:Jinsi Mirza Ghulam wa Qadiyyan anavyojikanganya katika maandishi yake
  Non - Arabic Articles Swahili

: Jinsi Mirza Ghulam wa Qadiyyan anavyojikanganya katika maandishi yake
: webmaster

BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIIM

Anti Ahmadiyya Movement in Islam

Jinsi Mirza Ghulam wa Qadiyyan anavyojikanganya

katika maandishi yake

[Na Dk Rashid]

Watukufu waislamu Asalamu Aleykum

Doublethink-Dhana dufu ni mtindo wa kujidanganya kiakili [George Orwel]. Dahan dufu ni dhana inayojengwa kwa ntu kukubaliana na upogotenge na urongo hasa hasa pale unapotumika kama  nyenzo ya kupandikizia fikra Fulani [kamusi ya America heritage,toleo la 3].

Mirza Ghulam Qadiyan ndiye muanzilishi wa harakati za dini ya Ahmadiyya.yeye alidai kuwa ni mjumbe mpya wa uislamu na nabii wa Mungu  na pia Masih aliyeahidiwa pamoja na madai mengine mengi.Enzi za uhai wake aliandika takriban vitabu 80 ambavyo ndio vitatubainishia wasifu wake.

Katika makala haya nitaibainisha mikanganyko katika maandiko yake yeye mwenyewe Mirza Ghulam Qadiyyan hata hivyo kabla ya kufanya ningependa kuwaomba wasomaji msome kwa makini nukuu mbalimbali zifuatazo toka katika vitabu vya Mirza Qadiyyan ambazo ndio zitatusaidia kumtia kitanzi Mirza wa Qadiyyani na kumnyongelea  mbali kwa kutumia maandishi yake mwenyewe.

Fatwa ya Mirza juu ya mikanganyiko ya maandiko

Mirza Ghulam Qadiyyani alitoa Fatwa kadhaa kuhusu mtu mwenye kujipinga pinga ya mwenye kujikanganya mirza anaandika  

‘Maandiko ya mtu mrongo lazima yawe na mikanganyiko[migongano] Tazama zamima Barahiin Ahmadiya sehemu ya 5,Roohan Khazain juz.21uk 275

Mirza  anaendelea kuandika

“Maandiko ya mtu mkweli na ya mtu mwenye akili timamu hayawi na migongano yoyote naam kama mtu ni punguani na majununi na  mnafiki bila shaka maandiko yake yatakuwa na kujikanganya [kujipinga] Tazama sat bachan,Roohan khazain juzu.10uk132

“Mtu yeyote mwenye akili timamu  na busara katu hawezi kuwa na imani mbili tofauti’ Tazama Roohana Khazain juzu.3uk220

sasa hebu tuangalie mifano ya mikanganyiko katika maandiko ya Mirza

Maadili ya Mirza

Mirza anaandika kwa kujitukuza

“Mungu ni mmoja ambaye amemtuma Mtume wake,naye ndio mimi mtu muungwana mwenye mwenendo na maadili mema ‘  Tazama Roohan Khazain juzu.17uk426

“Sijawahi hata siku moja kumjibu mtu kwa lugha ya matusi”   tazama Roohan Khazain juz19uk336

kuhusiana na mtu kumlaani mwingine Mirza anaandika

“kulaani sio sifa ya SIDDIQ[mtu mkweli]muumini wa kweli hawezi kuvurumisha laana kwa wengine”tazama Roohan khazain juzu.3uk456

nadhani wasomaji mmeona nukuu hizo zilizotanguliaMirza akitoa fatwa kupinga kulaani,matusi nk sasa tazameni Mirza anavyojikanganya kuhusu misimamo hiyo anasema nini na  anafanya nini sasa soma nukuu zifuatazo

Mirza hapo mwanzo alisema kuwa hajawahi kumjibu mtu kwa kwa lugha ya matusi sasa someni anaandika kwa hamaki na matusi na kulaani akijibu wapinzani wake Mirza anajibu kwa kuandika hivi;

