عرض المقال :Al-Zawaid
  الصفحة الرئيسية » مـقـالات الموقـــع » كشف البلية بفضح الأحمدية » Non - Arabic Articles » Swahili

اسم المقال : Al-Zawaid
كاتب المقال: webmaster

Bismillah Rahmanir Rahiim

Anti Ahmadiyya Movement in Islam

JE KWELI MIRZA GHULAM WA KADIYYANI  NI MAHDI?

Watukufu waislamu Asalam aleykum  

Uislamu ni dini teule ya Allah Qur an ni ujumbe wa mwisho wa Muumba kwetu wanadamu ulioletwa kupitia kwa Mtume wake Muhammad [SAW] Mtume wa mwisho katika mlolongo wa mitume wa Allah katika hadith kadhaa mtume ameripotiwa akisema kwamba yeye ni wa mwisho.mtume Muhammad alibashiri kuja kwa Mahd katika zama za mwisho.hata hivyo katika kipindi cha miaka 1400 iliyopita wamejitokeza wadanganyifu wengi wakitoa madai ya urongo kuhusiana na nyadhifa hizi tatu Mtume,Masih na Mahd mmoja wa wadanganyifu hao ni Mirza Ghulam wa Kadiyyan yeye alidai kuwa ni Mtume, Masih na pia akadai ni Mahd katika makala hii fupi tutachunguza  moja ya madai yake kuwa yeye ni Mahd kwa kutumia hadith  sahih za Mtume ili tuone kama kweli Mirza anazo sifa hizo mpaka adai kuwa ni Mahd maana Mirza kwa madai yake hayo ya uzushi amekuwa akidanganya wengi hasa wasiokuwa na mwanga mzuri wa mafundisho ya uislamu ambao k

Sifa za Mahd Kwa mujibu wa Hadith za Mtume [SAW] Mahd atakuwa kama ifuatavyo Mtume anasema

“Lau kama haitabaki katika dunia isipokuwa siku moja Mwenyezi mungu atairefusha siku moja mpaka amtoe mtu katika watu wa nyumba yangu jina lake linalingana na jina langu na jina la baba yake ni jina la Baba yangu ataijaza ardhi uadilifu na haki kama ilivyojaa dhulma na jeuri” (Tazama Sunan Abi Dawood Juzuu 2 uk 422 Sunan Ibn Majah juzuu 2 hadith namba 4082)

“Dunia haitaondoka mpaka awamiliki mtu kutoka katika watu wa nyumbani kwangu jina lake ni kama jina langu” (Tazama Sahih Bukhar jalada la 4 uk.143)

"Atatawala Mtu kutoka katika watu wa nyumba yangu jina lake ni kama langu na lau itabaki siku moja basi Mwenyezi Mungu atairefusha mpaka atawale” (Tazama Al jamius Sahih jalada la 9 uk74-75)

“Mahd ni katika watu wa familia yangu na katika nasaba ya Bibi Fatima” (Sunan Ibn Majah jalada la 2 hadith namba 4085)

“katika umma wangu atakuwepo Mahd kama ni kidogo basi ni miaka saba kama sivyo ni miaka tisa umma wangu utanufaika na kuneemeka mfano utajiwa na chakula chake wala watu hawatokuwa wanahodhi kitu mali zitakuwa nyingi mtu atamwambia , Ewe Mahd nipe ataambiwa chukuwa” (Tazama sunan Ibn Majah jalada la 2 hadith namba 4086)

Amesema Ibn Khaldun katika: ‘Fahamuni ya kwamba qauli iliyo mashuhuri ni kuwa katika zama za mwisho hapana budi adhihiri mtu kutoka katika familia ya Mtume [SAW] atakayeitia nguvu dini na atasimamisha uadilifu ni hakimu muadilifu anaitwa Mahd” (Tazama Muqaddimatu Ibn Khaldun uk.367-68)

Na amesema Ibn Hajar Al Asqalani katika Fat HulBari kuwa: "zimeenea hadith nyingi za kumuhusu Mahd kwa njia mutawatir atatokana na umma huu” (Tazama Fathu L Bari juzuu ya 5 uk.362-63)

Na amesema Imam Shaukhan: “Na hadith zilizokuja kuhusu Mahd zimekuja katika kiwango mutawatir kwa mwenye ubora wa kuchunguza”

