kutoka kwa watu, Mirza alibuni njia nyingi ikiwa ni pamoja na kuwaahidi watu kuwa angechapisha kitabu muhimu hivyo walitakiwa kuachangia gharama kuwezesha kutoka kitabu hicho. Aliweza kuchapisha Kitabu chake cha Braheen Ahmadiya kwa mbinu hii kisha kujikusanyia mapesa za mauzo. Moja ya maandiko yamemkairiri Mirza akidai:

“Taifa lazima lisaidie Jamaat kwa kila namna iwezekanayo. Vile vile wasisite pia kuisaidie kifedha. Tazameni, hakuna harakati zozote za duniani zilizoshamiri pasi na watu kuchangia... hivyo  kwa wanajamaat vile vile hili ni muhimu kwao kulizingatia. Iwapo kila mmoja atatoa pesa ndogo tu kila mwaka ni wazi mengi yatawezekana kufanywa. Na iwapo mmoja wenu hayuko tayari kujitolea walau visenti vichache alivyo navyo, ana haja gani ya kuwepo ndani ya Jamaat?”(Matamshi ya Mirza yaliyochapishwa katika Al Ahbar ABadr Qadian ya tarehe 9 JUlai1903).

Kauli hiyo inathibitisha wazi kwamba ili uwe mwanajamaat wa Ahmadiyyat hunabudi kuwa na tabia ya udanganyifu.

“Tangazo hili si la kawaida, najaribu  kutoa wito wa mwisho kwa wale wanaojiita muridi wangu kwamba mapenzi yangu yako kwa wale tu wanaoonekana kuwa ni watoa misaada, lakini wako wengi wanaotaka kumdanganya Mwenyezi Mungu. Sasa kwa mujibu wa mfumo huu mpya, kila mmoja arejee upya kiapo chake na atoe ahadi mpya ya maandishi kwamba ni sharti kwake kila mwezi achangie kiasi gani....  mpaka miezi mitatu baada ya kuchapishwa tangazo hili, tumekuwa tukisubiri majibu kutoka kwa kila mmoja wenu kulingana na alivyoahidi katika mfumo huu kwa kila mwezi na iwapo hapatakuwa na majibu kwa muda wa miezi mitatu jina la muhusika litaondolewa katika ahadi hiyo... na iwapo mtu baada ya kukubali kuchangia, hatatuma mchango wake kwa miezi mitatu, jina lake pia litafutiliwa mbali”.(Collection of Advertisement vol.3 uk 468-469).

Dua kwa malipo kwa malipo ya rupiya 500

“Nawab Saheb, chifu wa Maleer Kotla alipatwa na maradhi, maradhi hayo yalidumu muda mrefu. Mawakala wa Qadiani waliokuwa wakiishi eneo hilo wakamwambia mama yake Nawab Saheb kwamba iwapo Mirza Saheb angeombewa dua angepona haraka. Baadaye alipelekwa kwa Qadian Saheb ambaye aliahidi kumuombea dua na akawataka wailipie  kiasi cha Rupiya 500. Baada ya kupokea pesa hiyo kutoka kwa mama yake Saheb, Qadian Saheb alimuombea dua, hata hivyo Nawab hakuweza kupata nafuu yoyote na hatimaye akafariki dunia na ile pesa haikurejeshwa”.(Isha’at us Sunnah Vol. 18 uk. 146, iliyotajwa katika Raees-e-Qadian uk. 427 na Rafiq Dilawari).

Lengo la Zaka- Kueneza jina la Mirza

Zaka, na sadaka kwa kawaida hutolewa na waumini kwa lengo la kupata radhi za Allah, hayo ndiyo mafundisho ya Uislamu. Lakini kwa mujibu wa itikadi ya Ahmadiayya inelezwa kama ifutavyo:

“Wakati wa Hazrat Maseeh Mowood mwarabu mmoja *****ara alimjia. Mirza akampa kiasi kikubwa cha pesa. Mtu mmoja alipoona hivyo akapinga, lakini Mirza akamwambia. (Nimempa pesa hii) kwa kuwa kila atakakokwenda atakuwa akinijitaja mimi kwa msaada huu niliyompa, atakuwa akinitaja kila atakapopokea chochote, kwa ajili hiyo atakuwa ameeneza jina langu sehemu za mbali”.(Akhbar AlFazl, Qadian, vol.22. No.103, uk.9 ya tarehe 26 februari 1935).

Techee Techee

Mirza anadai alipokea msaada kutoka kwa malaika ulioitwa Techee Techee.