“Enyi makabwela! Mafedhuli!maadui wa Allahna mtume!mmefanya hila ya kiyahudi katika bishara hii ili muujiza huu mkubwa usionekane duniani…urongo wenu umebainika Enyi magalasa nyie…kwa msamiati gani hawa wapumbavu  walizielewa maana hizi?Enyi majuha! Vipofu nyie..!msio na haya hasahasa huyu kinara wa madajal Abul Haq Ghaznavi na wafuasi wake Malapa ya Laaana za mungu yakuangukieni mara laki moja ….Enyi madajal Wachafu!utabiri umetimia lakini chuki imekutieni upofu’Tazama Zamima anjam-e-Atham,Roohan khazain juz 11 uk 330

Haya wasomaji mwajionea wenyewe Mirza Ghulam Qadiyyan anaanza kujikanganya katika maandishi mwanzo anadai hajawahi na hawezi kumjibu mtu kwa lugha za matusi hapa mwajionea wenyewe anavyotukana akiendelea zaidi na  matusi anaendelea hapa sasa anamjibu kwa matusi mpinzani wake mwingine Hazrat Mehr Ally Shah. Mirza anajibu kwa matusi haya

“Bazaz,Fedhuli,…Nge! Laana ya mungu ikushukie ,wewe umelaanika kwa sababu ya mtu aliyelaanika’ tazama Roohan Khazain Juzu.18

mirza anaendelea na matusi  zaidi sasa hapa anatukana waisalmu wasiokubali utume wake anasema

“Maadui [yaani waislamu] wamekuwa kama nguruwe pori kwenye mbuga  na wanawake wao wamekuwa wachafu kuliko Malaya” Tazama Roohan Khazain Juzu.14 uk 53

Juu ya mpinzani wake Maulvi Saadullah Ludhianvi. Mirza kaandika kwa kumtukana

Hivi “kinyamkela,fisadi,Ibilisi,kizazi cha laana cha mtu muovu,fedhuli,fatani na toto  Nuksi la Malaya” Tazama Roohan Khazain Roohan khazain Juzu.14uk53

Baada ya Mirza kuwamiminia wapinzani wasiomkubali laana na matusi mazito sasa jikumbushe soma tena maneno haya ya Mirza “Mimi sijawahi hata siku moja kumjibu mtu yeyote kwa lugha ya matusi”Roohan Khazain Juzu.19uk.236

“Mungu ni mmoja ambaye amemtuma Mtume wake ambaye ni mimi mtu muungwana ,mwenye khulka na tabia njema”  Roohan KhazainJuz17 uk426

“kulaani laani sio sifa yaSIDIQ[mtu mkweli]muumini havurumishi matusi Tazama Roohan Khazain Juz3 uk 456

Haya wasomaji sisi hatuna mengi mmeona wenyewe Mirza navyojikanganya huku anasema hivi kule anasema vile mara yeyehajawahi kujibu kwa matusi lakini mmeona anajibu watu kwa matusi mara anasema kulaani sio vizuri mara yeye mwenyewe Mirza anageuka na kulaani.

Mirza Ghulam-ukweli dhidi ya urongo

Tukiendelea zaidi na uchambuzi wetu juu ya kujikanganya Mirza Ghulam Qadiyyan katika maandishi yake tazameni tena anavyojipinga yeye mwenyewe hapa anasema hana mwalimu! Anasema

“Mahd si mwanafunzi wa mtu yeyote yule Naapa kuwa huu ndio wasifu wangu    hasa.hakuna mtu yeyote anayeweza kuthibitisha kuwa kuna mtu Fulani ambaye amenifundisha mimi Qur ‘an” Tazama Roohan Khazain Juz 14 uk.394

wasomaji mmeona hapo Mirza Ghulam Qadiyyan anadai hajapata kuwa na mwalimu aliyemfundisha Qur’an sasa soma hapa anajikanganya anataja walimu wake waliomfunza Qur’an Mirza anasema

“Nilipotimiza umri wa miaka 10 mwalimu mmoja wa kiarabu akateuliwa kunifundisha jina lake fazal Ahmed … na nilipokuwa na umri wa miaka 17-18nikafundishwa na mwalimu mwingine[Moulvi saheb] ambaye jinalake ni Gul Ally Shah huyu aliajiriwa na Baba yangu kwa kazi ya kunifundisha Kule Qadiyyan Tazama Roohan Khazain Juzu.13uk180

Mirza anaendelea kukiri kuwa anao walimu waliomfundisha anasema,;

“Nilipokuwa mtoto wa miaka 6-7 mwalimu wa kiajemi aliajiriwa kunifundisha Qur’an tukufu….jina la mwalimu huyo ni Fazal Illah” Tazama Roohan Khazain Juz 13 uk 180