Na kwa upande wake Imam Ibn Hajar Al Haithami asema: “Na hadith zilizokuja ndani yake kuna utajo wa kuja kwa Mahd ni     nyingi  zote ni mutawatir” (Tazama Sawahiqul Muhriqa jalada la 2 uk.211-212)

kwa mujibu wa hadith nyingi tu Imama Mahd amelezwa hivyo

1.      Atatokana na nyumba y a Mtume [SAW] na katika kizazi cha Bibi Fatima

2.      Atakuwa na uso wa ubapa

3.      Atatokea usiku mmoja

4.      Atakuja muda mfupi kabla ya kiama

5.      Atafanana na jina la Mtume

6.      Atakimbia maka na kwenda Madina na watu watachukua kiapo kwake

7.      Atapigana vita

8.      Ataongoza Umma kwa mujibu wa kitabu na sunna kwa miaka saba

9.      Ataeneza haki na uadilifu mkubwa katika ardhi

10.  Ataondoa ufisadi na ukandamizaji

11.  Hatokuwa yule Masih aliyeahidiwa

12.  wakati wake uchumi utakuwa bora

JE MIRZA ALIFIKIA VIGEZO HIVI?

Watukufu waislamu nadhani mmeona sifa za mahd tulivyozitaja je ni kweli Mirza Ghulam mwana Kadiyyan alifikia sifa hizi? La hasha Mirza hana sifa hata moja aliyofikia katika sifa za Mahd yeye Mirza hatokani na familia ya Mtume kwani Mahd ni katika watu wa nyumba ya mtume bali Mirza ni Mtoto wa Chirag Bibi hakuwahi kutawala nchi maana  Mahd atatawala na kusimamisha haki na kuondoa uonevu na ukandamizaji lakini Mirza alikuwa  akisaidia ukandamizaji  na utwana kwa kuwa kwake kibaraka wa serikali ya kikoloni ya Uingereza na ndiyo wadhamini wa hii dini ya kadiyyani kama anavyo kiri yeye mwenyewe anasema

“Mimi binafsi nimeungana na serikali ya Uingereza kwa ajili hiyo ni kuonesha wema kwa serikali hii tukufu na  kwa hiyo ni kazi kubwa na bora kuliko babu zangu na kuwa   jukumu lenyewe ni hili nimekusanya vitabu vya kiarabu na kifursina kiurdu kwa ajili ya kazi ya kuwalazimisha waislamu kuwa kuitii serikali ya Uingereza ni wajibu kwa kila muislamu’ (collection of advertisment juzuu ya2 uk 366)

“Namshukuru mungu ambaye amenipa nafasi chini kivuli cha serikali tukufu ya  Uingereza ambayo kwa ulinzi wake ndio nakuwa huru kuhubiri ingawa ni wajibu kwa Ahmadiyya kufanya hivyo lakini mimi ni zaidi kwa sababu malengo yangu yote yasingefanikiwa bila hifadhi ya serikali ya Uingereza nisingeweza kufanikisha malengoyangu chini ya serilkali nyingine hata kama ingekuwa ya kiislamu” (Tazama Roohan Khazain jalada 12 uk.283)

Jambo lingine alilosema Mtume kuwa  Mahd atapigana jihad lakini Mirza hakupigana jihad zaidi hayo anaipiga vita jihad anasema “vitabu nilivyoandika katika kuutukuza utawala wa Uingereza ni vingi mno vimeshehena makabati hasa vile nilivyoandika ili kujaribu kuipiga vita dhana ya jihad kwa waislamu ambayo wameishikilia na kuiaminisana hili ni jukumu kubwa nililofanya kwa serikali ya Uingereza nategemea zawadi nono toka kwao inayolingana kazi hiyo” (Tazama Tablegh Risalat jalada 7 uk 19)

Mahd atatawala Nchi na kuongoza kwa mujibu kitabu cha Mungu na sunna lakini Mirza hakutawala nchi bali kama tulivyosema alikuwa kibaraka tena anauombea dua utawala wa kikafiri anasema:

“Oh!mwenyezi mungu uweke utawala huu wa Uingereza juu ya vichwa vyetu himaya yake idumu…..Oh! malkia Victoria Mungu akulinde haihitaji kutumia lugha ngumu kueleza jinsi ninavyokupendakatika moyo wangu dua zetu usiku kucha zimeendelea kukumiminikia” (Tazama Rohan khazain jalada la 15 uk 111)

nadhani hapo watukufu wasoamaji mmeona kuwa Mirza hana sifa za ya kuwa mtawala kama alivyo Mahd bali mirza alikuwa ni kibaraka tu wa Uingereza picha halisi inaonyesha jinsi alivyokuwa kiongozi wa ajabu maana anaamrisha wafuasi wake wakubali utwana na la kushangaza eti anamuomba Mungu adumishe utawala wa kikafiri ama kweli Mirza anasikitisha sana na hii yote ilikuwa ni tamaa tu ya nafsi yake kutafuta maslahi ya kidunia ana kazi kubwa mbele ya Allah siku ya hesabu maana anapoteza wengi mpaka sasa wafuasi wake wanaendelea kupoteza watu  jambo lingine ni kuwa tukiendelea kuchamua sifa za Mahd ni kuwaMahd atakuwa hakimu muadilifu lakini Mirza hakuwahi kuwa hakimu muadilifu wala hakujua sheria alikuwa karani tu mahakamani alijaribu kufanya kozi ya sheria hizi za kitwaghut lakini akafeli

anakiri kuwa alifeli mtihani wa sheria Mirza anasema“Niliajiriwa kama karani katika mahakama ya sialkot kwa kuwa kajimshahara nilichokuwa nalipwa kalikuwa kadogokwa kuwa ilikuwa ni vigumu kuishi kwa mshahara huonikajaribu na mimi kufanya kozi ya mtihani wa sheria lakini nikafeli” Tazama kitabu cha masih wa karne uk.48 sasa tumeona kuwa Mahd atakuwa hakimu lakini mirza hakuwa hivyo alijaribu kufanya kozi ya hizi sheria za kitwaghut akafeli kwa hiyosifa ya hakimu muadilifu hana

tukija katika sifa nyingine ya Mahd kuwa katika zama zake kutakuwa na mali nyingi mpaka mtu atamwambia Mahd nipe mali ataambiwa chukuwa lakini Mirza hakuwa hivyo bali Mirza anakiri yeye alikuwa si chochote anasema ‘Kwa kifupi hali ya nyumbani kwetu iliendelea kuporomoka siku hadi siku mwishowe tukafika mahali ambapo familia yetu ilikuwa daraja la chini kabisa’ (Tazama Roohan Khazain jalada la 12 uk 271) kutokana na hali yake ya kiuchumi kuwa mbovu Mirza aliogopa atakavyodumu maisha yake ya ndoa anasema ‘Nimepata ufunuo wa ndoa yangu lakini wasiwasi umeongezeka nikihofia namna nitakavyomudu gharama za ndoa’ (Tazama Rohan Khazain juzuu ya 22 uk.2470)  kutokana na hilo alichanganyikiwa Mirza  anasema kuwa kaanzisha hii dini ya kadiyyani ili apate faida ya kidunia kuvuna  pesa anasema “Nimepokea ufunuo ili kui

‘Nimewekeza mtaji wangu kwenu[makadiyyani]mnajua faida na hasara yake’ (Tazama Mansab khilafat uk 40)

“Na iwapo yeyote kati yenu hataki kujitolea katika jumuiya yangu walau vijisenti vichache basi sina haja naye hana umuhimu wa kuwepo ndani ya jumuiyya” (Tazama matamshi ya Mirza yaliyochapishwa katika Al Ahbar A badr qadiyyan ya tarehe 9 julai 1903) kwa hiyo Mirza si Mahd hana hata sifa moja Alhamdulilah Mirza mwenyewe alikuwa analijua hilo hatimaye akakiri kuwa yeye si yule Mahd halisi aliyetabiriwa na Mtume[SAW] anasema “Sijadai kwamba mimi ni yule Mahd wa kweli atakayekuja ambaye atatokana na Ahlu Bayt katika  nasaba ya Bibi Fatima” (Tazama baraheen Ahmadiyya jalada 5,Rohaan Khazain jalada la 21 uk.356)

“Nakiri hivi kwa sababu huenda wakaja Mahd wengisiku za usoni lakinimmoja wao huenda akawa  jina lake Imam Muhammad” (Tazama Roohan Khazain juzuu ya 3 uk 197) Mirza anaendelea kukiri kuwa yeye sio Mahd anasema “Inawezekana ikawa hivyo na kwa hakika muda fulani huko mbeleni atakuja mtu atakayeitwa Mahd ambaye ambaye amebashiriwa na Mtume kwa sababumimi sikuwa mtawala na sikuwa na amri  katika ulimwenguhuu bali nilikuwa *****ara na mnyonge”

