Knowledge of Mirza

Bismillah Al-Rahman Al-Rahiim

Harakati za Kiislamu dhidi ya Ahmadiyyah-Kampeni ya Uamsho

Ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayemzulia uwongo MwenyeziMungu au yule anayesema anapokea wahyi ilihali hakuna kilichoteremshwa kwake-AlQur'an.

Elimu ya Mirza

Uzushi, Uwongo na Ghiliba

Na Dkt. Rashid

Mwongo inabidi awe na Kumbukumbu Nzuri

Montaigne alisema kuwa ili mwongo afanikiwe katika uwongo wake, sifa ya kwanza kabisa ni ile ya kuwa na kumbukumbu nzuri. Mtu mwongo anahitaji sio tu kunyoosha kauli ziwe sawa sawa bali pia anyooshe kauli zake mbalimbali za marudio ili zote zisipingane. Hii ni kazi kubwa.

"Hakuna mwenye kumbukumbu ya kutosha kumfanya afanikiwe katika uwongo."- Abraham Lincoln

Mpendwa msomaji

Mirza Ghulam Qadiani, Mwasisi wa Jumuiya ya Ahmadiya, alidai kuwa yeye ni Nabii wa MwenyeziMungu, Masihi aliyeahidiwa, Imam Mahdi na mengine mengi kwa wakati mmoja. Alidai kuwa yeye kapokea wahyi kutoka kwa Mungu na kwamba Mungu kamfundisha kila kitu, pasipo kuwepo mtu wa kati.

"Na kama ninavyoamini aya za Qur'an, vivyo hivyo bila tofauti hata kidogo, naamini wahyi wa Mungu uliokuja kwangu..... Na naweza kusimama kwenye Khana Ka'aba na kuapa kuwa ufunuo mwema uliokuja kwangu, ni neno la Mungu yuleyule aliyeshusha wahyi kwa Musa na Yesu na Sayyidina Muhammad SallAllahu alaihi wassalam." (Aik Ghaltee kaa Izala uk.6 Roohani Khazain Juz.18 uk.210).

"Naapa kwa Mungu mimi naamini funuo hizi kama ninavyoamini Qur'an Tukufu na Vitabu vingine kutoka kwa Mungu, na kama ninavyoiitakidi Qur'an kuwa ni neno la hakika na lililokamilika la Mungu, ndivyo pia ninavyoamini kuwa wahyi unaoniteremkia ni neno la Mungu." (Haqiiqatul Wahi uk. 211, Roohani Khazain juz.22 uk.220).

Hivyo, tuna haki ya kujaalia kuwa chochote alichokisema Mirza Ghulam au kukiandika katika vitabu vyake kilikuwa kimefunuliwa kutoka kwa Mungu, kwa hiyo, hakuna suala la makosa, uwongo wala uzushi. Mirza alisema hivi:

"Bila shaka Mungu katu haniachi na kosa, hata kwa punde ya kupepesa jicho; na Hunikinga kutokana na makosa na Hunikinga na njia za mashetani." (Nur ul Haq, ukurasa wa mwisho, Roohani Khazain juz. 8 uk. 372).

"Kullama qultu qultu min amrahuu, wa maa fa'altu un amrii, wa maa aftaraitu 'alaa Rabbi al'Alaa'- Chochote nilichokisema, nimekisema kwa amri Yake (Mungu) na sijafanya chochote kwa matamanio yangu mwenyewe na sijamzushia chochote Mola wangu." (Mawahibur Rehman uk 3 Roohani Khazain juz. 19 uk.221).

" 'wa maa untiqu unil hawa in huwa illa wahun yuuha'- hasemi chochote kwa hiyari yake, bali chochote mnachokisikia ni wahyi wa Mungu." (Arba'iin Na. 3, Roohani Khazain juz. 17, uk. 426-427).

Matamshi haya ya Mirza Ghulam Ahmad Qadiani yako wazi. Chochote alichofanya au kukisema, chochote alichoandika, vitabu vyake vyote 83 vya ajabu ajabu, juzuu 10 za Mafuuzaat pamoja na mkusanyiko wa wahyi unaoitwa Tadhkirah, na juzuu 3 za mkusanyiko wa matangazo moja kwa moja vinafunuliwa kutoka kwa Mungu, kulingana na maelezo yake mwenyewe. Nina hakika kuwa Ahmadia/Makadiani/Malahori watakubaliana nami juu ya jambo hili.

Sasa basi, kama kuna kosa lolote au uwongo wowote katika vitabu hivi, ni nani anayehusika??? Je tunaweza kusema kuwa linatoka kwa Mungu (Ma'azAllah)? Kama si hivyo basi bila shaka 'Mungu' wake alimdanganya ili kumdhalilisha machoni mwa wapinzani wake.

Kwa kuwa MwenyeziMungu hawezi kufanya makosa au kutoa kauli ya uwongo, panaweza kuwa na ufafanuzi mwingine ambao nao pia unawezekana, na ndio unaoyumkinika zaidi, kwamba chanzo cha funuo zote hizo ni SHETANI aliyeletwa kwa Mirza na 'Eil', 'Tichee Tichee', 'Khairatii'. Naliacha shauri hilo kwa wasomaji.