Mnamo Machi 5 1905 niliota ndoto mtu mmoja ambaye alionekana kama Malaika, alikuwa mbele yangu na akaweka mdomoni kwangu pesa; nikamuuliza jina lake, akasema hana jina. Nikamuuliza tangu hapo unalo jina fulani; akasema jina langu Techee Techee, Techee katika lugha ya kipanjapi ni jina la muda fulani ulioahidiwa, nimekuja katika muda ule khasa ninaohitajika. Nikaamka. Kwa kweli sikuamini macho yangu nikajikuta nikipokea maelfu ya Rupiya kutoka kwa watu baada ya ndoto hiyo”.(Haqeeqatul Wahi, Roohani Khazain, juzuu ya 22,uk.345-346).

Pesa za misaada na matumizi yake

Pesa zilizokusanywa kwa njia mbali mbali zilitumikaje.

“Sasa tutazame namna gani tunavyoweza kumpa pesa za matumizi Mahdi aliyeahidiwa kutokana na ama hizi za msaada au vyanzo vingine kwa ajili ya familia, ndugu na jamaa zake. Kila mtu anafahamu jambo hili kwamba Hazoora(Mirza) angepaswa kupewa sehemu ya pesa kutoka katika makusanyo haya. Hivyo baada ya kifo chake iwe wajibu kwa Anjuman(Ahmadiyya) kuipa familia hiyo kama alivyofanya Masih Mowood mwenyewe, hiyo ni kwa sababu Anjuman hawezi kuwa muaminifu zaidi kuliko Masihi Mowood”.(Izhaar-e- Haqeeqat uk. 13 tarehe 28 Novemba 1913, iliyochapishwa na Anjuman Ansarullah Qadian).

Mirza ashtakiwa kwa kuiba pesa a ushuru na matumizi mabaya ya michango ya wafuasi wake.

“Mwaka huu Mirza Ghulam Ahmad kipato chake cha mwaka kilikadiriwa kuwa Rupiya 7200 na kodi itakayokatwa kutokana makadirio hayo ni Rupiya 187.50...Mirza Ghulam Ahmad akaidai anapata kipato chake kutoka katika shamba lake, ardhi na bustni zake; maingizo ya kutoka katika shamba lake ni kiasi cha Rupiya 82 annas 10, kutoka kaika kipande chake cha ardhi anachomiliki ilikadiriwa ni Rupiya 300 na kutoka katika Bustani yake ilikadiriwa kwa mwaka inaingiza Rupiya 200/300 au 400 au kiwango cha kabisa Rupiya 500. Mirza alidai kuwa hakuwa na vyanzo vingine vya pesa mbali ya maingizo hayo. Mirza Ghulam alidai vile vile kwamba alikuwa akitegemea kupokea kiasi cha Rupiya 5200 mwaka huo kutoka kwa wanafunzi na wafuasi wake. Hata hivyo hapakuwa na kumbukumbu zozote za namna alivyokuwa akitumia pesa hizo, aliyatamka hayo kutoka kichwani mwake. Mirza vile vile alidai kwamba kipato chake binafsi kutoka shambani kwake, ardhi aliyokuwa akimiliki na bistani yake kiliosheleza mahitaji yake binafsi, hivyo  hakuhitaji kupewa misaada na wafuasi wake kujikimu.”(Matamshi ya Munshi Tajuddin Saheb, Sub-divisional income tax collector, Batala, District Gurdaspur tarehe 31 Agost 1898, iliyorekodiwa katika Income Tax Case no. 46/55 ya 1898; haya yameelezwa katika Roohani Khazain juazuu ya 13. uk.516).

Mirza aliapa mbele ya watoza kodi kwamba hakuwa akitumia pesa iliyotokana na michango ya wafuasi wake kwa mahitaji yake binafsi. Lakini awali tuliona:

“Sasa tutazame namna gani tunavyoweza kumpa pesa za matumizi Mahdi aliyeahidiwa kutokana na ama pesa hizi za msaada au vyanzo vingine kwa ajili ya familia, ndugu na jamaa zake. Kila mtu anafahamu jambo hili kwamba Hazoora(Mirza) angepaswa kupewa sehemu ya pesa kutoka katika makusanyo haya. Hivyo baada ya kifo chake iwe wajibu kwa Anjuman(Ahmadiyya) kuipa familia hiyo kama alivyofanya Masih Mowood mwenyewe, hiyo ni kwa sababu Anjuman hawezi kuwa muaminifu zaidi kuliko Masihi Mowood”.(Izhaar-e- Haqeeqat uk. 13 tarehe 28 Novemba 1913, iliyochapishwa na Anjuman Ansarullah Qadian).

