عرض المقال :AlFatwa 29
  الصفحة الرئيسية » مـقـالات الموقـــع » كشف البلية بفضح الأحمدية » Non - Arabic Articles » Swahili

اسم المقال : AlFatwa 29
كاتب المقال: webmaster
"MsoNormal">« Sasa Enyi Arya! Hongereni! Ukweli wote kuhusu Mungu wenu (Permashwar) umefichuka ambapo kutokana na ushahidi wa Panditi Diyanand mwenyewe, ni dhahiri kuwa huyo Pershawar wenu ni mwili wa maji ambao hudondoka ardhini kama nafsi nyingine na huliwa kama mboga. Ndio maana wakati mwingine uligeuka kuwa Ramchander, na wakati mwingine uligeuka kuwa Krishna na wakati mwingine, Mara nyingi na mara mojamoja ulionekana kama nguruwe ambaye aliwaburudisha wale waliokuja kumuona kwa kule kula kwake kinyesi » (Roohani Khazain juz. 2 uk.395)

« Permeshwar anapata vidole 10 chini ya kitovu, werevu wataelewa. » (maana yake dhakari...Rashid )  (Roohani Khazain Juz.23 uk.114).

Lugha ya Braheen Ahmadiya ilikuwa chafu mno kiasi kwamba ilikuwa vigumu kwa Mkristo na Wahindu kuisoma bila kughadhibika. Yale mambo ambayo yameandikwa katika lugha ya uchokozi na shari yangeliweza kabisa kusemwa kiungwana. Ulinganiaji huo wa kashfa wa Mirza ukasababisha chuki ya kudumu dhidi ya Uislamu na Mtume Muhammad s.a.w katika nyoyo za Wakristo na Wahindu.

« Mirza Saheb alianza kuwashambuliya Wahindu na wanawake wao katika juzuu za Braheen, vitabu vingine na katika matangazo. Katika ukurasa wa 19 wa kitabu chake, Shuhna-e-Haq, kaandika hivi: « Ninyi hamtanipa mkono wa binti zenu kwani mnachunguza kitu changu”. Katika kitabu chake, Surma Chasme Arya, aliwaelezea wasichana wa Arya kwa lugha chafu na akakashifu masanamu yao. Zaidi ya hivyo akaanza kuwatisha Wahindu kwa funuo zake. Mambo hayo yakawakasirisha Wahindu na yakawa chanzo cha uhasama usiokwisha. » (Asha’at us Sunnah Juz. 18 uk.13-14)

Panditi Lekhram Peshwari wa Arya Samaj alikuwa msema ovyo sana na mtu jeuri. Katika kuijibu Braheen Ahmadiya, haraka sana aliandika kitabu kiitwacho « Takzeeb Braheen. »

« Mirza Saheb alikuwa ametangaza kuwa mtu yeyote asiye Muislamu ambaye angeandika majibu ya Braheen Ahmadiya angezawadiwa Rupia 10,000. Panditi Lekhram akaandika majibu kwa anuwani ya Takzeeb Braheen. Hata hivyo majibu haya ya kishenzi yalijaa kashfa na matusi na naamini kuwa, kwa vile wanadamu tumezaliwa, hakuna mpinga Mungu yeyote aliyewahi kukashifu Manabii na watu wengine waliojikurubisha kwa MwenyeziMungu kama vile Panditi Lekhram alivyoandika katika kitabu chake...

Iwapo mtu ataangalia mizani basi ni dhahiri kuwa Mirza Ghulam Ahmad Saheb ndiye aliyemchokoza Pandit ashambulie Uislamu na Manabii wa Uislamu na yeye ndiye aliyemlazimisha bwana huyo kuandika kashfa hiyo. »  (Raees-e-Qadian p. 1332-133 by Rafiq Dilawari)

Baruwa ya Panditi Lekhram kwa Mirza

Mnamo Juni 24 1893, Panditi Lekhram aliandika haya katika baruwa yake kwa mirza:

« Kama kuandika majibu ya Braheen ni uovu, basi wewe ndiye mwovu wa kwanza, kwani kwa mujibu wa Qur’an wewe ndiye  uliyefanya kufuru, ndiye uliyetuchokoza sisi, kwa sababu hiyo sisi tukaandika majibu. Lau usingetuchokoza, basi Peshwar anajuwa, kuwa sisi hatukuwahi hata kidogo kufikiriya kuandika dhidi ya dini ya Uislamu. Ndiyo kusema, Mungu aepushilie mbali, kama adhabu ya Mungu itashuka basi radi yake ya kwanza itapiga sebuleni kwako kule Qadian. Halafu kama kujitetea ni dhambi basi na mimi pia nilaumiwe. »  (Weekly Satdharam Parcharak, Jallundher, dated 16, July 1897 mentioned in Raees-e-Qadian by Rafiq Dilawari uk.133)

Tangazo la Mirza la kudhihirisha uwezo wake wa kufanya miujiza- Je Manabii wa Mungu wako hivyo?

Kwa kuchapisha Braheen-e-Ahmadiya, Mirza alitumai kuwa utukufu wake ungetangazika katika pembe zote za duniya. Lakini wapi! Aliyoyatarajiya hayakuwa, akapata fadhaa kubwa.  Wanazuoni wa kiislamu wakatowa fatwa kuwa yeye ni Kafiri. Mirza akabalidisha mkakati wake. Kwa kuwa nia ilikuwa ni kuutangazia umma utukufu wake, akaanza kutangaza hizo alizodai kuwa ni nguvu zake za kiroho na uwezo wake wa kufanya miujiza. Mnamo mwaka 1885 alichapisha tangazo na kisha maelfu ya nakala za Kiingereza na Kiudu za tangazo hilo zikasambazwa. Katika tangazo hilo aliwataka Machifu wasio waislamu na Viongozi wa dini wajitokeze kuona miujiza.