Mirza anaendelea anasema “Huenda wakaja Mahd zaidi ya 10,000lakini wa kweli ni yule atakayeshukia Damishqi” (Tazama Izala e Auham,Roohan Khazain juzuu ya 3uk 251)  pamoja na kukiri kote huko Mirza Ghulam Mwana wa Kadiyyani wafuasi wake wapotevu wanaedelea kudai kuwa Mirza ni Mahd na kwa sababu ya shetani anavyowachezea kama alivyokuwa akimchezea kiongozi wao Mirza kwani Mirza alikuwa mtu kigeugeu sana mara kwa mara anageuza madai mara yeye ndio Mahd, Dhurkarnain, Khidri, Nuhu, Yussuf, Ahmad, Adam, Is-haka kwa hiyo Mirza amejaa vituko chungu mzima na kwa kuwa ni mpenda pesa hatawaliomfuta baadae wote walikuwa na tabia hiyo mpaka sasa dini hii ya ukadiyyani inaendeshwa kwa michango chungu nzima mpa watoto wadogo wanakamuliwa watoe pesa wazee nao hawakuachwa nyuma wanakamuliwa pesa kwa ujumla huu unyang’anyi wa pesa za wafuasi wao ambao wameupa jina la chanda uko kama ifuatavyo ameandika Profeaa wa kikadiyyani bwana Munawar kuwa kuna utoaji wa chanda katika dini y

1.      CHANDA AAM

2.      CHANDA JALSA SALANA

3.      CHANDA TAHREEK JADEEED

4.      CHANDA WAKF JADEED

5.      CHANDA SAD SALA JUBELEE[sasa imefutwa]

6.      CHANDA KHUDDAMUL AHMADIYYA[ambayo wanakamuliwa vijana]

7.      CHANDA TAMEER HALL[ukumbi huu ilimalizika kujengwa tangu 1973 lakini bado wanauchangia mpaka leo]

8.      CHANDA AFRICA

9.      CHANDA DISH ANTENA[Ahmadiyya TV ]

10.  CHANDA LAJNA AMA’ALLAH[hii wanakamuliwa akinamama]

11.  CHANDA ATFAAL[Hii wanakamuliwa watoto]

12.  CHANDA ANSAAR[Hii wanakamuliwa watu wazima waliovuka miaka 40]

HITIMISHO  

Watukufu waislamu bila shaka mpaka hapo mmejionea wenyewe sifa za Mahd kama alivyobainisha Mtume [SAW] katika Hadith zake ambapo tukizilinganisha sifa hizo Mirza Ghulam wa Kadiyyani hana hata moja kwa hakaika pasina shaka makadiyyani ni makafiri hilo halina mjadala ni makafiri kwa asilimia 100 hivi juzi tu hapa walidhirissha ukafiri wa mwingine baada ya kufariki khalifa wa mzushi Mirza Tahir Ahmad waliuacha uso wake wazi na waombolezaji wakawa wanapita kumuaga huu ni ukafiri isitoshe wakaja kumzika ndani ya sanduku ndipo walipokamilisha mazishi yao ya kikafiri waislamu wote mnatambua taratibu za mazishi ya kiislamu kama alivyofundisha Mtume sasa hawa makadiyyani wanadai wao ni waislamu sijui taratibu hizo wamezitoa wapi yadhihirisha kudai kwao kuwa ni waislamu ni janja yao kutaka kuhadaa ulimwengu wa kiislamu lakini Alhamdulilah unafiki wao na ukafiri wao wanazidi kuudhihirisha hili genge la makadiyyani ni hatari sana katika ulimwengu wa ustaarabu wa kiislamu wanaj

WABILLAH TAWFIIQ

USTADH ZUBER KHAMIS BUZULU E mail buzulu7b@hotmail.com Mabibo Dar es salaam Tanzania

Ili kupata maandishi bure tafadhali andika au piga simu:- ANTI AHMADIYYA MOVEMENT IN ISLAM Dr. Syed Rashid Ali P.O. Box 11560 Dibba Al Fujairah U. A. E. rasyed@emirates.net.ae

اضيف بواسطة :   admin       رتبته (   الادارة )
التقييم: 0 /5 ( 0 صوت )

تاريخ الاضافة: 26-11-2009

الزوار: 2144


المقالات المتشابهة
المقال السابقة
Prof Munawwar Malik leaves the Jamaat
المقالات المتشابهة
المقال التالية
Facts & Figures
جديد قسم مـقـالات الموقـــع
القائمة الرئيسية
البحث
البحث في
القائمة البريدية

اشتراك

الغاء الاشتراك