Pesa za misaada kutoka kwa wafuasi na maisha ya nyumbani kwa Mirza

“Awali tulikuwa tukiwataka wanawake waishi kwa kuiga mwenendo wa Mtume; wale kiasi na wapendelee vitu vikavu, na wavae nguo chakavu na vilivyoziada wavitoe kwa ajili ya Allah.Kadhalika nasi tuwe na mwenendo huo. Kwa hotuba hii tuwe na kawaida ya kuhifadhi pesa na kuzipeleka kwa Qadian. Wake zetu walipokwenda kwa Qadian na kukaa huko, walifuatilia kila kitu kwa makini sana na waliporejea walitushambulia kuwa tu waongo wakubwa kwa kuwa wameshuhudia wenyewe maisha ya Mtume Mirza na wafuasi wake baada ya kutembelea Qadian. Maisha ya raha wanayopata wanawake huko ni sawa na 0.1%. Mbali ya ukweli kwamba tunaingiza mapesa mengi na vyovyote pesa itakavyotumika itakuwa imetumikia Taifa letu. Kwa hiyo ninyi ni waongo mliotudanganya muda mrefu, sasa hatutadanganywa nanyi tena. Hivi sasa hawatupi tena pesa tupeleke Qadian..”(Kashf ul Ikhtilaf uk. 13 by Sarwar Shah Qadian).

“Siku moja msikitini mbele ya Maulvi Mohammed Ali Khwaja Kamaludin, Sheikh Ramat Ali mtu mmoja kutoka Ludhiana alieleza kwamba jumuiya imechukua mkopo kadhalika watu hujitolea kutoka katika mishahara yao ya mwezi kuchangia jumuiya lakini inavyoonekana hapa pesa zinatumika kununulia nguo na mapambo ya mke wa Mirza(Biwi Saheb), nini hiki kinachofanyika?”(Sermon of Mira Mahamud, Khalifa wa pili Alfazl Qadian tarehe 31August 1938).

“Kikwazo kikubwa ni kwamba yeye(Dr. Abdul Hakeem) alitoa hoja kumpinga Masihi aliyeahidiwa kuhusiana na masuala ya pesa, eti Mirza anachukua pesa kutoka kwa watu na anazitumia atakavyo....yeye Mirza anakusanya pesa akidai kutaka kuchapisha vitabu na anazikusanya kwa kudanganya watu, na anazitumia hivi na vile atakavyo, haulizwi kwa matumizi hayo”.(AlFazl Qadian ya tarehe 20januari 1921).

Shaghalabaghala za mahesabu ya pesa za michango

Moulvi(Mohammed Hussein Batalvi) Saheb alisema unakwenda Qadian, mpe ujumbe wangu Mirza Saheb kwamba anipe hesabu za maingizo yake.. pesa za uma zinazotumika hovyo, pesa hii inatumika wapi na vipi... nilifika Qadian na nikampa ujumbe ule Moulvi Saheb. Hazrat Masih Mowood akaniambia kwamba nimjibu ya kwamba pesa iliyokuja ni kwa ajili ya Allah na tutaitumia kwa ajili hiyo, hatuna rekodi yoyote ya matumizi ya pesa hizo..”(Mapokezi ya  Qadian yaliyotajwa katika AlFazl Qadian Na. 201 juzuu ya 123 ya terehe 28August 1946).

Maoni ya wafuasi kuhusiana na Mirza

Iwapo itadhaniwa kuwa wafuasi wa Mirza walifurahiwa na namna ya ufujaji wa pesa ulivyokuwa ukifanywa na Mirza basi asome yafuatayo:

“Hazrat Maseeh Mowood.... alionesha kuhuzunishwa sana pale alipotakiwa na Kamaluddin  kukabidhi kazi ya  uangalizi wa meko ya umma kwao, kwa kuwa hawakumuamini. Na kwa hivyo aliona meko hiyo ifungwe badala ya kukabidhiwa waangalizi wengine. “Hii kazi imekuwa chini yangu lakini yeye  licha ya mimi kumwambia haya ni majaaliwa ya Allah na katika maisha yangu kazi ya nimekuwa nikifanya kazi hii alishikilia nikabidhi usimamizi huo .”(Kashf ul Ikhtilaaf uk. 14 na Srwar Shah Qadian).

Kulingana na matumizi mabaya ya pesa, utumiaji mbaya wa meko za umma, na ufujaji uliokuwa ukifanywa na Mirza, Kamaluddin kwa hasira alimwambia Moulvi Mohammed Ali kwamba:

“Hii ni haki kweli, kama unavyojua pesa za umma zinakusanywa kwa taabu sana na hoja inayotolewa na Taifa limekuwa likiwataka watu wajinyime katika mahitaji yao, sasa badala ya pesa hizo kutumika katika miradi iliyopangwa zinatumiwa na watu binafsi kukidhi mahitaji yao(Mirza na familia yake) na kiasi hicho cha pesa vile vile hakitoshelezi kuendesha miradi tuliyoinzisha. Tumelazimika kuiweka kando miradi mingine kwa ukosefu wa pesa, iwapo kusingelikuwa na matumizi binafsi haya ya pesa tungaliweza kutenga kiasi cha pesa kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo iliyowekwa kando.”(Kashaf ul Ikhtilaf uk. 15 na Sarwar Sha Qadiani).