Mirza asema yeye sio Nabii

Akiendelea kujikanganya sasa hapa anadai yeye sio Nabii Mirza anasema

“Hivi inawezekanaje mimi nidai unabii na nitoke katika uislamu na kujiunga na chama cha makafiri “ Tazama Humamatul Bushra,Roohan Khazain juz27 uk297

Mirza anaendelea kusema

“Enyi watu msiwe wapinzani wa qur’an na baada ya kukoma kwa unabii[khatamun nabiyyin]msianzishe silsila nyingine na wahyi wa kinabii”Tazama Asmani Faisla,Roohan Khazain Juzu.4uk335

“Je huyo mzushi mwovu anaedai kuwa yeye ni nabii na Mtume anaamini kweli Qur ‘an, na mtu mwenye kuamini Qur an na kuamini aya isemayo walakin Rasulullah wakhataman Nabiyyin kuwa ni maneno ya allah anawezaje kusema mimi pia ni mtume na nabii baada ya Nabii[s.a.w]”   Tazama Anjane ,Athan,Roohan Khazain juzu.11uk297

“Mimi simdai wa unabii wala sikanushi miujiza ,malaika,usiku wenye cheo  na baada ya sayidna na muhamad[s’a’w] namuhesanu mtu yeyote anayedai unabii   na utume kuwa ni mrongo na kafiri”Tazama Tabligh Risalatjuzu.2uk.22 collection of Advertisements Juzu 1uk 230

wasomaji nadhani mmeona hapo mirza anakataa yeye hawezi kudai unabii na pia anamuhesabu atakayedai unabii kuwa ni kafiri na adui mkubwa. Sasa soma tena maneno yake anajikanganya tena na kudai eti yeye ni nabii Mirza Qadiyyan anasema

“ Naapa kwa yule ambaye mikono mwake upo uhai wangu yeye amenituma mimi ameniita mimi nabii na amenitaja mimi kama ndiye masih aliyeahidiwa’Tazama Haqiqatulwahyi,Roohan Khazain Juzu.2uk503

“Mungu wa kweli ni yule aliyemtuma Nabii wake kule Qadiyyan”Tazama Dafal bala uk 11Roohan Khazain Juzu 18 uk 231

Tukiendelea zaidi na uchambuzi wetu kuhusu kujikanganya kwa Mirza wa Qadiyyan

Hapa sasa mirza anakataa yeye sio Masih aliyeahidiwa Mirza GhulamQadiyyan anasema

“Kamwe sijawahi kudai kuwa mimi niMasih aliyeahidiwa Issa BinMariyyam na yule anayenizushia jambo hilo huyo ni muongo na mzushi kabisa kabisa” Tazama Izala -E-Auham,Roohan Khazain Juzu.3uk192

"Mtu huyu muungwana yeye amejiita masiil masihi ambapo majitu majinga yakafikiri eti ni msihi aliyeahidiwa"Tazama Roohan KhazainJuzu.3uk192

watukufu wasomaji mmeoana hapo Mirza Ghulam Qadiyyan anakataa kuwa yeye sio masih aliyeahidiwa sasa tazamezi anajikanganya tena sasa anasema yeye kuwa ndio masih aliyeahidiwa Mirza anasema

"Natangaza kuwa mimi ndiye masih mwenyewe aliyeahidiwa ambaye vitabu vyote vitukufu vimebashiri kuwa atatokea katika siku za mwisho"  Tazama RohanKhazain juzu.17 uk 295

"Naapa kwa yule mungu ambaye kutunga urongo juu yake ni kazi ya wale waliolaaniwa yeye amenituma mimi kama masih aliyeahidiwa" Tazama Collection of Advertisiment of mirza ghulam juzu 3 uk 435

Mirza alalama haelewi lugha ya ufunuo

tukiendendelea zaidi na uchambuzi wetu kuhusu Mirza Ghulam Qadiyyan sasa wasomaji tazameni huyu Mirza anajiita Mtume na kuwa anapata ufunuo toka kwa mungu lakini sasa analalama kuwa ufunuo huo anaoshushiwa haulewi kwa kuwa unakuja katika lugha asiyoijua yaani inashangaza tangu lini mungu anatuma Mtume alafu anamshushia wahyi katika lugha asiyoijua Mirza alalama anasema