« Ikiwa una shaka yoyote kuhusu ukweli wa dini hii au ukweli wa ishara ya mbinguni, basi njoo Qadian ukiwa kama mtu unayetafuta ukweli na ukae na mtu huyu mnyenyekevu kwa MWAKA MMOJA na ujionee kwa macho yako ishara hizi za mbinguni; lakini kwa sharti kuwa uwe na nia (ambayo ndiyo ishara ya mtu anayetafuta ukweli), kwamba baada ya kuziona ishara hizi za mbinguni utatangaza kusilimu au kuthibitisha kuiona ishara isiyo ya kawaida. Endapo utakuja kwa nia hii, basi, kwa hakika, utaiona ishara ya mbinguni. Hii imeahidiwa na Mungu na hakuna uwezekano wa kuikawiza. » ( Collection of Advertisements Juz. 1 uk. 21).

« Onesho hili la miujiza si zao la fikra au uwamuzi wangu, bali limeidhinishwa na Mwenyezi Mungu na ikiwa kama ni bishara habari hii njema imepokewa kwamba wale wanaotumiwa baruwa hii watasutwa,  watashindwa kusema na watanywea. » (Coolection of Advertisements Juz.1 uk. 20).

« Kama utakuja halafu usione ishara yoyote ya mbinguni baada ya kukaa mwaka mmoja, basi utalipwa Rupia 200 kwa mwezi kama malipo ya adhabu au fidiya. » (collection of Advertisements Juz.1 uk.21)

SubHanAllah! Ni uwezo gani huu wa kuonesha muujiza ?

Nani atakayekuwa na muda wa bure wa MWAKA MMOJA.wa kukaa na Mirza Ghulam katika kijiji cha Qadian kilichoachiliwa mbali na Mungu, asahau maisha yake na familiya yake kwa kipindi chote hiki na abweteke MWAKA MZIMA kusubiri kuona ishara zisizojulikana, kwamba hakuna mtu ajuwae lini ishara yenyewe itatokea mikononi mwa Mirza? Na kinachotia shaka juu ya jambo lenyewe ni kwamba ili kujiwekea kinga mapema, mtu huyu ameweka sharti la NIYA ya MTAFUTA UKWELI ili kuiona hiyo ishara ya mbinguni. Ikiwa mtu hazioni ishara za mbinguni, basi kwa kujikinga na lawama, Mirza  anaweza kudai kuwa mtu huyo hakuja na niya ya kutafuta ukweli.

Mwenendo bora wa Nabii wa kweli wa Allah katika mazingira hayo

Je Mtume wa Kweli na wa  Mwisho wa Allah, mtukufu wa daraja, Muhammad (s.a.w) alihitaji  kutowa masharti kama hayo ili kufanya muujiza kwa Makafiri wa Maka? Je aliwahi kuwataka wakae naye kwa mwaka mmoja kusubiri ishara isiyofahamika ambayo eti ingetokea wakati wowote katika kipindi hicho? Hapana. Pale makafiri walipomtaka awaoneshe muujiza, Mtume mtukufu hakusita, hakuweka masharti yoyote na wala hakuwapa muda mahususi. Badala yake aliunyooshea kidole mwezi na ukapasuka vipande viwili. Mduwara mkubwa wa mwezi ukagawanyika vipande viwili mbele ya macho yao. Vipande hivyo viwili vikatengana na kuachana  mbali kabisa kiasi kwamba machoni mwa watazamaji, kipande kimoja kilionekana katika upande mmoja wa mlima na kingine katika upande mwingine wa mlima huo (Taz. Sahihi Bukhari). Kafiri mmoja  akadai kuwa kama vijiwe vingeshuhudia mikononi mwa Mtume(s.a.w) kwamba Muhammad(s.a.w) ni Nabii wa mwisho wa Allah, basi yeye angeukubali ukweli. Papo hapo Mtume mtukufu akaokota vijiwe chini na vikatowa shahada mikononi mwake na yule kafiri akasikia. Hapakuambatanishwa masharti, haukupangwa muda mahususi, na hapakuwa na sharti la niya. Kufikisha ukweli lilikuwa ni jukumu lake ama mtu anayefikishiwa akubali au asikubali, hiyo ndiyo ilikuwa jitihada yake ya mwisho, kwani uwongofu uko mikononi mwa Allah. 

Huo ndio ulikuwa mwenendo mtukufu wa Mtume Muhammad(s.a.w), Nabii wa kweli na mwisho wa Allah. 

Kwa ainisho lake muujiza ni jambo liendalo kinyume na kanuni za maumbile, jambo linalokwenda kinyume na akili ya mwanadamu, jambo ambalo wanadamu hawana kabisa uwezo wa kulifanya au kulielewa. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Muumba na Mola wa ulimwengu wote, miujiza ilifanywa na Manabii wake wa kweli kudhihirishiya umma heshima na utukufu wa Mitume yake, kuwaonesha wao wenyewe kuwa Allah yupamoja nao na kwamba yule ambaye ameumba kanuni za maumbile ana uwezo wa kuzigeuza kanuni hizo. Miujiza ilifanywa papo kwa hapo. Pasipokuambatanishwa na masharti, ili kuwashinda Makafiri na kuwaongezea Imani wale waliomuamini Mtume. Nukta nyingine muhimu kukumbuka ni kuwa hakuana Nabii yeyote wa Allah aliyejisifu kwa miujiza hii achalia mbali kuitangaza. 

