عرض المقال :AlFatwa 29
  الصفحة الرئيسية » مـقـالات الموقـــع » كشف البلية بفضح الأحمدية » Non - Arabic Articles » Swahili

اسم المقال : AlFatwa 29
كاتب المقال: webmaster

Bismillah Al-Rahman Al-Rahim

 Anti Ahmadiyya Movement in Islam

Al- Fatwa  International  No  29

(Imetafsiriwa kutoka lugha ya Kiingereza)

Waheshimiwa Wasomaji,

Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh.

Toleo hili jipya la Al-fatwa sasa linafikishwa kwenu.

Imam wa Jumuiya ya Ahmadiya, Mirza Tahir Qadiani afariki duniya.

Yule aliyeitwa Imam na Khalifa wa Kujitawaza wa Jumuiya ya Ahmadiya, Mirza Tahir Ahmad Qadiani alifariki duniya mnamo Aprili 19 2003. Kila mtu lazima afe siku yake ikifika, lakini vifo vingine ni fundisho kwa wengine.

Mnamo mwaka 1988 Mirza Tahir Ahmad alitowa chagizo la Mubahila (duwa ya maapizano) kwa Umma mzima wa Waislamu, akiwaita makafiri na waongo. Changamoto hii ya Mubahila ikamueleleza Mirza. Ilimtiya matatani na kumuweka katika hali ngumu ambayo hakuweza kujinusuru nayo kamwe na hatimaye ikamtowa uhai.

Baada ya kutowa changamoto hii, Mirza aliishi kwa kujificha lakini wanazuwoni wa kiislamu wakayafanya maisha  yake yawe ya moto kwa kumchagiza mara kwa mara kufanya naye duwa ya maapizano. Wanazuwoni wengi waliikubali changamoto yake na wakamwita katika duwa ya ana kwa ana ya maapizano ( kama ilivyokuwa Sunna ya Mtume Muhammad s.a.w). Said Abdul Hafiiz Shah aliyeanzisha harakati dhidi ya Ahmadiya mwaka 1991, naye pia aliikubali changamoto ya mubahila (duwa ya maapizano) lakini Mirza Tahir hakuwa na ujasiri wa kukabiliana na yeyote katika duwa ya maapizano. Kutokea kwenye jukwaa la harakati dhidi ya ahmadiya, mimi nikamchagiza Mirza kufanya naye Mubahila katika miaka ya 1994, 1995, 1997, 1998 na 2000, lakini Mirza Tahir alipiga kimya kiasi kwamba alishindwa hata kulijibu tu chagizo hilo  achililiya mbali kulikubali. Sheikh Manzoor Ahmed Chinioti amekuwa akienda London kila mwaka tangia mwaka 1989 na amekuwa akimchagiza Mirza kujiapiza kwamba yeye (Mirza Tahir) hakuwahi kufanya mambo ya kishoga (ubaradhuli). Ni muhimu kukumbuka kuwa baba yake Mirza Tahir, Mirza Bashiruddin Mahmud, Khalifa wa pili, alikuwa mzinzi, Muhuni, baradhuli wa kutupwa ambaye hakuacha kumpitiya hata binti yake wa kuzaa na hakuwaacha hata ndugu zake ambao kwa sheriya ya dini ya ufunuo, ni haramu hata kuwaoa. Lakini wapi? Mirza Tahir amebakia kujificha nyumbani kwake Gressenhall.  Mfuwasi wa zamani wa Ahmadiyya, Ahtesham-ul-Haq Abdul Bari, anayejishughulisha na harakati dhidi ya Ahmadiyya/Kadiyani mjini Mumbay, naye piya ametowa changamoto za mara kwa mara za Mubahila ambapo mwaka 1995 alikwenda hadi kwenye makao makuu ya Ahmadiyya mjini London kwaajili ya kufanya maapizano ya ana kwa ana na Mirza Tahir ambaye alikataa kumpa nafasi hiyo. Lakini hatimaye Mirza Tahir alifanya kosa baya sana la kukubali changamoto ya duwa ya maapizano (japo si ya ana kwa ana).

Mnamo Juni 3 1999 duwa ya maapizano iliafikiwa baina ya bwana Illias Suttar wa Karachi na Murabi wa Qadiyani wa Karachi bwana Mohammed Othman Shahiid.  Msingi wa maapizano haya ulikuwa ni ile changamoto ya mubahila aliyeitowa Mirza Tahir mwaka 1988. Mashahidi watatu kutoka kila upande walishuhudiya tukio hili la kihistoriya. Mnamo Julai 30 999, mbele ya wajumbe 18.500 wa Kadiyani waliotoka sehemu mbali mbali ulimwenguni ambao walijumuika kwaajili ya mkutano wa mwaka (Jarsa Salana) mjini London, Mirza Tahir alitamka hadharani kuikubali changamoto hii ya Illias Suttar na kusema: “Mungu atamuadhibu mtu muongo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Hata kabla ya mwangwi wa maneno yake haujamalizika, kweli muongo akatiwa mkononi na Mungu. Mnamo Agosti 20 1999 wakati Mirza Tahir alipokuwa akitowa Hotba ya Ijumaa nchini Norway, ghafla alipigwa na kiarusi kilichomfanya aseme maneno yasiyoeleweka. (Ambacho kilisababisha hotuba yake ivurugike na kutoeleweka).  Haraka haraka akakimbiziwa London ambako alikaa ndani kwa takriban mwezi mzima.  Mnamo Septemba 10,1999 alitowa hotuba ya dakika kumi ambapo alikiri kuwa alipatwa na ugonjwa wa akili ambao mlimfanya ashindwe kujielezea na hiyo ndiyo sababu iliyomfanya asionekane hadharani. Siku hiyo hakuweza kuongoza sala na badala yake Imamu akawa Ataul Mujiib Rashid.  Kwa kipindi fulani baada ya hapo alikuwa akionekana kufanya makosa ya mara kwa mara katika hotuba na sala, wakati mwingine akimaliza sala baada ya lakaa moja tu.  Adhabu hii ya Mungu ilidhihirisha mbele ya macho ya walimwengu kuwa Mirza Tahir pamoja na Mirza Gulam Ahamadi Kadiyani walikuwa waongo.  Illias Suttar bado yu hai na bukheri wa afya hadi leo. Jumuiya ya Ahmadiyya imepiga kimya cha jumla juu ya swala hili la Mubahila ya Illias Suttar. Ndani na nje ya jumuiya hiyo, mara kwa mara watu wamekuwa wakiuliza:  « Ni nani  mshindi wa Mubahila? »  Lakini Mirza Tahir naye amenyamaza kimya juu ya swala hili na hakutowa tamko lolote rasmi hadi mwisho wa uhai wake.