"Huu ni uchwara mtupu ni jambo lisilo na mantiki kabisa kwamba lugh asili aya mtu ni nyingine na ufunuo unashushwa kwa lugha nyingine   ambayo hawezi kuielewa hata kidogo kwa sababu  kuna utata mwingi ndani yake na ni nini basi manufaa ya wahyi huo ambao uko nje ya ufahamu wa mwanadamu” Tazama chashma –e-ma’arifa uk 209 Roohan khazain juzu.23uk218

Mirza aendelea kulalama kuhusu kutoelewawahyi anaoshushiwa

Anasema

“Hili ni jambo la ajabu kabisa kwamba aya zinazoshushwa   kwangu katika lugha ambazo mimi sizielewi kabisaa!!!kama vile kiingereza,kisanskrit,kiebrania n.k”Tazama Nuzuul- el-masih uk 57Roohan Khazain juzu.18uk435

'Tokea wiki hii ianze maneno kadhaa wa kadha yamefunuliwa kwangu kwa lugha ya kiingereza na kadhalika na japo kuwa baadhi yake yametafsiriwa na kijana wa kihindu lakini hiyo haotohi na baadhi ya aya zilitafsiriwa kwa na Mungu katika lugha na baadhiya maneno yapo katika lugha ya kiibrania yote hayo lazima yatafitiwena kupambanuliwa.... ebu jaribuni kupata ufafanuzi wake haraka iwezekanavyo nitaarifuni kwa mwandiko mzuri unaosomeka kirahisi"rejea barua ya Mirza Ghulam kwa Mir Abbas Shah,maktabat-e-Ahmadiyya ,collection of letters of Mirza Ghulam juzu.1uk68

subhanallah !jamani waislamu vioja hivi yaani mtu aliyeteuliwa na mungu haelewi lugha anayoshushiwa na mungu yaani mungu anamshushia aya nabii wake katika lugha asizoelewa mpaka analazimika kutafuata msaada toka  kwa vijana wa kihindu!!!

Mir Abbas Saheb alikuwa ni muridi wa kwanza wa Mirza Ghulam Qadiyyan baada ya kuona ubabaishaji wa anama hii toka kwa kiongozim wake Mirza hatimaye akamkana Mirza na kuingia katika uislamu kwa maelezo zaidi kumuhusu huyu bwana alivyomkana Mirza soma habari hii katika tovuti<http://alhafeez.org.rashid/abbas.htm>

Kwa kumalizia nakukumbusha tena soma tena maneno haya ya Mirza ili umuhukumu vizuri “maandiko ya mtu mrongo lazima yatakuwa na mapingano’Zamima Braheen ahmadiyya sehemu ya 5,RoohanKhazain juzu.21uk275

“Maandiko ya mtu  mkweli mwenye akili timamu katu hayawezi kuwa na migongano naam kama mtu punguani na majununi au ni manafiki ambaye ni mtu wa kukubali tu mambo kwa lengo lwa kuvikwa kilemba cha ukoka maandiko yake bila shaka yatagongana gongana ‘Rejea Sat Bachan Roohan khazain juzu.10uk132

‘Mtu yeyote mwenye busara hawezi kuwa na imani mbili tofauti”Rejea Rohan khazainjuzu 3 uk 220

HITIMISHO

Tunawaomba wasomaji wenyewe mchukue fursa hiyo kumuhukumu Mirza Ghulam alikuwa ni punguani?,murongo?,mwendawazimu?au kikaragosi sisi tumetaja vit6abu ambamo mikanganyiko hiyo imo tumetaja ukurasa na jalada lake kama kuna kadiyyani yeyote mwenye kutaka kujua haki basi fursa ndio hiyo akarejee vitabu hivyo ajionee mwenyewe mikanganyiko ya Mirza wala asikalie ushabiki bali kama ana nia njema ya kutafuta kujua haki iko wapi tunaomba kwa moyo mkunjufu Makadiyyani wakasome  vitabu hivyo tulivyorea InshaAllah ataiona haki na kurejea katika uislamu

Amani iwe juu ya yule anayefuata uongofu

Dk syed Rashid Ali P.O.Box 1156 Dibba Al-Fujaira United Arab Emirates rasyed@emirates.net.ae http://alhafeez.org/rashid/

 

 

:   admin       (   )
: 0 /5 ( 0 )

: 26-11-2009

: 2233