Lakini Mwenendo wa wazushi ulikuwa ni kinyume kabisa na huu, kama ilivyobainishwa hapo juu na kama wasomaji watakavyoona katika kurasa zifuatazo.

Barua ya Pandit Lekhram kwa Mirza Gulam.

Punde tu Pandit alipoliona tangazo, akamshambulia Mirza kufichuwa urongo wa madai yake.  Tayari Pandit huyu alikwisha ghadhibishwa kwa namna Mirza alivyoikashifu Dini ya Uhindu na vitabu vyake, na akaona hii ndio fursa muhimu ya kuripiza kisasi chake.  Akamuandikia barua Mirza na kuelezea niya yake ya kukaa Kadiyani.  Aliandika hivi:

« Nimeiona barua yako iliyochapishwa na Murtazai Press Lahore.  Katika barua hii umeagizwa na Mungu kuandika kuwa mtu yeyote wa Dini nyingine, ambaye licha ya kukaa na wewe kwa mwaka mmoja, bado haioni ishara yoyote ya mbinguni na asilimu baada ya kutoshelezwa nafsi yake, basi wewe utamlipa lupia miambili kwa mwezi yakiwa ni malipo ya adhabu au fidiya. Hivyo basi, ili kuweza kuiona Ishara hiyo ya mbinguni mimi nipo tayari kuja kwako kwa sharti kwamba katika lile dau la rupia miambili kwa mwezi weka rupia 2400 katika Bank ya serikali ili zihifadhiwe natowa maelezo ya maandishi kuwa kama mimi sitatoshelezwa na sitaingia katika Uislamu baada ya mwaka mmoja wa uongozi wako na ishara ya mbinguni na miujiza, basi rupia hizo 2400 zitakabidhiwa kwangu, na kwa kipindi cha mwaka mzima pesa hizo zitaendelea kuhifadhiwa katika Benki ya serikali, wewe hutakuwa na haki ya kuzichukuwa tena pesa hizo.  Nakubali kuwa mwanafunzi wako kwa mwaka mmoja. » (Letter to Mirza Gulam dated 3rd April 1885, Menentioned in Raees-e-Qadian by Rafiq Dilawali P.163-baruwa kwa Mirza Gulam, Tarehe 3 Aprili 1885, imetajwa katika Raees-e-Qadian ya Rafiq Dilawali uk163).

Majibu ya Mirza Gulam - masharti ya mtego.

Mirza Gulam yumkini atakuwa amekasirishwa sana na majibu ya Pandit Lekhram. Kama ilivyokuwa ada yake, akaanza kumtega Pandit kwa masharti ya kumkwamisha, hii ikiwa ni jitihada ya kumkwepa.  Aliandika hivi:

« Katika ile baruwa yangu iliyochapishwa mimi nimewaalika wale watu ambao ni wanazuoni wa kuheshimika na viongozi mashuhuri kwa jumuiya zao, ambao kukubali kwao kwaweza kuathiri kundi kubwa la watu, lakini wewe si mtu mwenye nafasi au hadhi hiyo, na kama mimi nakosea kwa fikra hii na kwamba wewe kweli ni kiongozi wa jumuiya yako basi vizuri sana, sitaki kukupa shida sana, wewe fanya hivi, kwamba wanajumuiya wote wa jumuiya tano, Arya Samaji Kadiyani, Arya Samaji Lahore, Arya Samaji Amritsar, Arya Samaji Ludhiana, Arya Samaji Peshawer, wote miongoni mwao watoe maelezo ya maandishi kwa kiapo kwamba Pandit Lekhram ambaye ni kiongozi wetu, kama akishindwa katika jambo hili na akaiona ishara fulani basi sisi sote tutasilimu bila kusita.  Ikiwa utakusanya maelezo haya na kunitumia ndani ya kipindi cha majuma mawili basi wewe utaonekana ni mtu wa kawaida tu ambaye hustaili kualikwa. » (Letter of Mirza Gulam Dated 17th, April 1885, Menented in Raees-e-Qadian by Rafiq Dilawali uk 163).

Majibu ya Pandit Lekhram

« Methali inayoswihi kwako ni hii: Meno ya tembo yafaa kwa shoo na si kwa kutafunia.  Na mimi nilidhani kuwa kwa mujibu wa maudhui ya barua yako wewe utatimiza ahadi yako, lakini kumbe nilikosea. Kauli yako kuwa mimi nipate maelezo ya maandishi kutoka kwa wanajumuiya wa jumuiya ya tano za Arya Samaji (za miji mitano) inathibitisha kuwa methali hiyo ni sahihi kwamba « warongo wanasababu na visingizio vingi. » Wanajumuiya wa Jumuiya tano za Arya Samaji wanawezaje kulazimishwa kusilimu kwasababu ya kushindwa kwangu na kuukubali kwangu Uislamu? Hebu jaaliya wewe unakuwa Arya, je kaka yako, ndugu zako wa nasaba na Waislamu wengine wa Kadiyani nao wataingia katika Dini ya Arya?  Abadan. Mirza Sahil? Visingizio visivyo na kichwa wala miguu havileti chochote ila kero tu.  Ikiwa wewe utafanya uchunguzi kamili na kuikubali dini ya Arya, basi hicho ndicho kitakachokuwa kielelezo cha ukweli wa dini ya Arya.  Halikadhalika Mtu kama mimi kuwa Muislamu itakuwa ni Ishara ya wazi ya Muujiza wa Dini ya Uislamu. Kwa vile urongo wa madai yako ya kufanya muujiza umekwishafichuka bayana kwangu mimi kupitia Arya Samaji ya Kadiyani basi kwakweli nisingeiga msemo usemao, “kumtahini mtu aliye mtihanini ni ujinga.” Hata hivyo ningependa kusema wazi kwamba wewe kwa makusudi unakwepa na kulipiga chenga swala hili.” (Barua ya Mirza Gulam ya tarehe 9 April 1885, imetajwa katika Raee-e-Qadiyani ya Rafiq Dilawali uk 164).