 Udanganyifu na ulaghai mwingine mkubwa wa Mirza Tahir ulihusiana na ongezeko la idadi ya watu walioingia katika jumuiya ya Ahmadiya.  Tokea mwaka 1993 Mirza amekuwa akitangaza kuwa kila mwaka kumekuwa na ongezeko maradufu la watu wanaoingia katika jumuiya ya Ahamadiya. Hivyo, kwa mujibu wa tangazo hilo la Mirza Tahir, katika mwaka 2000 pekee, takriban watu milioni 20 walijiunga na Ahmadiya.  Huu ulikuwa ni urongo ambao hata wafuasi wa Tahir mwenyewe hawausadiki.  Profesa Munawari Malik ambaye ni Ahmadiya wa kuzaliwa anayetokea Jhelum, Pakistan hakuweza kuuvumiliya tena uongo huu.  Akaikana hadharani Ahmadiya na kurejea katika Uislamu. Al-hamdulillahi.  Aliandika makala ndefu kufichuwa udanganyifu wa takwimu, ambayo ilichapishwa na gazeti la kila mwezi la Laulaak la Multan.  Makala hii inapatikana katika tovoti yangu katika mtandao huu:  http:”alhafeez. Org/rashid/figures 2.htm.

Pigo jingine ambalo Mirza Tahir alilipata miezi michache nyuma ni lile la ku*****uzwa katika Jumuiya hiyo kwa mshirika wake wa karibu na mwanajumuiya wa ngazi ya juu bwana Hadi Ally Chaudhary kwa mashitaka ya ufisadi.  Kwa Taarifa ya wasomaji, huyu Hadi Ally Chaudhary ndiye yule aliyeandika kitabu kiitwacho « Disciples of Satan » (Wafuasi wa shetani).  Kwa maelekezo ya Mirza Tahir. Kitabu hiki kiliandikwa ili kupoza kampeni ya uamsho  dhidi ya harakati za Ahamadiya na hasa hasa kilielekeza mashambulizi binafsi kwa Said Abdul Hafidhi na kwangu mimi.  Baada ya kutimuliwa kwake katika Jumuiya, Hadi Ally Chaudhary alijibu mapigo kwa kufichuwa ufisadi wa Mirza Tahir na Mubaliga wengine wakuu wa Jumuiya ya Ahmadiya.  Alieleza jinsi wote hao akiwemo Mirza Tahir walivyojilimbikiziya mali nyingi kwa kufuja michango ya wafuasi wa kawaida wa Ahamadiya.

Pamoja na hayo fedheha na idhilali ambayo Mirza Tahir amekumbana nayo baada ya changamoto za Mubahila za Illias Sutta, Ahtesham-ul-Haq, Shekhe Manzur Chinioti na kwa harakati dhidi ya Ahamadiya katika Uislamu haifichikani machoni mwa kila mtu masahibu, maradhi na mateso ni sehemu ya maisha.  Hali kadhalika kifo ni kipengele chamaisha kisichoepukika, lakini mambo haya yanapotokea kutokana na duwa ya maapizano basi hapo huwa ibra.  Mirza Gulam Kadiyani aliandika hivi: 

« Muongo miongoni mwa wale wanaoapizana, kwa mubahila  hufa wakati wakweli wakiwa hai. » (Malfoozaat, Roohani Khazain II Juz. 9 uk.440)

Ndio kusema bwana Ellias Suttar, Bwana Ahtisham-ul-Haq,shekh Manzur Chiniot, Said Abdu Hafidh Shaha na mimi mwenyewe, kwa rehma za Allah bado tuhai na tuwazima wa afya, wakati ambapo Mirza Tahir Kadiyani Khalifa wa nne aliyaaga makazi  haya ya muda, April 19, 2003 akiacha nyuma yake ishara za kuwaidhisha kwa wale wanaozingatiya. Laa haula! Hakuzingatiya barua ya mwisho ya Ahtasham-ul-Haq ambaye alimtaka atubiye na asilimu kabla ya kifo. Tunaomba duwa kuwa Mirza Tahir abakie milele katika kundi la Baba yake (Mirza Mahamoud) na Babu yake (Mirza Gulam Ahamdi Kadiyani). Amiin.

Sifa zote njema anastahiki Allah mmoja na wapekee.  Rehma na Amani za Allah ziwe juu ya yule ambaye baada yake hakuna Mtume mwingine.

Barua ya wazi kwa Khalifa mteule wa Tan 

Mhe Mirza Masroor Ahmad Kadiyani Sahib

Salamu iwe juu ya wale wanaofuata uongofu

Pongezi nyingi kwa kuwa kiongozi wa Jumuiya wa Ahmadiya.  Nilizisoma habari hizi katika gazeti la kila siku la « Khabrain » kwamba wewe umewazuiya Murabi na Mubaliga wa Kadiyani ulimwernguni kote wasishiriki katika Mubahila au Mdahalo wa aina yoyote ile. Kama habari hizi ni za kweli, basi si haba zinathibitisha kuwa hatima mbaya ya mtangulizi wako iko mbele yako.  Yawezekana wewe unapanga mkakati fulani mpya au yawezekana kuwa unachelea msiba uliomfika Mirza Tahir. 

Kutokana na barua hii mimi nataka kukuwekea wazi jambo fulani.  Kama kweli wewe unataka kujifunza kutokana na kifo cha Mirza Tahir basi lazima ukumbuke kuwa Msingi wa Mubahila kati ya bwana. Illias Surttar na Mirza Tahir ulikuwa ni changamoto ya Mubahila iliyotolewa na Mirza Tahir mwaka 1988. 

Kushindwa kwa Mirza Tahir katika Mubahila hii, kulikuwa ni ushahidi wa uongo wa Mirza Gulam Ahmadi Kadiyani.  Na kusihi uzingatie fundisho litokanalo na hatma ya kuwaidhisha ya Mirza Tahir, kwaajili ya kuiyokoa nafsi yako pamoja na nafsi za wafuasi wako, ukane uongo huu wa miaka mia wa Ahmadiya na Usilimu.  Inshaa Allah kwa njiya hii utafanikiwa duniani na kulipwa na Allah. 

La sivyo, mimi nakualika wewe katika mdahalo wa kupembuwa ukweli na urongo wa Mirza Gulam Ahmad Kadiyani.  Piga Moyo konde naukubali mdahalo huu.  Kwaajili ya kulinda utukufu wa Mola wangu na heshima ya bwana Mtume Muhammad (s.a.w), mimi niko tayari kukabiliana na wewe ana kwa ana.  Sasa naomba nijuwe kama wewe ambaye ni Khalifa wa Tano wa Mirza Gulam, uko tayari  kuikabili changamoto hii na kukutana nami au la.

Kwa kuzingatiya adhabu aliyoipata Mirza Tahir katika Maapizano, huenda wewe hutakuwa tayari kwa maapizano, na labda jambo lenyewe si la lazima kwa sasa. Lakini pasiwepo na kigugumizi katika  kufanya mdahalo. Kwa kuikubali changamoto hii, kwa upande mmoja utaimarisha ukhalifa wako mpya katika Jumuiya na kwa upande mwingine utapata fursa adhimu ya kubainisha ukweli au uwongo wa Mirza Ghulam Ahmad Qadiani mbele yaulimwengu.

Natumai utatowa jibu la haraka

Salam kwa wale wanaofuwata uwongofu.