“Katika tukio moja wakati zilipokwenda kukusanywa pesa kwa ajili ya ujenzi wa shule, Khawaja alimwambia Moulvi Mohammed Ali kwamba Hazrat Saheb(Mirza Qadian) peke yake amekuwa akiishi maisha ya anasa huku akituhutubia sisi tujinyime na kwa kupunguza matumizi yetu. Katika kujibu Moulvi Saheb alisema ndiyo hatuwezi kulipinga hilo, huo ndiyo ubinaadamu.”(Barua ya Mian Mahmud kwa Hakeem Nuruddin, Haqeeqat e Ikhtilaaf uk. 53 na Muolvi Mohammed Ali).

Mirza akasirishwa na Muridi wake

Mirza anatakiwa kutoa mahesabu ya pesa za jumuiya badala ya kuto hesabu hizo anageuka kuwakaripia wanaomuhoji.:

“Yule anayenipa, kisha akanikemea kwa namna ninavyotumia, amenishambulia, na shambulio hilo haliwezi kuvumiliwa...sitowajali hata kidogo watu hao, nitawaona sawa na vijidudu vifu ambavyo nyoyo zao zimejaa kutu na kukosa uaminifu... Mimi si mfanyibiashara ninayeweka mizania ya mauzo, manunuzi na matumizi. Mimi vile vile si muweka hazina ninayetakiwa kuhakikiwa na yeyote .”(Matamshi ya Mirza Qadian yaliyochapishwa katika gazeti la Alhakm la tarehe 31 Machi 1905; Mafoozaet juzuu ya 7uk.325).

“Yeye(Mirza Saheb) alisema kwamba leo Khawaja Saheb ameleta barua ya Moulvi Mohammed Ali na akasema kwamba Saheb ameandika kwamba matumizi ya meko ya uma ni kiasi, maelfu ya rupiya zinazokusanywa yanakwenda wapi? Na kisha yeye(Mirza)alikuja huku na kutuambia kwa hasira kwamba hawa jamaa wanatuona sisi ni Haram Khor(wabadhirifu)? Wana uhusiano gani na pesa hizi? Iwapo mimi nitajiondoa kwenye jumuiya pesa hizi hazipatikana tena.”(Barua ya Man Mahmud kwa Muolvi Nuruddin, Haqeeqat e Ikhtilaf uk. 52 na Moulvi Mohammed Ali).

Kustawi kwa ukadiani na vishawishi kwa Muridi

Mirza alithubutu hata kuwahonga watu ili kuwafanyawajiunge na uqadiani, kwa maneno mengi Mirza alitumia pesa:

“Tuliota Ukadiani umekuwa kama Jiji kubwa na soko lake likiwa limetandwaa kwa mawanda ya mbali. Majengo yenye roshani 2 na 4 yenye maduka yaliyo na dari na kuta zinazovutia, na matajiri  wanene wakiwa mbele ya masoko yaliyofura bidhaa na mapambo ya almasi, lulu, fedha na sarafu za dhahabu.(Matamshi ya Mirza yliyonukuliwa na gazeti la AlHakam Qadian la tarehe 3 Aprili 1902).

Masharti ya kuzikwa katika eneo la makaburi ya  watu wa 'mbinguni '

Mnamo mwaka 1906, Mirza Ghulam alitoa andiko lenye masharti kadhaa kwa wafuasi wake wanaotaka wazikwe kwenye makaburi maalum ya watu mbinguni baada ya umauti kuwafika. Aliorodhesha masharti kadhaa baadhi yake ni haya:

1.   Sharti la kwanza

  

“...Kwa hiyo sharti la kwanza ni kwamba, yeyote ambaye angetaraji kuzikwa katika makaburi haya, atapaswa kuchangia pesa ili kufidia gharama za ujenzi.

2.   Sharti la pili

“Sharti la pili ni kwamba mwanajumuiya yeyote wa Ahmadiyya atapaswa kuzikwa hapa iwapo ataacha wasia akiwa bado yu hai kwamba atakapokufa moja ya kumi ya mali yake yote itakwenda kwenye m*****o wa mazishi ya eneo hili la makaburi haya”.

  

3.   Sharti la tatu

  

“Sharti la tatu ni kwamba yule anatarji kuzikwa katika eneo hili la makaburi atapaswa kuwa muangalifu sana katika uhai wake, yule ambaye atajiepusha na makatazo yote na ambayo hatafanya dhambi yoyote ya shirki”(Chanzo: The Will. uk. 40-44. Roohan Khazain juzuu ya 20 uk.316-327).