Kisingizio kingine cha Mirza

« Rupia 200 kwa mwezi zilitengwa kwaajili ya watu wenye hadhi kubwa.  Iwapo nitaweka rupia 200 kwa watu wa hadhi ya juu na ya chini, sasa mimi nitapata wapi kiasi chote hiki cha fedha? Kama unapata kiasi hiki cha fedha kutoka sehemu nyingine basi mimi sina pingamizi. Thibitisha tu kuwa wewe ni mtu wa hadhi....Ni wajibu kwako wewe kuja Qadiyani ili uepukane na fikra hii mbaya nauthibitishe ukweli wa jambo hili. » (barua ya Mirza Gulam ya tarehe 16 Aprili 1885, imetajwa katika Raees-e-Qadiyani ya Rafiq Dilawali uk 163). 

Msisitizo wa Lekhram.

« Mirza Saheb? Maana ya barua yako uliyochapisha mara ya kwanza ilikuwa nyingine kabisa, barua yako ya April 7 inasema kitu kingine na barua yako ya April 16 inaelezea kitu kingine tofauti kabisa.  Mungu anajuwa, kwanini wewe unazikwepa kauli zako.  Ombi langu ni kuwa kama kweli wewe ni mkweli katika ahadi yako na ni mtafiti wa ukweli, na mtafutaji wa uongofu na kama umeteuliwa kwaajili ya uongofu wa wanadamu, basi weka rupia 2400. Katika lile dau la rupia 200 kwa mwezi katika Benki natowa maelezo ya maandishi kwamba kama mimi sitoshelezwi na siukubali Uislamu baada ya mwaka mmoja wa uongozi wako na ishara ya mbinguni na miujiza, basi hizo rupia 2400 zitakabidhiwa kwangu, na kwa kipindi cha mwaka mmoja kiasi hicho cha fedha kitaendelea kuhifadhiwa katika Benki ya serikali. Kama kweli wewe umeteuliwa na Mwenyezi Mungu, kwanini basi unasiti kutoa maelezo hayo ya maandishi na kuweka kiasi hicho.  Wakati ambapo ukweli haupaswi kufifilizwa na wewe una Imani kamili na miujiza yako basi ni upuuzi kuuepuka. Kama Mungu amekufahamisha na ameifanya bishara hii, na wewe, kwa mujibu wa kauli yako mwenyewe umethibitisha bishara zako mara nyingi, basi mimi kwa hakika nitaponzeka, nitashindwa na nitafungwa mdomo. Mungu amekuahidi wewe na wewe sasa unakwepa kutimiza ahadi hii. Sasa yawezaje kukubalika kuwa swala la kusitasita (kulisiya lisiya) halipo juu ya jambo hili, wakati wewe mwenyewe huna imani nalo kamili. Madai ya kukoma kwa mzunguuko wa dunia na kutowa tangazo kwamba pale jua litakapochomoza upande wa magharibi basi wewe ndipo utakapolipa kiasi hicho, yanatia dowa jeusi kwa mtu mwerevu kama wewe. Ni kwasababu hiyo ya kukiuka ahadi zako ndiyo maana hakuna jamaa yeyote wa Arya aliyetayari kuja kwako. Mimi nakuandikia tena na tena kwamba ili kuthibitisha uwezo wa kufanya miujiza, mimi najitolea nafsi yangu kama mtihani na kwa moyo wa dhati kabisa nakubali kuwa mwanafunzi wako na kukaa Qadiyani kwa mwaka mmoja. Kama safari hii utalikwepa tena swala hili basi maandikiano hayana maana tena. » (Baruwa ya Mirza Gulam ya April 30 1885 iliyotajwa katika Raees-e-Qadiyani ya Rafiq Dilawali uk. 164).

Mirza ajibu-Sharti jingine tena

Pale Mirza alipotanabahi kuwa Lekhram hatoacha msimamo wakekwa ghalama yoyote, akakubali kuweka pesa Benki lakini kwa sharti jingine:

« Kwa upande mmoja mtu huyu mnyenyekevu ataweka rupiya 2400, na kwa upande mwingine wewe pia utaweka kiasi hicho hicho kwa matakwa yangu katika duka la Muhajin (Muhajin ni mmiliki wa duka vijijini ambaye hutowa mikopo kwa riba), kama adhabu ya kukataa kuukubali Uislamu, ili yeyote anayepewa ushindi na Mungu hii itakuwa zawadi ya ushindi wake. »  (Baruwa ya Mirza Gulam ya Julai 17 1885, imetajwa katika Raees-e-Qadiyani ya Rafiq Dilawali uk. 163).