Dk Syed Rashid Ali    

Dibba Al-Fujairah

Mei 13, 2003

Namna Jumuiya inavyowatendea wapinzani wak 

Siku zote ukweli unauma. Yahitaji moyo kwelikweli kuukubali au kuukabili.  Uongofu daima hutoka kwa Allah na hutolewa kwa yule anayeutafuta. Kazi yetu sisi si nyingine bali ni kufikisha ukweli.  Maandiko mengi yenye ukweli kuhusu maandiko na wasifu wa Muasisi wa harakati za  Ahmadiya, Mirza Ghulam Ahmad Kadiyani ambayo yanasambazwa na harakati za kupambana na Ahmadiya, yamesababisha Mkanganyiko mkubwa katika harakati za Ahamadiya na kwa wafuasi wake. Wakiwa hawajuwi jinsi ya kukana maandiko haya ya kweli, wanajihami kwa mbinu zisizo na hoja na zilizo kinyume na maadili, ili tu kuwapa moyo na kuwaongezea mori wafuasi wao na kuhamisha mazingatio katika ukweli halisi.  Kwa kiasi kikubwa wanatushutumu sisi kwa kupotosha maandiko au kukana kuwepo kwa maandiko haya. Wakati mwingine wanaandika vitabu kama vile « Apostle of Satan » ambamo wanatushambuliya kibinafsi wakijaribu kuyadhihaki maandiko yetu kwa msingi huo. Kuna wakati ambapo wanajihami kwa njiya za shari zaidi.  Ili kuwanyamazisha wapinzani wao wanadiriki kuwabambikizia kesi  Polisi au hata kujaribu kuwaondoa (duniani).  Katika toleo hili la Al-fat-wa tutaangalia baadhi ya mikasa. 

Kifo cha Jenerali Zia-ul-Haq.

Mnamo mwaka 1974, kipindi cha Uwaziri mkuu wa Zulfiqal Ally Bhutto, baraza teule la kutunga sheriya la Jamuhuri ya Kiislamu ya Pakistan, kufuatiya majadiliano ya miezi sita ambapo wanazuoni wa Qadiyani na Lahori walipewa nafasi ya kutosha ya kuthibitisha dini yao, kwa kauli moja lilipitisha sheria iliyotangaza wazi kuwa Jamii ndogo ya Ahmadiya/Qadiyani/Lahori si jamii ya Kiislamu, sheriya hiyo ikawapa haki zote ambazo wanazipata watu wengine wachahe nchini Pakistani.  Licha ya sheriya hii, Makadiyani wakaendelea kuhubiri hadharani kwa jina la Uislamu, hivyo kuchokoza hisiya za Waisalmu Milioni 150 wa Pakistan.  Mnamo mwaka 1984 Rais wa Pakistan Jenerali Zio -ul –Haq alilitilia manani swala hilo na kutowa amri ambayo baadaye ikawa sehemu ya sheriya na hivyo kufanya kuwa ni kosa la jinai kwa Makadiyani au mtu mwingine yeyote kutumia jina la Uislamu. Jenerali Zi-ul-Haq akauwawa katika jali ya ndege katika mazingira ya kutatanisha.  Licha ya ushahidi kuonesha kuwa makadiyani walihusika, watuhumiwa, kwasababu fulani, kamwe hawajafikishwa mbele ya sheriya.

Kifo cha Shekhe Yusufu Ludhianvi

Tukio jingine la hivi karibuni ni lile la mauwaji ya kikatili ya Sheikh Yusuf Ludhianvi yaliyofanywa mchana kweupe. Kwa kipindi cha miongo miwili iliyopita Sheikh Yusuf alikuwa akijishughulisha na kazi ya kitaaluma ya kufichuwa uongo wa Makadiani kwa njiya ya maandiko na mihadhara. Aliandika vitabu chungu mzima juu ya suwala hili. Ilikuwa asubuhi ya Mei 18, 2000 wakati Sheikh alipotoka nyumbani kwake kwenda kwenye ofisi ya Khatmi Nabuwat mjini Karachi,aliuliwa kati shambulio la Kalashnkov. Wauwaji ambao walikuwa wakiendesha baiskeli walikimbia baada ya kuwatobowatobowa kwa risasi yeye na dereva wake. Kijana wake piya alijeruhiwa vibaya. Hadi leo hii wauwaji bado hawajakamatwa.

Ndunguye Ahteshami-ul-Haq Abdul Bari abambikiziwa kesi ya mauwaji

Ahtesham-ul-Haq ambaye hapo zamani alikuwa Ahmadiya, anaishi Mumbai India. Baba yake alinaswa na mtego wa Ahmadya muda mrefu huko nyuma. Kwa hiyo yeye na familiya yake nzima wakawa wanajumuiya wa jumuiya ya Ahmadiya. Wakahamia katika jumba la ghorofa la Alhaq, ambako wapangaji wengi walikuwa Qadian/Ahmadiya. Lakini baada ya miyaka michache Baba yake Ahteshami akaanza kupata shaka na Alhamdulillah kabla ya kifo chake yeye pamoja na watoto wake walirejea katika Uislamu. Kama kawaida Murabi wa Qadiani wakaanza kuiandama familiya yake, wakijaribu kuwarubuni warejee katika Uhamadiya. Hteshami alipopata makamo makubwa alikusanya taarifa nyingi juu ya udanganyifu wa Ahmadiya na akawa mwanachama hai wa Harakati dhidi ya ahmadiya katika Uislamu. Yeye ndiye aliyeanzisha Harakati dhidi ya Ahmadiya/Qadiani mjini Mumbai kuwaelimisha waislamu juu ya udanganyifu huu, Alhamdulillah, kwa mafanikio makubwa, alisafiri huku na kule ndani  ya Mumbai, maeneo yanayozunguuka Mumbai na sehemu nyinginezo za India, akifichuwa hadharani udanganyifu wa Ahmadiya, akiwabwaga Murabi wote wa Qadiani katika mijadala na midahalo ya wazi. Hivyo Makadiani wakapoteza watu wengi waliongia katika jumuiya hiyo hivi karibuni nchini India. Alisafiri hadi London kumkabili Khalifa wa Ahmadiya, Mirza tahir, ambaye alikataa kukutana naye.

Katika jaribio la kumnyamazisha, Jumuiya ya Ahmadiya imetumia kila mbinu katika kitabu, wakimtishia maisha, wakimuhusisha na kesi za kughushi, wakitumia mbinu za hali ya juu za kumtimuwa yeye na familiya yake kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi (fleti la Alhaq Building).

Hivi karibuni hapa walimbambikiza nduguye kesi ya mauwaji. Lakini Allah ni muweza wa yote, Alhamdulillah, baada ya miaka miwili nduguye akaonekana hana hatia na akafutiwa kesi.