Hapa msomaji atakuwa ameona kwamba ukiacha sharti la tatu, masharti mawili ya mwanzo yote yamejiegemeza kwenye pesa. Kwa mujibu wa masharti hayo, ni wale tu watakaoweza kulipia ndiyo watakaopta fursa ya kuzikwa eneo maalum la watakatifu na hatimaye kuingia peponi! Si hivyo tu, ili kupata nafasi katika makaburi hayo, mtu atapaswa kuacha wasia kwamba atakapokufa sehemu ya mali yake iingie katika m*****o wa Jamaat. Zaidi ya hivyo, Mirza alisisitiza kwamba:

“Hazrat Masih Mowood anasema..yule ambaye hataacha wasia(utengao fungu la pesa kwa jamaat), ni mnafiki”(Minhaj ut Talibeen, collection of Speech na Mian Mahmaud, Khalifa wa pili

Nukuu zote hizi zinathibitisha kuwa alichokithamini Mirza Ghulam Ahmad katika uhai wake ilikuwa ni pesa. Ilikuwa ni pesa zilizomsukuma kuibua fikra potofu na kuanzisha miradi ya kuwanyonya watu kwa jina la dini na ilikuwa ni kwa sababu ya kutafuta pesa na maslahi ya kidunia yaliyompelekea Mirza kikaragosi wa Serikali ya Uingereza. Kwa sababu hizo Mirza hakusita kuuza imani yake na wala hakuogopa kupoteza imani ya maelfu ya watu waliomfuata.

1.   Mirza alipandikiza fundisho potofu la imani ya kurithisha katika mafundisho ya kiislamu ili kuhalalisha na kudumisha  madai yake ya kikafiri.

2.   Aliugawa umma wa kiislamu

3.   Alihubiri kuwatumikia makafiri na akawafanya waliomfuata kuwa watumwa wanaowanyenyekea makafiri(hasa serikali ya Uingereza).

  

Mirza Qadian na Serikali ya Uingereza

Akitumia vipeperushi na makala, Mirza Ghulam alijigamba kuwa angeweza kuifutilia mbali dhana ya Jihad miongoni mwa waislamu. Alifanya kazi hiyo kwa kutumwa na serikali ya uingereza:

“Waheshimiwa maafisa wa serikali mara kwa mara katika nyaraka zao wamekuwa wakieleza wakitoa ushahidi juu ya msimamo huu wa maoni kwamba familia hii tangu huko imeendelea kuwa imara yenye matarajio na yenye utii. Serikali iwe makini na mbegu hii inayojiotosha yenyewe....inapaswa kuwaelekeza maafisa waoneshe ukarimu, wanisaidie na kutoa kipaumbele kwangu na kwa Jamaat yangu. Sisi hatutasita kumwaga damu zetu kwa ajili ya kuwalinda watawala wa kiingereza, hatukusita huko nyuma wala hatutasita sasa kufanya hivyo”. (Roohan Khazain juzuu ya 13 uk. 350).

“Mimi binafsi nimeungana na serikali ya Uingereza kwa jili hiyo ambayo kwa hakika ni ya kuonesha wema kwa serikali hii tukufu, hiyo ni kazi kubwa na muhimu kuliko wahenga wangu(mababu zangu) na kwamba jukumu lenyewe ni hili, nimekusanya vitabu vya kiarabu, kifursi na kiurdu kwa ajili hii kwamba...kuitii serikali kwa dhati kabisa ni wajibu kwa kila Muislamu”.(Advertisement of Mirza Qadian, collection of Advertisement vol. 2 uk.366).

“Hivyo nimetumia kiasi kikubwa cha pesa kuchapisha vitabu hivi na kuvigawa katika nchi za kiislamu. najua kwamba vitabu hivi vitakuwa na athari kubwa katika nchi hizo pia. Na wale wote wenye usahiba nami wa kiitikadi unaotufanya tuwe jumuiya ambao mioyo yao imeshibishwa imani ya kuitii serikali , msimamo wao thabiti na nadhani kwamba watakuwa wazalendo kwa nchi  na wenye dhati ya kuyatoa muhanga maisha yao kwa ajili ya serikali.”(Advertisement of Mirza Qadian, Collection of Advetisment vo.2uk.367).