Majibu ya Lekhram

« Msingi wa maandikiano yetu ni lile tangazo lako ulilolichapisha katika Murtazi Press Lahori ambamo ulikuwa umedai kwa maneno ya wazi kuwa Mungu amekuamrisha wewe kuwaita watu wa dini nyingine katika Uislamu na yeyote akaaye na wewe kule Qadiyani kwa mwaka mmoja na baada ya kuona ishara ya mbinguni na muujiza bado asisilimu, wewe utamlipa fidiya ya rupiya 200 kwa mwezi, kiasi cha rupiya 2400 kwa mwaka mzima.  Baada ya hili mimi nikakuomba wewe kuwa niko tayari kukaa nawe kwa mwaka mmoja. Mbona sasa wewe umeweka sharti jipya ... Ndugu yangu wee? Kwanini unazipiga chenga ahadi zako mwenyewe zilizotangazwa hadharani na kwanini wewe umeutupa uadilifu?  Je huu ndiyo mwenendo wa watu wa dini na watu walioongozwa katika njiya sahihi? Ni jambo la uadilifu  kwamba wewe kwanza uchapishe tangazo hili kuwa kile ulichokitangaza awali, sasa unakifutilia mbali.  Wakati ulipokuwa umetangaza muujiza wako, ungelikuwa na imani thabiti kwamba pasiposhaka utaufanya muujiza huo na athari zake zingetokea pao hapo na yeyote ambaye angeshuhudiya basi kwa hakika angeukubali Uislamu.  Maana ya Kiistilahi ya muujiza ni kumfanya kila mtu aondokewe na uwezo. Kama mpinzani aondokewi na uwezo na hashindwi basi huo hauwezi kuwa muujiza. Hii inaonesha kuwa wewe mwenyewe unashaka na muujiza wako kwamba mtu huyu (Lekhram) hatopatilizwa kwa muujiza wako. Ndiyo maana unatowa sharti jingine hata hivyo kulingana na kanuni « mwendee muongo hadi nyumbani kwake », mimi bado nipo tayari kulikubali sharti hili jipya, kama unavyofanya wewe mimi piya nitaweka rupiya 2400. »  (Baruwa kwa Mirza Gulam, ya Julai 20 1885 imetajwa katika Raees-e-Qadiyani ya Rafiq Dilawali uk. 168).

Baada ya kulikubali sharti jipya Lekhram akamuandikia tena baruwa Mirza Gulam:

« Kwakuwa mimi nautiliya shaka msimamo wako basi eleza wazi ni aina gani ya ishara utakayoifanya...... Pia weka tarehe maalumu na muda makhsusi wa kuonesha muujiza wako ili ipate kutangazwa. » (Baruwa kwa Mirza Gulam, Julai 20 1885, imetajwa katika Raees-e-Qadiyani ya Rafiq Dilawali uk.168),

Mirza afanya jitihada nyingine kumpiga chenga Lekhram

« Mimi siwezi kuweka sharti lolote katika kuonesha muujiza na wala siwezi kuonesha huo muujiza unaodaiwa.  Mimi sijuwi nini kitakachotokea. Mimi ni mja niliyeteuliwa.  Sijuwi kwamba ni aina gani ya ishara atakayoionesha Mungu.  Hatujuwi na hatuelewi kama ishara hiyo ni ile ambayo iko nje ya uwezo wa binadamu.  Sisi tunadai tu kuwa Mungu bila shaka ataonesha ishara hiyo kwa kile ambacho wanadamu hawana uwezo nacho, lakini SHARTI ni kwamba ili kutowa jibu la YES (ndiyo) au No (hapana) kuhusiana na muujiza wetu, wateuliwe majaji wanaokubalika kutoka pande zote mbili ambao hawahusiani na Dini ya upande wowote kati ya pande hizi mbili. »  (Baruwa ya Mirza Gulam iliyotajwa katika Raees-e-Qadiyani ya Rafiq Dilawali uk. 170)

Lekhram amcharukia Mirza Gulam

« Kama wewe ungetaka upande wa pili nao uweke pesa, basi ungelitaja sharti hili katika tangazo lako la kwanza kwamba mithili ya mcheza kamari weke dau dhidi ya dau langu, ili baadaye masharti yasibadilike na kufutwa. Kama ungeandika hivyo wazi wazi basi hata mtu mwenye akili ndogo asingetilia manani mchezo huo wa kamari achiliya mbali mimi kupata usumbufu wa kukuandikia wewe. Sababu ya kutoziamini ahadi zako ni majigambo yako yasiyo na msingi na visingiziyo vyako visivyo na msingi.....Ukweli ni kwmaba wewe umeyafanya majigambo yako kuwa chanzo cha kujipatiya chumo.  Ni kwasababu hizi mimi nilikuomba uweke Banki mapema kile kiasi ulichoahidi. Haukuwa sahihi kudhani kuwa kwa yale masharti yako magumu basi pasingekuwa na mtu ambaye angependa kuwa kifungoni bila pingu kule Qadiyani kwa mwaka mmoja, kuwa miongoni mwa wakulima na watu mbumbu wa huko; na zaidi ya hivyo ni kwamba kama asingekuwepo mtu wa kujibu basi madai yako yangekubalika upande mmoja. Lakini pale mimi niliposimama kidete kukosowa dai lako na kwasababu ya sababu zilizotajwa kujaribu kupata fidiya iliyoahidiwa mapema, kinyume na tangazo lako umebuni mbinu mpya ya kukwepea....