Uasherati wa Mirza Bashiruddin Mahmud (mtoto wa Mirza Ghulam Ahmad Qadiani na Khalifa wa Pili wa Jumuiya ya Ahmadiya) na jaribio la kuyadhuru maisha ya Bashir Masri

Baba yake Bashir Masri, Abdur Rahman Masri aliingia katika ule aliodhani kuwa ni Uislamu mikononi mwa Mirza Gulam Ahmadi Qadiyani. Abdur Rahman masri akawa mwanajumuiya hai kweli kweli wa Ahmadiya ambapo wakati wa ukhalifa wa hakiim nuruddin na Mirza Mahmud alitowa mchango mkubwa wa huduma kwa ajili ya jumuiya ya ahmadiya. Mirza Mahmud ni mtoto wa Mirza Ghulam Ahmad Qadiani. Mirza Mahmud alikuwa mzinzi, baradhuli na Muhuni wa kupindukiya. Wakati Mirza Ghulam Ahmad akiwa hai,  alishitakiwa kwa kumbaka binti mdogo wa Mfuwasi mmoja wa Mirza Ghulam, lakini tukio hili lilizimwa chichini kutokana na njama ya baba yake na Wafuwasi wake waaminifu. 

Punde alipokuwa Khalifa wa Qadian, Watoto wadogo wa kiume, wasichana na kina mama na ndowa zao wa kule Qadian wote wakawa wahanga wa usharati wake. Hata binti yake wa kuzaa mwenyewe, katoto kadogo, ummatul Rashiid, hakusalimika na ukware wake. Binti huyo alizirai kwa maumivu, mama yake (mke wa Mirza mahmud) aligomba:

«  Kwa nini umekuwa na papara namna hiyo, wewe si ungesubiri tu mwaka mmoja au miwili, huyu binti haondoki kwenda popote pale. Hivi wewe hukupata wanawake wengine? » (City of Sodom uk. 108 by Shafiq Mirza).

Pale mshirika wa karibu wa Mirza Mahmud alipoipinga tabiya hii ya uasherati, Mirza Mahmud anakaririwa kusema hivi:

« Watu ni wapumbavu sana, Wanalima bustani, wanaimwagilia na pale miti inapostawi na kutowa matunda eti wanasema kuwa mtu mwingine ndio achume matunda na kuyala! » (City of Sodom uk. 108 by Shafiq Mirza)

Bashir Masri alizaliwa mjini Qadia nchini India mwaka 1914. Wakati akiwa mvulana mtanashati wa kikashimiri mwenye umri wa miaka 18, aliitwa siku moja na Khalifa Mirza Mahmud kwa mahojiano binafsi ndani ya Kasri lake. Katika Jumuiya ya Ahmadiya, Khalifa ni kama Mungu-mtu, anaheshimiwa na kunyenyekewa. Bashir Masri aliona amepewa heshima kubwa kwa mwaliko huu. Lakini punde si punde njozi hii ikafutika pale alipoingizwa kwenye wigo wa ndani ambamo wavulana na wasichana mara kwa mara walikuwa wakibakwa na kulawitiwa na Khalifa au walikuwa wakishurutishwa kufanya uzinzi na watumishi wa kike wa Khalifa huku Khalifa akiburudika kwa mchezo huo. Bashir Masri akapitisha siku nyingi bila kulala usiku, akilia kwa machungu, pasina kujuwa namna ya kujitowa katika hali hiyo ngumu. Mwishowe akapiga moyo konde, akaandika orodha ya majina ya wahusika wa mchezo huu, ikiwa ni pamoja na tarehe na saa, na kisha akamsimuliya baba yake mkasa mzima. Mwanzoni baba yake hakumuamini, lakini kwa msisitizo wa mwanae, akatafuta nafasi ya kufanya mahojiano na Khalifa, akitumai kuwa yale mashaka yake yote yangeondshwa baada ya mkutano huu. Hata hivyo aliporudi kutoka mkutanoni akaamini yale yaliyosemwa na mwanaye. Akaandika baruwa baada ya baruwa  kwa Mirza Mahmud akimtaka ama akanushe madai haya kwa kiapo au ajiuzulu ukhalifa. Katika kujibu, Khalifa akaitenga familiya ya Masri.  Kwa maneno yake mwenyewe Bashiir Masri anasimulia mkasa huu kama ifuatavyo:

Tokea nilipotengwa na « duru za ndani » za Khalifa, maisha yangu yakawa hatarini siku zote. Genge lake la mfano wa mafia likaanza kuniwinda. Kwa hali hii mbaya, mimi nikaamua kumshika ng’ombe mapembe. Nikaenda kwa Khalifa na kumuonesha baruwa ndefu ambayo ndani yake niliandika maelezo yote ya maisha yake ya ndani ikiwa ni pamoja na majina, tarehe, matukio na takwimu. Nikamwambia kuwa nakala za baruwa hii zilizofungwa ndani ya bahasha zimehifadhiwa na viongozi fulani, zikiwaagiza wazifunguwe pale tu yeye akifa au kutoweka. Baada ya hapo ndipo sasa nilipojiona niko salama na kutembea kwa uhuru katika mitaa ya Qadian.

Kadri nilivyozidi kuona ufisadi huu ndivyo nilivyozidi kuchoshwa na dini , Hatimaye nikaishia kuwa kafiri kabisa. Hata hivyo, awamu hii chafu ya maisha yangu ikaniachia ombwe (pengo) la kiimani ambalo sikuweza kulihimili peke yangu, na ikabidi nimwambie baba. Jambo hili likamletea mshituko mkubwa. Kimaumbile asingeweza kulikubali hata neno moja la kijana wake mdogo bila uchunguzi na akaanza kufanya uchunguzi wa chini chini, haikumchukuwa muda mrefu kuthibitikiwa kuwa nilichokuwa nikimwambia ni kweli.

Baba yangu akaandika barua ndefu kwa huyu aliyeitwa Khalifa, akimtaka aelezee mwenendo wake na akimtaka ajiuzulu. Hapakuwa na jibu, ila zikafuwata baruwa  mbili za kukumbushia. Khalifa akatangaza kuwa Sheikh Abdul-Rahman Masri ( baba yangu) na familiya yake yote wame*****uzwa na kutengwa. Baruwa hizi tatu baadae zikachapishwa nchini India.

Kiutendaji kutengwa huku kulikuwa na maana ya kususwa na kutengwa kabisa kijamii. Maisha yetu, yalikuwa hatarini mno kiasi kwamba serikali ikabidi itowe ulinzi wa masaa ishirini na nne wa jeshi la Polisi pale nyumbani kwetu. Hakuna mwanafamiliya yeyote aliyeweza kutoka nje bila kusindikizwa na Polisi. Licha ya tahadhari zote hizo, mimi na wenzangu wawili tulishambuliwa mchana kweupe madukani. Mwenzangu mmoja, mtu mzima hivi, yeye alichomwa mshale kifuwani na kufa. Mwinginen alichomwa shingoni na begani na akalazwa Hospitalini kwa muda mrefu mno. Mimi nikaweza kupambana na kufanikiwa kumpiga kichwani na rungu nililokuwa nimelishika, kiasi kwamba akaanza kuvuja damu.  Haramia huyo aliyejeruhiwa akakimbiziwa mafichoni na jamaa zake, lakini Polisi wakamkamata kwa kufuatilia michirizi ya damu. Baadae akapatikana na hatia ya mauwaji na kunyongwa. Ikiwa ni dharau ya wazi juu ya sheria na amri kule Qadian mazishi ya muuwaji huyo yalifanyika kwa mbwembwe na fahari kubwa (riya), huku Khalifa mwenyewe akiongoza sala.