“Katika ukurasa wa 241 wa Braheen Ahmadiyya, kuna bishara juu ya serikali ya Uingereza. Na bishara yenyewe ni hii: Mwenyezi Mungu si yule ambaye ataifanya serikali ipate isumbufu na ninyi watu muishio ndai ya utawala huu. Kokote mtakakoelekea, Mwenyezi Mungu yuko huko. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu anajua kwamba moyo wangu unafuraha chini ya kivuli cha ulezi wake na serikali ya amani, nabaki kuwa mwenye hamasa ya kuiombea dua kwa sababu siwezi kufanya kazi zangu kikamilifu katika miji ya ya Makkah na Madina wala Istanbul(Rome), Syria, Iran, wala Kabul”.(Collection of Advertisement vol.2 uk. 370).

“Hazrat Masih Mowood anasema, Serikali ya Uingereza ni upanga wangu. Kwa nini sisi Ahmadiyya tusifurahie ushindi huu dhidi ya Baghdadi(Iraq), iwe ni Arabuni au Syria, tunataka kuona mnga’aro wa upanga wetu kila mahali”.(Matamshi ya Mirza Mhamud katika AlFazl Qadian ya tarehe 7 septemba 1918).

“Huu ni kama ushahidi wa kuchomoza mwanga katika siku mpya kwamba kiuhalisia Serikali ya Uingereza ni ngao inayokinga uahmadiyya uweze kusonga mbele. Jaribu kuondoa ngao hii walau kwa muda mdogo tu utaona ni namna gani utakavyoandamwa na kuchomwa na mvua ya mikuki yenye sumu kichwani mwako. Hivyo kwa nini tusiwe wenye shukrani kwa serikali hii? Maslahi yetu yanasimamiwa na serikali hii na kuvurugwa kwa serikali hi itakuwa ni kuvurugwa kwetu na kustawi kwake itakuwa ni kustawi kwetuPopote utakapoenezwa utawala wa serikali hii, itakuwa umefungua eneo jipya kwa mahubiri yetu. Kwa hiyo hapatakuwa na upinzani wowote dhidi ya serikali utakaogeuza utiifu wetu kwayo, na kamwe hapatakuwa na mpumbavu aliyetayari kuhatarisha maisha yake mwenyewe”.(Alfazl Qadian, vol.3 Na.51 ya tarehe 19Oktoba 1915).

“Namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amenipa nafasi chini ya kivuli cha serikali hiyo, ambayo kwa ulinzi wake naweza kuwa huru kuendelea na kazi ya kuhubiri na kushauri. Ingawa ni wajibu kwa kila mmoja kuonesha shukrani kwa ufadhili wa serikali hii lakini nadhani imekuwa wajibu zaidi kwangu kwa sababu malengo yangu haya makuu yamefikiwa kutokana hifadhi na ulinzi wa serikali hii ya Malikia Victoria, nisingaliweza kukamilisha malengo hayo chini ya serikali nyengine yoyote ile hata kama ingalikuwa ni serikali ya kiislamu.(Roohani Khazain vol. 12uk. 283).

SubhanAllah!! hapa ndipo mahali pa kupazingatia. Ni malengo yepi hayo aliyokusudia Mirza kuyakamilisha ambayo yasingaliwezekana bila ya ulinzi wa Serikali ya Uingereza ambayo yasingaliwezekana kufikiwa chini ya hata serikali ya kiislamu.

“Awali ya yote namshukuru Allah kwa kwa fadhili zake kwangu wakati wa utawala wa Malkia wa India(Malkia Victoria) na amuongezee hadhi na heshima abaki kuwa mwenye furaha yeye, jamaa na watoto wake”... uaminifu huu una kiwango cha juu cha utiifu, mapenzi na unyenyekevu ambao sina maneno ya kuuelezea  kwa Hazoora Malika-Aalia(Mtukufu Malkia) na waheshimiwa Maafisa wake . Kwa sababu ya imani na mapenzi ya kweli, naandika juzuu kwa mnasaba wa sherehe za jubelee na kuiita “Tohfa e- Qaiseriyah” ambayo nitaituma kwa Janab Mamdooha(mtukufu) kama Darwesh wa sasa...nanyanyua mikono yangu kuomba; Ee Mwenyei Mungu uweke utawala  huu wa mpendwa Malkia wa Uhindi juu ya vichwa vyetu, himaya yake idumu. O Qaisariyya e Mubaraka Malkia! Mwenyezi Mungu akulinde, akupe uhai mrefu, heshima na mafanikio, nyoyo zetu zielekee kwako... ni ukweli kwamba nyoyo zinazopendana hukumbukana), Sihitaji kutumia lugha ngumu kuelezea ninavyokupenda katika moyo wangu, moyo umekita mapenzi na  heshima kwako. Dua zetu za usiku na mchana zimeendelea kukutiririkia kama mkondo... ingawa najua kwamba nimetekwa na hisia kali katika moyo wangu, ningepaswa kelezea heshima, utii na shukrani zangu mbele ya Hazoora e Hind, utawala wake uwe daima dumu, lakini siwezi kuelezea shauku ya dhati niliyo nayo”.(Sitara -e-Qaisariyah, Roohan Khazain juzuu ya 15 uk. 111).