Kwa kusema kuwa « mimi ni mtumishi niliyeteuliwa tu » na sehemu kubwa ya kile ulichokiandika katika mistari ya mwanzo ya tangazo lako, ni dhahiri kabisa kuwa wewe unadai Utume, na kwa kuandika jina tukufu la Nabii Issa, umejielezea mwenyewe kuwa uko sawa naye. Haitakuwa nje ya mada kuvuta hisiya za    wanazuoni wa kuheshimika wa Kiislamu, kwasababu ni dhahiri kama lilivyo jua kwa Waislamu makhususi na Waislamu wa kawaida kwamba Nabii Muhammad ni Mtume wa mwisho.  Sasa basi kwanini hawatowi fat-wa juu ya mtu huyu, kwani maaduwi wa ndani huleta madhara makubwa na nyoka aliyenguoni ni hatari zaidi.  Kauli yako (kauli ya Mirza) kwamba mimi sijuwi aina ya ishara atakayoionesha Mungu haina mashiko kabisa. Kwa namna wewe ulivyoteuliwa kwa utumishi muhimu na kwa jukumu kubwa, kwanini basi hujafahamishwa siri za Utume wako?  Na kama hujuwi aina ya ishara itakayooneshwa kwanini basi ulitangaza dai la kuonesha ishara ya mbinguni bila Mungu kusema hivyo? Ikiwa Bismillahi ya ufunuwo wako yenyewe tu ni batili, nini utakachoambuliya hapo? Ni dhahiri kuwa kwa ujinga huu, kukuteuwa wewe katika hadhi kubwa ya Nabii hakuwezi kuwa kazi ya Mungu, mjuzi wa mambo yote yaliyofichikana.  Hii ni kazi ya mtu mwingine  (Shetani). Mimi nilikuwa nimekuomba wewe uoneshe ishara zilizo nje ya uwezo wa kibinadamu, hatukukuomba kingine chochote. Lakini bado wewe umelikwepa hilo. Na sasa umeitupa nusu ya dai lako, katika ILE ISHARA YA MBINGUNI umebakiwa na nusu tu,  na hii nusu ya pili ambayo ni ISHARA nayo piya umeifunika, kwani hujui ni kwa namna gani na wakati gani itakuwa. Kwa hiyo dai lako limekuwa batili kabisa. Mwishoni kabisa umebainika. Baada ya kushindwa yote haya, sijui kwanini tena wewe unaweka sharti hili kwamba ili kutoa jibu la NDIO au HAPANA basi wateuliwe Majaji. Ni kweli kwamba pale kesi inapoendeshwa, jambo lenye hatihati nalo huwasilishwa mbele, hapo unahitaji Majaji. Lakini kwa vile wanadamu hawana ilimu ghaibu, (majaji nao) piya wanapapasa gizani. Kama muujiza wako ni wa hati hati namna hiyo, bora basi uoneshe miujiza hiyo kwa wachunga mbuzi na utuombe radhi sisi. Badala ya kuona muujiza wako wa majigambo, sisi tunapenda kubakia kimya »(baruwa kwa Mirza Ghulam ya Agosti 5 1885, iliyotajwa katika Raees-e-Qadian ya Rafiq uk.171-172)

Mirza amuomba Pandit kwenda kukaa Qadian

« Mirza Ghulam alifungwa mdomo na bwana huyo, akona ni busara kutojibu. Baada ya miezi mitatu Pandit akaandika postikadi yakukumbushia. Katka majibu, Mirza naye akatuma postikadi ambapo aliandika kuwa Qadian si mbali sana, njoo ukutane nami, yatumainiwa katika mkutano huu masharti haya yatamalizwa. » (Takzeeb Braheen-e-Ahmadiya by Pandit Lekhram, mentioned in Raees-e-Qadian by Rafiq dilawali p. 171-172).

Maandikiyano haya  baina ya Mirza saheb na Panditi yalidumu kwa miezi mitano. Yalichapishwa katika magazeti mbalimbali ya Punjab, kwa mfano Aaftaab Punjab, Kohinur na mengineyo (Takzeeb Braheen-e-Ahmadiya by Pandit Lekhram p.331, mentioned in Raees-e-Qadian by Rafiq Dilawari p.171-172)

Kwa kuwa Mirza alishindwa wazwazi na kudhalilika hadharani katika maandikiano haya, maandikiano haya hatuyaoni katika maandiko ya Ahmadiya. Takzeeb Braheen na toleo lake la ziada (Zameema) yalichapishwa enzi za uhai wa Mirza Saheb, aliyasoma na kulalamikiya lugha kali ya Pandit katika vitabu vyake kadhaa. Pale maandikiano haya yalipochapishwa katika Zamiima (Toleo la ziada) la Takzeeb, Mirza Saheb hakuweza kuwa na ujasiri wa kukanusha.             

Pandit Lekhram atinga Qadian

« Punde tu Panditi alipopata mwaliko, haraka akawasili Qadian na kuanza kuyazungumziya yale masharti. Kwa mara  nyingine akaanza kupiga chenga na kulikwepa suwala hili. Bahati mbaya kwake, Panditi hakuwa mtu wa kumwachiya kwa namna yoyote ile. Akamng’aninia kooni kama ndege wa baharini albatross. Kila Mirza alivyojitahidi kumkwepa, Panditi Lekhram, ambaye alitumikia jeshi la polisi kwa miaka mingi hakumwachia achomoke kwenye ndowano. Siku moja Panditi alikuwa amekaa ndani ya nyumba ya Mirza akitimiza masharti ya kukaa Qadian kwa ajili ya kuziona ishara za mbinguni. Wakati wa maongezi neno « Khawariq-E-AADAAT » (kinyume na maumbile) likaibuka katika mazungumzo. Pandit akasema:

« Khawariq-e-Aadaat » maana yake kukiuka maumbile. Kisu kimepewa uwezo wa kukata, moto huunguza chochote kinachotumbukizwa humo, miti huota ardhini. Iwapo kwa amri ya Mungu wewe (Mirza) utavunja kanuni hii, yaani kama muujiza wako unazuia kisu kukata au unazuia moto kuunguza kitu kilchotiwa humo. Au mti uanze kutembea ardhini, basi mimi nitakuwa Muislamu. Ikiwa hutaweza kufanya muujiza huo, basi wewe uwe Arya na uwache kutowa madai ya uongo. »