Baada ya tukio hili Jumuiya moja ya kiislamu ijulikanayo kama « Majlis-e-Ahrar-ul-Islam », ikaanza kupeleka vikundi vya walinzi wa kujitolea (sungusungu) kulinda nyumba yetu sambamba na jeshi la Polisi. Walikita mahema yao nje kwenye mazingira ya nyumba yetu ambayo ilianza kuonekana kama ngome iliyozingirwa.

Uwongozi wa Ahmadiya ukaanza kumuusisha baba yangu na kesi za kughushi mahakamani ili kumshushia heshima yake kubwa ya uwadilifu pamoja na kumkaushia vijiakiba vyake. Kwa kifupi aina zote za mbinu chafu zilitumika kuyafanya maisha yawe magumu kwake. Ili kuisaidia familiya yake ya watoto kumi na mmoja, ikabidi auze vito vya thamani vya familiya na mali zake za kuhamishika. Janga baya zaidi lililoisibu familiya yetu katika kipindi hiki lilikuwa ni kukwama kwa masomo ya watoto. Maelezo yote ya mashambulizi haya na madhila yalikuwa yakichapishwa na Gazeti la India.

Pakawa na shinikizo kubwa  kwa familiya yetu, kutoka serikalini serikalini na kwa watu wengine kuwa tuhame Qadian na hatimaye tukahamia Lahore. Baba yangu akajiunga na kundi la Lahori ingawaje hakuna tofauti kubwa baina ya imani zao na imani za Makadiani. Lakini mimi binafsi sikujihusisha na kundi hilo. Kama nilivyosema hapo nyuma, mimi nilipoteza imani na jumuiya hiyo ya dini. Hata hivyo katika kipindi hiki nikaanza kuwasiliana na viongozi wa Ahrar ambao walikuwa na taathira kubwa kwangu. Miongoni mwao walikuwa ni Sayed Ataullah Shah Bukhari, Sheikh Habib-ur-Rahman Ludhianvi, Chaudhari Afzal Haque, Sheikh Mazhar Ali Azhar- watu hawa mimi niliwaona ni Waislamu wacha  Mungu na marafiki wa dhati kabisa.

Baba yangu aliukubali ukafiri wangu kwa zile tuhuma tu lakini moyoni alisononeka sana. Aliniambiya kuwa mara zote alikuwa akiniombea duwa na akaniomba mimi mwenyewe nitafute uwongofu wa MwenyeziMungu kwa njia ya sala. Jibu langu likawa ni kumwambiya kwamba je alikuwa ananitaka nimuombe Mungu ambaye hayupo. Mwishowe baada ya majadiliano marefu, akaanza kuninasihi kuomba duwa za hisiya nami nikaamza kuomba kwa maneno haya: « Mungu kama upo, nipe dalili fulani  ya kuwepo kwako; vinginevyo kama kwa bahati nasibu wewe upo basi usinipatilize kwa kutokukuamini Wewe... »

Ingawaje duwa ya aina hii yaweza kuonekana kama ya kufuru kwa waumini wakweli, ilileta matokeo bora kwangu. Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa maombi, niliota ndoto mbili zilizofuatana haraka haraka. Kwa vile ndoto zenyewe ni za kibinafsi mno, siwezi kuthubutu kuzisimulia hapa.  Itoshe tu kusema kuwa ndoto hizo hasa ile ya pili zilikuwa ndefu, za wazi na zenye kueleweka. Hata kwa mtu muovu kama mimi hapakubakia tena nafasi ya shaka kwamba yupo Mola mkubwa tunayemwita Mungu au Allah, naweza kuelezea japo mwishoni mwa ndoto hiyo nilioneshwa kuwa Khalifa wa Ahmadiya ni muovu mkubwa mwenye uso uliotapakaa dhambi. 

Baada ya ndoto hizi nilipata faraja kubwa sana.  Ilionekana kama vile tatizo langu la Imani limekwisha.  Nikaamuwa kugeuza ukurasa mpya na kuwa Muislamu rasmi.  Almaruhumu Saidi Ataullah Shaa Bukhari alichukuzana nami hadi kwa Sheikh Mohammed Ilyas Muasisi wa Jumuiya ya Tablighi katika kijiji kiitwacho Mehroli, maili chache kutoka Delhi. Huko, mnamo mwaka 1940, nilikula kiapo cha utii wa Imani ya Kiislamu (Bai’at) mikononi mwake.  Ulikuwa ni mkutano wa kheri kwamba Sheikh al Habith wa India, Shekhe Mohammad Zakariya nao pia walikuwepo, baada ya swala ya magharibi iliyosalishwa na Sheikh Ilyas, jamaa yote iliyokuwa na takriban waumini 40 ikaniombea duwa maalumu. 

Mnamo mwaka 1941 nikahamia Afrika Mashariki nikiwa na mseto wa hisiya za faraja na dhambi.  Nikiwa nimesimama juu ya meli katika Bandari ya Bombey, nikaanza kusoma kimoyo moyo aya ifuatayo ya Qur’an: « Na mna nini  hampigani katika njiya ya Mwenyezi Mungu (katika kuwaokowa) wale waliodhaifu- katika wanaume na wanawake na watoto- ambao husema: “Mola wetu’ tutowe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu na tujaaliye tuwe na mlinzi anayetoka kwako, na tujaaliye tuwe na wakutunusuru anayetoka kwako. » 4:75. 

Baada ya kukaa Afrika kwa miaka 20 nikahamia Uingereza mwaka 1961. 

IMAMU MJINI WORKING.

Mnamo mwaka 1964 niliteuliwa kuwa Imamu wa Msikiti wa Shahjehan mjini Working nchini Uingereza.  Uteuzi huu unahitaji maelezo ya kuwekwa katika kumbu kumbu.  Msikiti huu ulijengwa na Mustashirikina, Dkt. Leitner mnamo mwaka 1889 kwa fedha zilizotoka kwa Waislamu wa India na baadaye likaundwa baraza la wadhamini kuuendesha msikiti huo. Hicho kilikuwa ni kipindi ambacho Ahamdiya ilikuwa bado haijaonesha kikamilifu ile picha yake halisi na baraza la wadhamini likakubali kuukabidhi uongozi wa Msikiti kwa Jumuiya ya Lahori ya harakati hizi. 

