:Mubahila with Mirza Tahir
  Non - Arabic Articles Swahili

: Mubahila with Mirza Tahir
: webmaster

BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIIM

Anti Ahmadiyya Movement in Islam  

Mirza Tahir na Mubahila[maapizano]

[by Dk syed Rashid Ali]

"Wale waongo ambao hufanya mubahila[maapizano]na wakweli basi waongohufa wakati wakweli wangali hai"[taarifa ya Mirza Ghulam Qadiyyan katika malfoozat]

Mnamo mwaka 1988 ilitolewa changamoto ya mubahila[maapizano]kwa umma wote wa kiislamu. Changamoto hiyo ilitolewa na kiongozi wa jumuiyya ya Ahmadiyya duniani Mirza Tahir Ahmad Qadiyyan aliyewaita waislamu kuwa ni makafiri na waongo.

Chapisho la changamoto hiyo lilitupwa kinyemela ndani ya majumba ya waislamu usiku wa manane mjini Karachi. Wanachuoni wengi wengi wa kiislamu waliitikia changamoto hiyo toka kwa Mirza Tahir,miongoni mwao akiwa Syed Abdul Hafiz Shah mwanzilishi wa harakati za kiislamu dhidi ya Ahmadiyya.

Mwanachuoni huyu alijitolea kuja London kwa ajili ya mubahila [maapizano] ya ana kwa ana [kama inavyotakiwa na sunna ya Mtume mtukufu SAAW] hata hivyo Mirza Tahir akafyata mkia na kuogopa kuapizana.hata maombi ya waislamu kutaka ajitokeze hadharani ili wafanye naye mubahila wa uso kwa uso hakuyajibu.tokea wakati huo,mimi binafsi kwa niaba ya jumuiyya ya harakati za kiislamu dhidi ya Ahmadiyya,mara kadhaa nilitoa changamoto ya mubahila kwa Mirza Tahir. Nilitoa changamoto mwaka 1994,1995,1997,1998na 2000,lakini Mirza Tahir akaogopa kuzikubali changamoto hizo.

Sheikh Manzoor Chinioti alikuwa akienda London karibu kila mwaka na kumpa changamoto ya mubahila Mirza Tahir lakini wapi changamoto zake ziliishia patupu naye ndugu Ahtesham-ul-Haq Abdul Bari alikwenda London mwezi September 1996.akafika mpaka makao makuu ya Ahmadiyya na kutaka kukutana na Mirza Tahir kwa ajili ya mubahila lakini Mirza Tahir akakataa kabisa hata kuonana naye.

Katika lugha kiurdu kuna msemo mmoja usemao ‘msiba unapofika mbweha ukimbilia mjini’katika miaka mingi ya ukhalifa wake Mirza Tahir amekuwa na kiburi na jeuri kwelikweli lakini kila mtu anasiku yake na baadhi ya siku ni ndefu kuliko nyingine.licha ya kuwa mjanja wa kukwepa mubahila,Mirza Tahir alifanya kosa baya sana mwaka 1999. mnamo mwezi Juni 1999,bwana Illias Suttar alifanya mijadala na Mohamed Usman,kiongozi wa kadiani mjini Karachi Pakistan wakati wa mjadala siku ya tarehe 3/6/1999,Mohamed Usman akatoa kijarida chenye kichwa cha habari ‘changamoto ya mubahila kwa umma wote wa waislamu’ kijarida hicho kiliandikwa tarehe 10/6/1988.Usman akampa bwana Illias kijarida hicho na kuomba kufanya naye mubahilla kwa niaba ya Mirza Tahir,kuthibitisha ukweli wa Mirza Ghulam Ahmad Qadiyyani jambo hili likakubaliwa kwa hamu kubwa na bwana Illias Suttar.

Baada ya hapo Mirza Tahir wakati wa Jalsa Salana mwezi julai 1999,akatangaza rasmi kukubali kufanya mubahila alitamka hivyo mbele ya wafuasi wake 18,000 waliojumuika kwa ajili ya Jalsa hii kule Izlamabad,surey uingereza.

Takriban siku ishirini baada ya kuikubali changamoto hiyo.Mirza Tahir akiwa ziarani Norway alipatwa na laana ya mubahila wakati akihutubia ghafla alipoteza kauli,hakuweza kusema chochote,akakimbiziwa London na akawa ndani kwa majuma mengi akiugua ugonjwa usiojulikana. Maelezo na matokeo ya mubahila huu yakachapishwa na bwana Illias Sutar. Na kutafsiriwa hivi;

Mirza tahir atangaza mubahilla kati yake na Illias Suttar katika Ahmadiyya TV

Mnamo tarehe 30 July 1999 wakati wa jalsa salana ya 34mjini London mbele ya umati wa 18,000 wote wakiwa makadiyyani waliotoka sehemu mbambali duniani,kiongozi wa makadiyyani Mirza Tahir Ahmad Qadiyyani alitangaza mubahila dhidi ya Illias Suttar , tangazo hilo lilitolewa dunianai kote kupitia kituo chaTV cha Ahmadiyya baadhi ya nukuu kutoka katika hotuba ya Mirza Tahir ni hizi zifuatazo