Mirza Saheb akasema:

« Kwa istilahi ya Qur’an hii siyo maana ya Muujiza »

Naye Panditi akasema:

« Ikiwa neno hili halikutajwa hata katika Qur’an, hoja ya istilahi ya Qur’an yawezaje kuwa sahihi ilihali neno lenyewe halimo hata katika Qur’an »

Mirza Saheb akazidi kusisitiza kuwa neno hili limetajwa katika Qur’an. Pandi Lekhram mwenyewe akampa Qur’an Mirza Saheb na kumuomba: « Kwa ridhaa ya Mungu hebu nioneshe ni wapi ndani ya Qur’an neno « muujiza » limetajwa? (Ni kweli kwamba neno hili halikutajwa katika Qur’an, bali badala yake neno « JAMAAT-sign » ishara ndilo lililotumika.... Rashid). Mirza Saheb akafunuwafunuwa kurasa za Qur’an tukufu kwa dakika chache lakini hakuweza kuliona neno hilo. Mwishowe akaacha na kusema: nalirudi dai langu, kwa kweli neno hili halimo ndani ya Qur’an. Pandit Lekhram akaandika katika kitabu chake kuwa wakati huo Hakiim Kitten All, ALA Inhale Chained, Pandit Jai Kitten, ALA Lax Sahib, binamu yake Mirza Saheb Mirza Kamaluddin, Mince Mural Ali na Msafiri mmoja mtu mzima walikuwa wamekaa nasi. Inatumainiwa kuwa Mirza saheb hatolikanusha tukio hili.  » (Takzeeb Braheen-e-Ahmadiyya by Pandit Lejkhram p.86, mentioned in Raees-e-Qadian yan Rafiq Dilawari p. 172-173)

Shutuma za Pandit Lekhram na Fedheha ya Mirza

Panditi alifanya jitihada zote ili ilhaami Saheb (Mirza) aache kupiga chenga na akubali kwa masharti ya haki na ya kisheria kukaa kwake Qadian mwaka mmoja. Lakini hakuweza kumleta Mirza katika mazungumzo yenye mizani ya hoja. Hatimaye akaacha kuzungumzia masharti ya kukaa Qadian. Badala yake akaanza kudai kufanya muujiza wa papo kwa hapo. Kila siku Panditi Lekhram akawa anakwenda nyumbani kwa Mirza na kusema: Kama kweli wewe ni mkweli katika madai yako,  basi onesha muujiza fulani. Masikini wee, Mirza hakuwa na cha kuonesha isipokuwa kuinamisha kichwa kwa fedheha kwani kufanya muujiza ni jambo lililoshindikana kwa mzushi. Wakati huo huo, Panditi akafanya mkutano wa hadhara wa mamia ya Wahindu (Arya) katika soko la Qadian na kutowa maneno makali na kumkashifu Mirza na hiyo imani yake, watu wakawa wanachekea nyoyoni kisha Panditi akarejea kwao. Mirza Sahib akalilalamikia kwa uchungu tukio hili zima katika kitabu chake, « Faryaad-e-Dard ». Kwa mfano aliandika hivi:

« Katika siku zile ambazo Lekhram alipania kuutusi Uislamu ambapo katika kila sentensi alitumia matusi matupu, kwa jazba yake, akaja pale Qadian na kukaa mwezi mmoja ili abishane nami. Mimi sikuwahi kwenda kijijini kwake kulumbana nae wala sikuwahi kuanzisha maandikiano ya baruwa na yeye. Yeye mwenyewe ndiye aliyekuja Qadian na jazba yake ya kihayawani, na Wahindu wote wa hapa ni mashahidi kwamba alikaa kwa takriban siku ishirini na tano hapa Qadian na hata siku moja hakuweza kujizuiana lugha  kali na ya kashfa mno. Sokoni kwenye uwanja wa Waislamu, alikuwa akiporomosha matusi kwa Mtume Mtukufu s.a.w na akatumia maneno ya kuwachokoza Waislamu. Kwa kuchelea kuvurugika kwa amani, mimi nikawaagiza Waislamu wasisimame sokoni wakati wa hotuba zake na asithubutu mtu yeyote kumkabili. Hivyo licha ya ukweli kwamba kila siku yeye alikuwa tayari kuleta fujo akishirikiana na wahuni fulani, lakini kwa sababu ya nasaha zangu za mara kwa mara, Waislamu walijizuia na ghadhabu.Waislamu kadhaa wa kuheshimika wakawa wananijia nyumbani siku hizo wakilalama kuwa mtu huyu (Panditi Lekhram) anamkashifu Mtume wetu Mtukufu(s.a.w) hadharani nami nikaona walikuwa wamekasirishwa sana, basi mimi, kwa upole nikawanasihi kuwa huyo ni msafiri (mpita njia tu), amekuja kubishana, nyie tulieni. Kwa kuwazuia kwangu mara kwa mara, wakajizuia na hasira. Na Lekhram akawa na kawaida hii kwamba, kila siku alikuwa akija nyumbani kwangu na kutaka aone ishara au muujiza, na maneno ya kashfa na ya kifedhuli kwelikweli yakawa yanamtoka mdomoni. Mara nyingi alikuwa akija asubuhi au jioni,  akikashifu Uislamu na kumkashifu Mtume s.a.w kwa namna mbalimbali ambapo kama walivyovumisha Mapadri katili wa Kikristo, mara kwa mara alikuwa akisema kuwa « Mtume(s.a.w) hakufanya miujiza yoyote wala bishara zake hazikutimia; ila tu kwa kuitukuza dini yenu Mamulla wamejaza vitabu kwa miujiza feki: » (Faryad-e-Dard by Mirza Gulam P. A, Maentioned in Raees-e-Qadiyani by Rafiq Dilawari P. 175-176)

Kushindwa kwa Mirza kufanya muujiza.