Hadi kufikia miaka ya 1968 ni Jumuiya chache tu za Kiislamu. Zilizokuwa zimejiimarisha nchini Uingereza na shinikizo likaanza kuongezeka kuwa Msikiti huu urudishwe katika hadhi yake iliyokusudiwa awali ya kuwa kituo cha Kiislamu.   Akanijia Katibu na mweka hazina wa Baraza la wadhamini kuniomba nikubali kuwa Imamu.  Nikawabainishia wazi kuwa mimi ni Muislamu wa Sunni na nikawaonesha nakala za baadhi ya makala zilizochapishwa ambazo nilikuwa nimeziandika kuipinga Ahmadiya.  Wao wakaniambia kuwa fikra zangu walikuwa wanazifahamu fika na kwamba waliziona kama ni rasilimali.  Aidha wakanihakikishia kuwa Balozi wa Pakistan ambaye zamani alikuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo na ambaye ndiye angesaini baruwa ya uteuzi wangu, alikuwa amekwisha towa idhini yake. 

Baada ya kuchukuwa uongozi wa Msikiti, muda si mrefu ikanidhihirikia kuwa mimi nilikuwa nikitambuliwa na umma mzima wa Waislamu kuwa ni mfuwasi wa Mirza.  Kwa takriban robotatu ya karne iliyopita kulikuwa na mlolongo wa maimamu wa Ahamdiya.  Waislamu hawakuweza kuamini kwamba ghafla bin vuu angeweza kutokea Imamu wa Kisuni.  Nikajiona nimeangukia baina ya vigoda viwili. Tofauti zangu za kitheolojia na makundi yote mawili ya Lahori na Makadiyani zisingeliweza kwisha; wakati huo huo Waislamu walidhania kuwa mimi lazima tu ni mfuasi wa Mirza, vinginevyo nisingeteuliwa.  Ilinichukuwa muda mrefu kupata Imani ya baadhi ya viongozi wa Kiislamu nchini Uingereza. 

Ilikuwa ni tamaa yangu ya muda mrefu kusafiri kwa gari katika nchi za Kiislamu ili niweze kusafiri hadi vijijini na kutafiti jinsi Waislamu walivyokuwa wakiendesha mambo yao ya dini kwa vitendo. (Safari hii ilinichukuwa karibu miaka mitatu ikiwa ni safari ya maili 45.000 katika zaidi ya nchi 40).  Hata hivyo kabla ya kuondoka pale msikitini, nilitaka kuhakikisha kuwa Msikiti na kituo hiki mashuhuri cha Kiislamu unabakia mikononi mwa Waislamu moja kwa moja.  Katika bodi ya Wadhamini walikuwemo wafuasi wawili au watatu wa Mirza, lakini walikuwa wakijituma  kweli kweli na walikuwa na ushawishi mkubwa.  Hawakuacha kufanya kila njiya kumrudisha Imamu wa Kimirza baada ya mimi kuondoka.  Baada ya majadiliyano na mashauriano ya muda mrefu na jamaa zangu Waislamu, nikaitisha mkutano  wa Jumuiya zote za Kiislamu za Uingereza na Eire, mnamo Julay 20 1968 kwenye Msikiti wa East London.  Mkutano huo ulihudhuriwa na zaidi ya wajumbe miamoja.  Nikawafafanulia  hali ya mambo kwamba mimi nilikuwa mbioni kuanza safari yangu mwishoni mwa mwaka na kwamba Ahamadiya walikuwa wakijaribu kwa kadri ya uwezo wao Imamu wao apachikwe. 

Kulikuwa na nukta moja muhimu sana ya kisheriya ambayo ilionekana kutusaidia katika mvutano uliotokea.  Kwa mujibu wa kifungu cha hati ya makubaliano, nafasi ya kisheriya ya wafuwasi wa Mirza, tangia mwanzo kabisa ilikuwa ni ile ya wapangaji wa Baraza la wadhamini jambo ambalo lingeweza kukoma. Kifungu hiki kilibakia pasipo kuonwa na Waislamu hadi pale mimi nilipokibainisha kwao. Katika mkutano huu ikaamuliwa kwa kauli moja iundwe kamati ya Msikiti iliyoitwa « Working Mosque Regeneration Commitee. » Ambayo ichukuwe umiliki wa Msikiti kwa pingamizi na kuteuwa Imamu maalumu baada ya kuondoka kwangu. Aidha mkutano ukaazimia kuwa Baraza la Wadhamini liombwe kuwa*****uza Wajumbe wake wa Kimirza na lisiteuwe tena Imamu wa Kimirza.  Ilikuwa ni katika mazingira haya ambapo mnamo Novemba 1968 nikaukabidhi Msikiti kwa Waislamu na kuondoka Uingereza. Kuanza safari yangu. 

Hisia za Jumla miongoni mwa wasio Waislamu ni kwamba upinzani wetu kwa Ahmadiya unatokana na ukosefu wa stahamala ya kidini.  Wanashindwa kuukubali ukweli kuwa mbali na tofauti za kiitikadi, genge hili linatumiwa na maaduwi wa Uislamu kama washirika katika kuimarisha maslahi yao ya kisiasa na kiuchumi katika ulimwengu mzima wa Kiislamu.  Juu ya yote haya kuna ufahamu unaozidi kushitadi miongoni mwa Waislamu kuwa mwenendo mchafu wa Makadiani unakussudiya kubomoa muruwa wa maadili ya vijana wa Kiislamu. 

A.L-Hafiz B. A. Masri

Machi, 1989.

(Bane of Ahmadiyat By Masri, Tarehe 18 Agost 1988 Published In London as « An Open Letter to Mirza Tahir Ahmad In Response to Mubahila » and available on line at http: « alhafeez. Org/rashid/Bane. Htm »

Mauaji Ya Fakhruddin Multan

Fakhruddin Murtan alikuwa Ahmadiya mwingine mtiifu ambaye alikula kiapo cha utii mikononi mwa Mirza Gulam Ahmadi Kadiyani. Yeye alihama kutoka mji wake wa asili wa Murtan na kwenda Kadiyani. Alianzisha duka la vitabu vya Ahamadiya kule Kadiyani na alitumia maisha yake akiitumikia jumuiya na familia ya Kadiyani.  Yale madai kuhusiana na tabiya ya uasherati ya Khalifa Mirza Mahmoud naye pia yalimuondosheya Imani juu ya Ukhalifa wa Ahmadiya. Akiwa pamoja na Abdur Rahman Masri, akaanza kudai kuwa Khalifa atamke kwa kiapo kuwa madai haya ni ya uongo na kwamba kama yeye Khalifa anaongopa basi ashukiwe na adhabu ya Mungu.  Au vinginevyo iundwe kamati ya kuchunguza madai haya na kuwasilisha hadharani utafiti wake.  Kama kawaida yake, Khalifa akam*****uza bwana huyu katika jumuiya na kuitenga familiya yake yote. Ni kisa kirefu lakini kwa kifupi baada ya miaka 32 ya utumishi katika Jumuiya ya Ahmadiya Murtan alitupwa nje ya Jumuiya kwa ujiti wa kalamu.  Kutengwa kwakwe kulimaanishwa kuwa.  Hakuna mtu yeyote pale Kadiyani aliyeruhusiwa kuongea nao, kushughulika nao, kuwauzia kitu chochote hata vyakula. 