“Vitabu nilivyoandika katika kuutukuza utawala wa kiingereza vimesheheni makabati, hasa vile vilivyojaribu kufutilia mbali dhana ya Jihad ambayo waislamu wengi wameishikilia na kuiamini sana. Hili ni jukumu kubwa kwa serikali. Kwa hiyo natumai zawadi nono inayolingana na kazi hiyo”.(Tabligh e Risalat, Vol.7, uk. 19).

Picha halisi ndiyo hii. Jukumu la Mirza lilikuwa kujiingia katika kupiga vita moyo wa Jihad miongoni mwa Waislamu ili wawe watiifu kwa makufari. Alikuwa akimuomba Mwenyezi Mungu adumishe utawala wa serikali ya kikafiri kwa sababu ilikuwa ndio ngao yake. Mirza Ghulam Ahmad alikuwa ndiye wa kwanza kujiita Mtume katika historia ya Uislamu aliyehubiri utwana kwa wafuasi wake. Tukiwaweka kando Mitume wa Allah, hajatokea kiongozi wa nchi yoyote ile iliyependelea utumwa badala ya uhuru kwa nchi yake. Lakini Lahaula! Mirza kwa tamaa ya maslahi ya kidunia, aliuza imani yake na imani ya maelfu ya waliomfuata. Hii ndio maana alipokula kiapo cha utii, moja ya masharti ilikuwa utii kwa serikali ya Uingereza:

“Masharti ya uzinduzi: Nimewasilisha vielezo vya hotuba zangu za muda wa miaka 17...ambazo zinazothibitisha wazi kwamba nimekuwa nikiitakia mema serikali ya uingereza kwa dhati ya roho na moyo wangu..kama nilivyoelekeza mwanzo katika sharti la 4 la uzindui kwamba kwa ukweli kabisa nimekuwa mtiifu kwa serikali ya kiingereza na ni mwenye roho yenye kujali  ubinaadamu”...”(Kitab ul-Bariyyah, Roohan Khazain vol.13 uk.10).

Ukweli huu waweza kuwashangaza wafuasi wengi wa Ahamadiyya wa hivi sasa kwa kuwa wengi wao hawajawahi kusoma vitabu vya Mirza Ghulam Ahmad na elimu yao juu ya mafundisho yake kwa kiasi kikubwa imeegemezwa katika maandiko ya propaganda yanayosambazwa ndani ya jumuiya hiyo. Uthibitisho mkubwa ni mfumo wa kuapa. Kiapo cha asili hivi sasa hakipo. Kiapo cha hivi sasa hakina sharti Na. 4 lililotajwa hapo juu. Limekwenda wapi sharti hilo? Nani aliyeliondoa sharti hilo? Nani anayejaribu kumdanganya nani? Makadiani  waulize maswali haya kwa masheikh(murrabbi) wao.

Dondoo kutoka maisha ya Mirza

Mnamo mwaka 1907 kuelekea mwisho wa uhai wake, Mirza alifanya tathmini ya kazi ya aliyoifa kwa miaka yote na mafanikio aliyoyapata:

“Hakuna anayenijua. Wala hakuna ajuaye kuwa ningaliweza kuja kuishi maisha ya wasaa. Nilivyokuwa navyo ni ilikuwa sehemu ndogo tu ya urithi  katika vijimali alivyoacha baba yangu. Baadaye Mwenyezi Mungu akaniwepesishia kidogo wakati ambapo sikuweza kutegemea kupata walau rupiya 10 kwa mwezi. Hata hivyo Mwenyezi Mungu akaigeuza hali yangu ya maisha na akaniunga. Sasa  nina zaidi ya rupiya laki tatu”(kwa kulinganisha na pesa za sasa hivi rupiya laki tatu ni mamilioni ya dola).(Roohan Khazain, Vo. 22,uk.220-221, Haqeeqat ul-Wahi, uk.211-212, 1907).

“Imekuwa ni wajibu kwetu kubaki tukiishukuru serikali hii tukufu ya Uingereza”.(Iza e Auham, footnote).

“Ushauri wangu kwa Jamaat ni huu, wanapaswa kuufanya himaya ya Kiingereza kama yenye mamlaka juu yao(Uulil Amr) na wabaki kuitii kwa moyo mkunjufu kabisa”.(Zuroorat ul Imam uk.23).