Swali hapa ni kuwa wakati Pandit Lehram alipokuwa akimkashifu Mirza hadharani, akiutusi Uislamu na akimkshaifu Mtume(s.a.w) mbele ya Mirza Gulam na tena ndani ya nyumba yake, Pandit Lekhram kila siku alikuwa akitaka aoneshwe muujiza. Kama kweli Mirza Gulam alikuwa na uwezo fulani wa kufanya miujiza (kama alivyodai katika matangazo yake mwenyewe)  Ni nini basi kilichomzuwia kuonesha muujiza huo wote?  Ni nini kilichoisibu heshima ya Mtume(s.a.w)? Kwanini yeye hakumpatiliza Pandit ambaye, kila uchao na kila uchwao alikuwa akitowa Kashfa mbaya mno dhidi ya Mtume(s.a.w)?  Baada ya kudai (kwa ile inayoitwa idhini ya Mungu kuwa anao uwezo wa kufanya muujiza, kwanini hakumkata kilimilimi Lekhram, ili wengine wapate fundisho?  Dai lifuatalo la Mirza liko katika kumbukumbu: 

« Kwa kulinganisha na Manabii waliotangulia mimi ndiye mwenye miujiza na bishara zaidi, zaidi ya hivyo hakuna mlingano baina ya miujiza na bishara za Manabii waliotangulia na miujiza na bishara zangu:  Isitoshe bishara na miujiza yao hivi sasa imebakia hadithi na visa vitupu, lakini miujiza na bishara zangu mimi imeonwa na maelfu ya watu na ni mikubwa na mitukufu zaidi kiasi ambacho hakuna mwingine yeyote unaoweza kuonekana mkubwa zaidi kuliko hiyo; yaani maelfu ya watu katika duniya ni mashahidi wa miujiza hiyo, lakini kwa miujiza na bishara za Manabii waliotangulia hakuna hata shahidi mmoja aliyehai, ispokuwa kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) ambaye miujiza na bishara zake mimi  ambaye niko hai ni shahidi wake na Qur’an tukufu ambayo bado ipo ni shahidi wake. Na mimi ndiye yule, ambaye kwa baadhi ya miujiza yake na bishara zake kuna mamilioni ya mashahidi. » (Statement of Mirza Gulam, Rohan Hazayn Vol. 18 p. 460- 461).

Hata hivyo, ushahidi wa vitendo wa dai hili ulikuwa ni kwamba, licha ya kubanwa  na aduwi wa Uislamu, bado Mirza hakuweza kufanya hata muujiza mmoja. Ni dhahiri kuwa kama kungelikuwa na chembe ya ukweli katika madai yake ya kuteuliwa na Mungu au  madai ya kuwa na uwezo wa kufanya muujiza au madai ya kuwa Mungu amemuahidi kuwa ishara ya mbinguni itaoneshwa mikononi mwake, basi katika wakati huo mgumu ambapo aduwi wa Uislamu. Alikuwa akiuponda Uislamu na kumshambulia Mtume(s.a.w), hapakuwa na sababu kwanini Allah, pale pale asioneshe ishara mikononi mwa  Mteule wake? Si hivyo tu kwamba hakuweza kuonesha muujiza wowote bali hakuweza hata kumpatiliza kwa laana aduwi huyu wa Uislamu kwa maneno yake.  Aliwazuiya hata wengine kukabiliyana naye.  Hii inathibitisha kuwa madai yake yote ya kuteuliwa na Mungu, kuambiwa na Mungu kuwa ishara za Mbinguni zingeweza kuonekana Qadiyani au yeye kuweza kufanya miujiza hayakuwa chochote bali ni kuidanganya tu nafsi yake.  Kwa vile alikuwa  ametunga uongo juu ya Allah,  hivyo kwa makusudi alimshushiya heshima Allah mikononi mwa aduwi huyu wa Uislamu.  La haula! Mirza hakuweza kusoma maandiko au hati ukutani. 

Silaha nyingine ya Mirza – mwito wa mubahila na Arya

Baada ya kushindwa kwa fedheha mikononi mwa mshirikina na kafiri (Lekhran, mnamo mwaka 1886 Mirza aliandika kitabu kilichoitwa ‘Surma Chashm-e-Arya.’ Katika kitabu hiki akawaalika viongozi wa Arya katika duwa ya maapizano (Mubakhila.  Aliandika kuwa atahara za maapizano haya zingetokea ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. Insha Allah katika toleo lijalo la Alfa-twa tutasoma sehemu iliyobaki ya kisa cha Lekhran ambacho kiliishiya kwa mauaji ya Lekhran.

Wassalam

Dr.  Syed Rashid Ali

May 2003

P O Box 11560, Dibba Al-Fujairah, United Arab Emirates.

rasyed@emirates.net.ae

http://alhafeez.org/rashid/

 

الصفحات[ 1] [2]
اضيف بواسطة :   admin       رتبته (   الادارة )
التقييم: 0 /5 ( 0 صوت )

تاريخ الاضافة: 26-11-2009

الزوار: 4592


المقالات المتشابهة
المقال السابقة
AlFatwa 28
المقالات المتشابهة
المقال التالية
Shatam
جديد قسم مـقـالات الموقـــع
القائمة الرئيسية
البحث
البحث في
القائمة البريدية

اشتراك

الغاء الاشتراك