Fakhruddin Murtan akaandika hivi:

« Tangazo la ku*****uzwa kwangu katika Jumuiya nilieleza adhabu hii kwamba kuzungumza, kusalimiana au kuwasiliana na Fakhurddiin ni maru*****u ».  Hata hivyo kinachofanyika ni hiki 

Mke wangu na wanangu nao pia walitengwa eti tu kwasababu ni watoto wangu, Upatikanaji wa maziwa kwaajili ya mtoto wangu anayetambaa ambaye ni mgonjwa umesitishwa eti tu kwasababu ni mtoto wangu, Mtumishi wangu wa kike anayemsaidia mke wangu mlemavu naye amepigwa maru*****u kuja nyumbani kwangu, Jamaa na marafiki zangu wamepigwa maru*****u kuja nyumbani kwangu, Wapangaji wa nyumba zangu wameshurutishwa kuhama, Mlemavu Shamsu Diin aliondolewa dukani kwangu eti tu kwasababu ananitazamia dunkani langu (pale nisipokuwepo), Familiya yangu inatishiwa kwa vitendo vya kigaidi kwa kuwekewa makundi ya wanaume wa makamu na vijana wanaozingira nyumba yangu usiku kucha mchana kutwa, Wauza maduka ya Ahmadiya wamepigwa maru*****u kuniuzia bidhaa.  Mpango umesukwa kuifunga biashara yangu ili kunitiya umasikini na kuitia umasikini familiya yangu ili tukose hata chakula, Baada ya kuizingira nyumba yangu, majira ya usiku tarehe 13 na 14 wezi wakaingia nyumbani mwangu kunishambuliya na kuchukuwa mali zangu.  Kwa miaka kumi na tatu iliyopita mimi naishi katika nyumba hii lakini leo hii yanatokea mambo haya huku nyumba yangu ikiwa imezingirwa,  Mbele ya madirisha ya nje ya nyumba yangu, kwa saa 24 vijana hao wanakaa hapo, na pale ninapowasha taa za nje kwasababu za kiusalama, baadhi ya vijana hawa huvuwa nguo zao na kusimama uchi wa mnyama mbele ya mke wangu na binti yangu,  Watoto wangu wasio na hatiya wamenyimwa elimu na ku*****uzwa shule.” …

(Truth Behind the announcement of My Mysterious Expulsion by Fakhrudiin Murtan- Ukweli kuhusu tangazo la ku*****uzwa kwangu katika mazingira ya kutatanisha.)

Kama Khalifa wa Kadiyani, Mirza Mahmoud alikuwa akifikiri kuwa kwa kutumia mbinu hizo angeliweza kumshinikiza Murtan aachane na madai yake ya kumtaka ale kiapo au iundwe tume ya uchunguzi, basi asikitikiwe kuwa alijidanganya. Fakhrudiin Murtan na Abdur Rahman Masri wakaendelea kushikiliya madai yao kwa njiya ya barua na vipeperushi.  Sasa Khalifa amebadilisha mbinu ambapo kupitiya khotuba zake kali dhidi yao akaanza kuwachocheya wafuasi wake wanafiki:

« Mnamo Agost 6,1937, Khalifa Saheb alitowa khotuba yake ya mwisho siku ya Ijumaa ambayo kwayo wafuasi na mashujaa wake walihamasishwa kuwawinda watu hawa (Murtan, Bashiri Masri na wengineo).  Siku iliyofuata tu, yaani Jumamosi Agost 7, majira ya saa kumi na nusu, muda wa sala ya Laasri, Shekhe Fakhurdiin Saheb Murtan, Hakimu Abdul Azizi Saheb na Hafidh Bashir Ahmadi Masri (mtoto wa Shekh Abdulr Rahman Masri), wote watatu walikuwa wakielekea kituo cha Polisi. Wakiwa umbali wa Yadi 100 kutoka kituo cha Polisi walishambuliwa na silaha yenye ncha kali.  Silaha hii yenye ncha kali ikapenya kwenye mbavu za Fakhrudiin Saheb Murtan na kumtobowa pafu. Hakimu Abdul Azizi Saheb naye piya akapata majeraha makubwa mdomoni na mashavuni kutokana na silaha hiyo hiyo.” (Pope of Rabwa uk 52 na Mohammad Mazihruddiin Murtan).

Fakhruddiin Murtani alishambuliwa mchana kweupe na aligaa gaa chini akivuja damu huku akigumia  kwa maumivu kwenye geti la Kasri la Khalifa, lakini hakuna aliyethubutu kumuhudumiya. Baadaye baadhi ya Waislamu kutoka Majirsi-e-Ahrar (Jumuiya ya Kiislamu iliyojitowa muhanga kufichua udanganyifu wa Ahamdiya)  Wakasikia habari hizi na wakaja kuwachukuwa watu waliojeruhiwa na kuwapeleka kwenye Hospital ya Gurdaspur. Fakhurddiin Murtan akafariki duniya Hospitalini mnamo Agost 13 1937. Miongoni mwa wafuasi 1000 wa Ahmadiya wanaoishi katika mazingira ambamo jinai hiyo ilitokea, hakuna hata mmoja aliyepata ujasiri wa kutowa ushahidi dhidi ya watuhumiwa. Dkt. Gurbakhsh Singh MBBS alikuwa na Kliniki yake pale pale madukani na alikuwa shahidi aliyeshuhudiya tukio hili kwa macho yake.  Ingawaje alipewa hongo ya mapesa mengi, lakini tamaa ya pesa haikumzuiya kutowa ushahidi wa kweli.  Baada ya Ushahidi wake, Azizi Ahmadi Kadiyani alihukumiwa adhabu ya kifo.  Mirza Mahmud, Khalifa wa pili akasalia maiti kwa mbwembwe na akamwita muuwaji huyo kama ni shahidi wa Ahmadiya. (Pope of Rabwa uk 52 by Mohammed Mazihrudiin Murtan)