Taratibu za kipesa katika Ahmadiyya ya leo

Waliomfuatia Mirza katika uongozi wa Maqadian walikuwa na utamaduni wa kujali pesa zaidi:

“Ndoa ya Binti wa Amiiril Muuminina, Khalifa wa Masihi al Rabbi(Mirza Tahir), Atiya tul Mujiib(Tooba), Mwenyezi Mungu amlinde, ilifanyika mnamo saa 1.00 usiku uliokuwa wa furaha sana na baraka ndani ya eneo la Msikiti wa AlFazl...si chini ya wageni 600 walihudhuria... kabla ya hapo wakati wa swala za Ijumaa na Alasiri  siku hiyo, Huzoora aliitangaza ndoa hiyo ambayo ilifanyika kwa Muoaji Mukarram Malik Sultan Mohammed Khan Saheb mtoto wa Mukarram Malik Sultan Haroon Khan Saheb kulipa Mahari ya  Rupiya Milioni 1”.(AlFazl International 119 Novemba 1999 mapka 25 Novemba 1999).

Leo hii, kuna kiwango cha moja ya kumi au theluthi moja ya kipato  cha mwezi kinachotakiwa kilipwe na kila mwanachama wa Ahmadiyya kusaidia harakati za kueneza itikadi hiyo. Zaidi ya hivyo, kuna taratibu za aina nyingi za ukusanyaji pesa kwa madhumuni maalum. Profesa Munawaar amendika katika makala yake:

Kuna utoaji na utozaji mkubwa wa pesa katika jumuiya ya Ahmadiyya. Kila Ahmadiyya anapaswa kulipa asilimia 6 ya kipato chake kama CHANDA AAM. Ni malipo ya wajibu, kiasi ambacho hakitalipwa huoneshwa kama deni linalotakiwa kulipwa baadaye kupitia katika akiba yake ya benki. Iwapo Ahmadiyya atakataa kulipa CHANDA, anakoma kuwa mwanachama. Ingawa hiyo CHANDA ni kitu cha hiyari kisicho na kiwango maalum, mwanachama huweza kulipa zaidi kwa kadri ya uwezo wake wakati ambapo ushuru una kiwango maalum na ulipaji wake huwa wajibu, na kiasi kisicholipwa huoneshwa kama salio la deni lisilokwisha abadan.

Mbali ya malipo ya CHANDA AAM, pia kuna malipo mengine ya:

·         ·          CHANDA JALSA SALANA

·         ·          CHANDA TEHREEK JADEED

·         ·          CHANDA WAQF JADEED

·         ·          CHANDA SAD SALA JUBILEE(hii hivi sasaimefutwa)

·         ·          CHANDA KHUDDAMUL AHMADIYYA(CHANDA MAJLIS) ambayo inatakiwaitekelezwe na vijana

·         ·          CHANDA TAMEER HALL(ukumbi huu ulijengwa mwaka 1973 na kumalizika lakini ukusanyaji wa CHANDA hii unaendelea.

·         ·          CHANDA AFRICA

·         ·          CHANDA DISH ANTENA (Ahmadiyya TV Network).

·         ·          CHANDA LAJNA AMA’ALLAH(hii inatozwa wanawake)

·         ·          CHANDA ATFAAL(hii wanatozwa watoto).

·         ·          CHANDA ANSAAR(hii wantozwa watu wazima waliovuka umri wa mika 40).

  

Kwa ufupi, Ahmadiyya anatakiwa kulipa walau asilimia 10 ya kipato chake cha mwezi. Kuna mfumo wa hiyari wa ukusanyaji wa pesa za CHANDA ambazo mkusanyaji hapati sehemu. Ni mfumo ambao haupatikani mahali popote nje ya Ahmadiyya. Mara mbili tatu kwa mwaka wasimamizi tofauti wa CHANDA tofauti huja kutoka vituoni kuhakiki Akaunti ili kuhahakikisha kama kiasi kilichopokelewa kimetumwa(Chanbnagar-Rabwah). Kwa sababu ya mfumo huu, Jamaat inaonekana kama mtandao uliopangwa vizuri kumbe ni shaghalabaghala tupu usiofuata sheria wala kanuni. Jamaat ni kundi lililojiweka vyema katika ukusanyaji wa pesa. Kama kusingalikuwa na mfumo huu mzuri wa CHANDA, leo hii familia za watoto(warithi) wa Mirza Saheb wasingalimiliki maeneo makubwa ya Ardhi(murrabba)(inakadiriwa Murrabba 1 ni sawa eka 25) wala wasingeishi maisha ya anasa na ubadhirifu kama walivyo. Hii ndiyo “Baraka” ya mfumo huu wa pesa za Ahmadiyya). Waahmadiyya wengi huchanga pasi na kujua undani wa michango hiyo.

Rejea

Growing Number of Member in Jamaat Ahmadiyya by Prof. Munnawwar

Email: rsyed@emirates.net.

تاريخ الاضافة: 26-11-2009
طباعة