"hivi sasa kwanza kabisa nitakupeni tathmini ya mahudhurio. Punde tu Idrisa Sahib ametoa muhtasari wa twakwimu anasema kuwa muhudhurio ya katika mkutano huu yamepiku mahudhurio ya mwisho ya mwaka jana Alhamdulillah thuma Alhamdulillah.mkutano wa mwisho kabisa wa mwaka jana ulihudhuriwa na watu 17,500.mkutano wa kwanza wa mwaka huu, mahudhurio yake ni 18,500 jambo moja ni kuwa kule Karachi kuna jahili mmoja[jitu mbumbumbu]limethubutu kutaka kufanya mubahila wanazuoni lazima waelewe kwamba mimi nikiwa kama mkuu

wa jumuiyya duniani kote si kazi yangu kuitikia tu wito wa Tom,Dick na Hary anayetaka mubahila si kazi yangu. Lakini sijui ni kwa nini watu hawaelewi sasa imetokea kuwa vingozi wawili wa kule karach walitiwa mtegoni na adui na wakataka afanye nao mdahalo.mtu huyo[Illias]alikuja na dhamira hii kwamba wakati wa mdahalo ghafla akaibua suala la mubahila. Hivyo wakati wa mdahalo alitoa changamoto ya mubahila na licha kwamba haikunipasa mimi kwani sikupata kutoa changamoto kwake haikuwa wajibu kwangu kabisa kuitikia changamoto yake na hata kama ningekubali changamoto hiyo bado ningeweka masharti haya kama vile ‘ni kiongozi gani aliye nyuma yake ?na nani anamuunga mkono?nani anayemkubali?je kama atashindwa ataukubali ushindi wa Ahmadiyya?lakini ukiachilia mbali yote haya,viongozi wetu hawa wadogo sio tu waliitikia changamotoya mubahila bali pia walimpa changamoto yangu sasa nini namna hii?hawakuwa na haki ya kufanya hivyo hata mimi naelewa kuwa hawa wapiganaji wa jeshi la Ahmadiyya hivyo wao walikubali na MIMI PIA NAKUBALI NA MTAZAMO HUU MIMI NIMEIKUBALI CHANGAMOTO YA MUBAHILA NATANGAZA JAMBO HILIWAZI WAZI MBELE YENU KWAMBA YULE MTU ANAYEFANYA MUBAHILA NA SISI ATABAINIKA KUWA MUONGO TU"

Mubahila uhalalika baada ya pande mbili kukubali

Tarehe 3 mwezi Juni ,mwaka 1999 mada ya mjadala ilikuwa changamoto ya yenye thawabu ya mubahila ya Illias Suttar. Mukarram Uthman Sahib alimpa alimpa mukaram Illias Suttar changamoto ya mubahila ya Mirza Tahir,kiongozi wa Ahmadiyya na akamkabidhi kipeperushi cha mubahila kilichochapishwa tarehe 10 mwezi JUNI,mwaka 1988,muhtaram Illias Suttar akaikubali changamoto hii ya mubahila. Gazeti la kikadiyani la AL Fazl Internations la tarehe 3 semptemba 1999-12 septemba lilichapisha habari ya mubahila huu likisema ‘Illias Suttar aikubali changamoto ya mubahila iliyotolewa na jumuiyya ya Ahmadiyya"

Maneno ya Mohammed Zakaria Khan Qadiyyani,kiongozi wa shah Faisal Colony Qadiyyan Halqa;kuhusiana na mubahila huu kiongozi huyu wa kadiyyani alijigamba kwa kusema

"kwa vile Illias Suttar amejifikisha mwenyewe katika mahakama kwenye korti ya Allah,sasa Allah atahukumu kwa hakiInshaAllah"

Faiza Ayesha[kadiyyani]akamtumia barua pepe Illias Sutar tarehe 5/10/2002 akilalama kwa kusema ‘Ilias Sahib sasa Mirza Tahir anaumwa pengine ugonjwa huu unatokana na mubahila kati yenu’ faiza ayesha@hotmail.com <mailto:ayesha@hotmail.com> Tafsiri

Mirza Tahir apatwa na ugonjwa siku 20 baada ya kutangaza mubahila[maapizano]

‘London, September10 1999:Huzoor [Mirza Tahir]alitoa hotuba fupi ya dakika 17-18 hivi kama kawaida television ya Ahmadiyya[MTA] ilirusha hewani moja kwa moja[live]kuhusiana na ugonjwa wake na kuadimika kwake katika msikiti wa AlFazl Huzoor[Mirza Tahir]alisema kuwa kulikuwa na hofu na wasiwasi kichwani ugumu wakuelezea kitu mpaka ukaeleweka sababu kubwa ya hofu ilikuwa ni Jalsa salana watu wanaume na wanawake takriban 21,000 nimetakiwa kukutana nao mzigo wa mikutano ni mzito zaidi kuliko mzigo wa hotuba katika jalsa salana kila watu wakusimulie mikasa yao kisha usimame na kupiga picha nao.mizigo yote hiyo ibebwe pamoja matokeo yake kichwa changu kikatingwa na fikra kiasi kwamba nikaona heri nisije kutoa hotuba namuomba Mugu ajaalie hotuba hii iwe mwanzo wa uzima wangu kiafya kwa hiyo nimejitokeza mbele yenu ili mnione kwa macho yenu kuwa ni mzima hali ya kichwa changu na uwezo wangu kiakili uko katika hali nzuri naweza kuzungumza chochote kwa imani na kwa kujiamini kabisa [Al Fazl international 14september 1999] hii ndio hotuba ya kujihami ya Mirza Tahir akijaribu kuficha ugonjwa aliopata baada ya mubahila