Mirza Ghulam, Hindu Arya Samaj na Pandit Lekhram

Kile kipindi kilichofuwata baada ya kushindwa kwa Vita vya kupigania Uhuru kilikuwa ni kipindi cha mtihani kwelikweli kwa Waislamu wa Bara Hindi. Kwa upande mmoja Waingereza walipora madaraka kutoka kwa Waislamu na kwa upande mwingine Wamishenari wa Kikristo  na Wahindu wa Arya Samaj walianza kampeni kamambe ya kuwaritadisha Waislamu wengi mbumbu. Ili kutekeleza malengo yao yaliyofichikana, katika mazingira hayo magumu, kwa njama zilizopangwa na wakoloni wa kiingereza ambapo Mirza alichaguliwa kwa kazi ya kuleta mgawanyiko miongoni mwa Waislamu na kudhohofisha Imani ya Kiislamu katika nyoyo zao ili wasipigane dhidi ya ukoloni wa kibeberu, Mirza Ghulam Ahmadi akaingizwa katika jamii ya Kiislamu kama mtumishi wa Uislamu. Alifika Lahori mnamo mwaka 1869 na kwa kisingizio cha kuutumikia Uislamu, akaanza kuwachagiza Wameshanari wa Kikristo na viongozi wa Arya Samaji ya Wahindu wafanye nae midahalo ya Kidini. Lengo la kazi hiyo halikuwa kuutumikia Uislamu bali kujipatiya umaarufu miongoni mwa Wananchi Waislamu wa India na alifanikiwa sana kwa hilo. Kutokana na changamoto zake kwa Viongozi wa Arya Samaj ya Wahindu, aliweza kuvuta hisia za Waislamu wa kawida, baadhi ya jamaa wa Kiislamu wanaoishi Lahori pia walitowa mchango mkubwa katika propaganda hii. Popote walipokwenda, walimpamba Mirza Saheb na mapenzi yake ya Uislamu.  Hii ilikuwa ni hatuwa ya kwanza ya Mirza Ghulam katika mwelekeo wake wa kujijiengea sifa kama mtumishi wa Uislamu. Hapa iwekwe wazi kuwa Mirza Ghulam hakuwa mzungumzaji fasaha wala mbishani wa hoja, bali alikuwa mwepesi wa kuandika makala.  Katika historia ya Ahmadiya hakuna tukio ambapo Mirza Gulam alimchagiza mpinzani kufanya naye Mdahalo na kutoka mshindi. Naam, wapinzani wake mbumbumbu kwa hakika walivutika na uongeaji wake lakini pale mtu wa taaluma aliposimama dhidi yake basi Mirza Gulam akajaribu kumtia mtegoni kwa njiya za mzunguuko na kumtisha na kumvuragiza kwa tabiri zake. 

Baada ya kutumia miezi michache akileta sokomoko la Kidini pale Lahori, Mirza Saheb akarudi tena Kadiyani na kuanza kampeni ya kawaida ya kujitangaza.  Lengo la zoezi hili lote lilikuwa si kuutumikia Uislamu kama alivyoamini kila mtu bali kuikuza haiba yake. Kuwachagiza Arya Samaje piya ilikuwa ni sehemu ya harakati hizo hizo.  Mirza Saheb alianza kampeni hii ya kujitangaza mnamo mwaka 1877.  Mnamo mwaka 1880 Mirza alichapisha sehemu ya kwanza ya Braheen Ahmadiya ambamo alitangaza dai lake la kuteuliwa na Allah kuthibitisha ukweli wa Uislamu.  Huu ulikuwa ni mwanzo tu. Kutokana na huko « kuteuliwa na Mungu », kidogokidogo Mirza akaendelea kudai kuwa yeye ni Mujadidi na Masihi.  Kwa muongozo wa funuo zake pia alidai kuwa yeye ni Hindu Avtar, Mungu Krishna.  Ili kueneza madi hayo ililazimu kuwa awachokoze Arya Samaj (kundi la Wahindu). 

Kuna kanuni kadhaa zilizowekwa na Uislamu katika ulinganiaji wake. Allah anasema katika Qur’an:

« Waite watu katika njiya ya Mola wako kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako ndiye anayemjuwa aliyepotea katika njia yake, naye ndiye anayewajuwa walioongoka », (16:125).

« Wala msiwatukane wale ambao wanawaabudu kinyume  cha Mwenyezi Mungu wasije wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri zao bila kujuwa. (6:108) »

Lakini tukiangalia njiya zilizotumiwa na huyo aliyeitwa « muhubiri wa Uislamu », Mirza Ghulam, tunaona kuwa kanuni hizi za msingi zimepuuzwa kabisa. Kwa miaka elfu moja waislamu na Wahindu wamekuwa wakiishi Bara Hindi kwa amani na utangamano wakizingatia dini ya kila mmoja wao kwa heshima, wakiwa na mijadala ya kiilimu kwa kuzingatiya maadili ya kila mmoja bila kujiingiza katika ubishani wa matusi na kashfa. Lakini baada ya kuja mtawala wa kiingereza nchini India, mambo yakabadiklika. « Pandikizi » la Waingereza likafanya kazi  yake barabara.

Tangiya ilipoanza midahalo iliyoanzishwa na Mirza Ghula Ahmad, Wahindu wakaanza kuutusi Uislamu na kumtukana Mtume (s.a.w) hadharani, jambo ambalo halikupata kuonekana kwa karne nyingi. Lilitokeaje hili? Ni kisa kirefu, lakini kwa kifupi ni hivi. Mnamo mwaka 1877 Mirza alitangaza kuwa alikuwa mbioni kuandika kitabu cha juzuu 50 kinachoitwa « Braheen Ahmadiya », kuthibitisha ukweli wa Uislamu. Mirza akatangaza kuwa yeyote ambaye angeaandika majibu ya kitabu hiki angezawadiwa Rupia 10.000 (donge nono la miaka ya 1880). Kitabu kikaingia sokoni, na watu wakakisoma kwa mshituko kwa namna Mirza alivyorudia kuwachagiza Wahindu kutukana miungu Vedas na Shasters ya dini ya Wahindu. Katika juzuu hizi za mwanzo za Braheen Ahmadiya, katika matangazo na vitabu vyake vya miaka ya awali, Mirza alitumiya lugha ya kuwadhalilisha na kuwachokoza watu wa imani nyingine, hasahasa Wahindu. Baadhi ya mifano ni hii:

« Ndiyo kazi ya watu hawa warongo kupayukapayuka, dini yao, imani yao, mungu na Bhagwan wao ni matamaniyo ya vitu vya kiduniya, au heshima ya bandia au taifa lao au kabila lao...nani basi atakayewaita Panditi Ji na Guru Ji na Swami Ji? » (Braheen Ahmadiya part 1, Roohan Khazain Juz. 1p.107)

« Dhehebu hili jipya ambalo limeibuka miongoni mwa Wahindu, ambalo linauita mkusanyiko wao wa kidini kama Arya Samaj, siku hizi kiongozi wake, na si mwasisi wake, ni Pundit Saheb ambaye jina lake ni Diyanand. Fikra zote na maana zote za kiroho ambazo dhehebu hili limezitunga kuhusiana na Vedas, kwa ujumla hazimo katika dini ya asili ya kihindu... badala yake miongoni mwa mkusanyiko huo wa fikra tofauti, baadhi ni matamanio tu ya nafsi yake » (Ni machache mno aliyoyajuwa Mirza wakati huo ambapo utafika wakati eti atakuwa na hadhi katika dini ya Uislamu na mafundisho yake!!!..Rashid) Braheen Ahmadiya, Roohani Khazain Juz. 1 uk.72)

الصفحات [1] [ 2]

اضيف بواسطة :   admin       رتبته (   الادارة )
التقييم: 0 /5 ( 0 صوت )

تاريخ الاضافة: 26-11-2009

الزوار: 4936


المقالات المتشابهة
المقال السابقة
AlFatwa 28
المقالات المتشابهة
المقال التالية
Shatam
جديد قسم مـقـالات الموقـــع
القائمة الرئيسية
البحث
البحث في
القائمة البريدية

اشتراك

الغاء الاشتراك