Katika mfululizo ufuatao, nabainisha baadhi ya mifano thabiti ya uzushi, upotoshaji ya ukweli na uwongo wa waziwazi. Lakini kabla sijaendelea kufanya hivyo, hebu soma kile anachokisema Mirza kuhususiana na mtu anayetunga uwongo:

"Kuongopa si chochote ila ni uasi." (Arba'iin Na.3 uk. 24 tanbihi, Roohani Khazain juz. 17 uk.56, 407).

"Pale mtu anapothibitika kuwa ni mwongo katika jambo moja, basi haaminiki tena katika mambo mengine." (Chashma-e-Ma'arifat uk.222, Roohani Khazain juz. 23 uk.231)

Mirza Ghulam ameeleza katika vitabu vyake kwamba kuna aina aina mbili za ilihamu:

1.Ilihamu kutoka kwa Mungu (Ilham Rehmani)

2.Ilihamu kutoka kwa Shetani (Ilham Shaitaani)

Ilihamu kutoka kwa Mungu, mara zote, ndiyo sahihi. Ilihamu ya Shetani, mara nyingi, ni uwongo lakini inaweza kuwa sahihi nyakati na nyakati pale anapotaka kumpoteza mtu kwa maslahi makubwa zaidi. Funuo/ilihamu za Mirza nazo zikatiwe hukumu kwa msingi huo huo.

Mfululizo wa uzushi Na. 1

Na Dkt. Rashid

Nitauanza mfululizo huu kwa mifano michache kutoka katika maandiko ya Mirza Ghulam ambayo yanahusiana na mambo ya kihistoria na hivyo yanaweza kuthibitishwa na vyanzo huru. Hakuna sherehe inayohitajika, hakuna ulazima wa ufafanuzi, kwa maneno mengine, haya ni maandiko mepezi yanayoeleweka moja kwa moja.

"Wanahistoria wanajua kuwa ndani ya nyumba yake (Mtume Mtukufu saw) walizaliwa watoto 11 wa kiume na wote walikufa...." (Chashma-e-Ma'arifat uk.286, Roohani Khazain juz. 23 uk.299).

"Angalia ndani ya nyumba ya Mtume wa Mungu wasichana 12 walizaliwa, hakusema hata kidogo kwa nini hakuzaliwa mvulana." (Malfuuzaat vol.6 p.57).

"Mtume Mtukufu (saw) hakupata hata nafasi ya kujifunza lugha mama kwa wazazi wake, kwa sababu alipotimiza umri wa miezi sita wote wawili walikufa." (Ayam-us-Sulh uk. 150, Roohani Khazain juz. 14 uk. 396 tanbihi).

Mpendwa msomaji

Fungua kitabu chochote cha sira (historia) au wasifu wa Mtume Mtukufu Muhammad (saw). Alikuwa na watoto wanne wa kiume na wanne wa kike. Hakuna kitabu chochote kinachosema kuwa Mtume (saw) alikuwa na watoto 12 wa kike au 11 wa kiume. Baba yake Mtume saw alikufa kabla yeye hajazaliwa na mamaake akafariki dunia wakati yeye akiwa na miaka 6.

Kipi kilikuwa chanzo cha taarifa za Mirza? Sasa soma hii:

"Chochote nilichokisema, nimekisema kwa amri Yake (Mungu) na sijafanya jambo lolote kwa matamanio yangu mwenyewe na sijamzulia jambo lolote Mola wangu." (Mawahibur Rehman uk. 3, Roohani Khazain uk.19 p.221).

Haya basi ni 'mungu' gani huyu anayetoa taarifa za uongo, akimdhalilisha 'nabii' wake mwenyewe?? Si yawezekana kuwa hizi zilikuwa ni funuo zilizotoka kwa Shetani? Au Mirza alichanganyikiwa? Lakini mbona Mungu hamuachi Mirza na kosa hata kwa pepeso moja la jicho, kama alivyojigamba mwenyewe.

"Bila shaka Mungu katu haniachi na kosa hata kwa punde ya kupepesa jicho; na Hunikinga na kila kosa na Hunikinga na njia za Mashetani". (Nur ul Haq Ukurasa wa mwisho, Roohani Khazain juz. 8 uk 372).

Hata kiwe chanzo gani cha ufunuo huu na hata awe nani nyuma ya ufunuo huu, kuna jambo moja la hakika. Ufunuo huu hautoki kwa MwenyeziMungu, kwa hakika unatoka kwa shetani. Kuna uhakika gani kuwa funuo nyingine hazitoki katika chanzo hicho hicho.

Nawaomba Ahmadiya walitafakari hili.

Wassalaam

Dkt. Syed Rashid Ali

rasyed@emirates.net.ae

http://alhafeez.org/rashid/

تاريخ الاضافة: 26-11-2009
طباعة