Swali kutoka kwa Illias Suttar

Illias Suttar alihoji kuhusiana na hotuba ya Mirza Tahir hivi

Ikiwa sababu ya ugonjwa ni kutokana na jalsa salana kwa nini ugonjwa huo uzuke siku 20 baada ya Jalsa?angelipatwa na ugonjwa huu muda mfupi tu baada ya jalsa isitoshe hii ilikuwani jalsa ya 34 je yeye au khalifa mwingine yeyote yule aliwahi kuugua kwa muda mrefu namna hiyo katika Jalsa Salana33 zilizopita?katika Jalsa pia kulikuwa na wajumbe wengi takriban 17,500 kwa nini hukuugua wakati huo?

Gazeti la wiki la khatme Nubuwwat

London;

Katikati ya mwezi Agost 1999 kiongozi wa kadiyyani Mirza Tahir alitoa khutuba ya ijumaa Norway ambayo ilidumu kwa dakika 10 tu lakini hakuna aliyeweza kuelewa hata neno moja la kile alichokisema ilielekea kuwa ulimi wa mtu huyu aliyelaanika ulipata kiharusi akasafirishwa haraka haraka na kupelekwa hadi London .hadi tarehe 9 mwezi wa September hakuweza kutoka nje kuswali wala hakuna aliyeweza kuonana naye alibaki ndani akitumikia adhabu ya Mungu kwa sababu ya laana zake.

Ni muhimu kutilia maana ni kuwa pale hotuba ya Mirza Tahir alipokumbwa na kiharusi nini kilichokuwa kinaendelea vichwani mwa wale makadiani waliokuwa wanajua kuwa siku 20 za nyuma Mirza Tahir alikuwa ametangaza mubahila[maapizano]dhidi ya bwana Illias Suttar izingatiwe kuwa gazeti la wiki khatme Nubuwwat huko nyuma halikupata hata mara moja kuchapisha taarifa za laana walizopata makhalifa wa kikadiani lakini kwa mara ya kwanza taarifa za laana dhidi ya Mirza Tahir zimechapishwa katika gazeti la wiki la khatme Nubuwwat katika Qur an dua ya laana kwa ajili ya mubahila ni kuwa laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wasemao urongo na kweli laana ikamshukia Mirza Tahir kwa kuwa ni mrongo .

Barua ya Ahtesham-ul-Haq Abdul Bari

Mwanaharakati madhubuti katika harakati za kupinga ukadiani huko mumbai bwana Ahtemsham-ul-Haq Abdul Bari[zamani alikuwa kadiani]mnamo tarehe 6/8/200 alimuandikia barua Mirza Tahir Ahmad Qadiani ambapo alisema hivi kumwambia Mirza Tahir "Baada ya kufanya mubahila na Illias Suttar umeona yaliyokufika. Ulikuwa bukhari wa afya lakini baada ya mubahila laana ya Mungu ikakushukia kwa njia ya kiharusi sasa ebu acha ukadiyyani na silimu we mtu.

Maulana Manzoor Ahamed Chiniota ,mbunge wa zamani wa bunge la Punjab na katibu mkuu wa internation Nubuwwat movement.anasema

"Siku 20 tu baada ya kusoma dua ya laana Mirza Tahir laana ikampata alikumbwa na ghadhabu za Allah hajawahi kuwa na ugonjwa wa kiharusi mwenyezi mungu kahukumu baina ya mkweli na mrongo Alhamdulillah mwaka ule haki ilidhihirika na ushindi ukapatikana upande wa uislamu,Illias Suttar alishinda"

Dailly Hindustan,Mumbai,India 23/4/2003

Wakati wa jalsa salana ya 34 mjini London iliyoonyeshwa moja kwamoja na Ahmadiyya TV mbele ya umati wa watu 18,000 waliohudhuria kutoka sehemu mbalimbali duninai,Mirza Tahir alitangaza MUBAHILA na Illlias Suttar.katikati ya mwezi huu wa Agosti 1999 khalifa huyu wa kikadiyyani alitoa hotuba huko Norway ambapo alichukua dakika 10tu hapohapo mungu akamuangamiza alipata ugonjwa wa kiharusi uliompoozesha ulimi wake.

Fatwa ya Mirza Ghulam Qadiani

Kusiana masuala ya mubahila Mirza Ghulam Qadiani anasema

 

"Ndio ni kweli kabisa kuwa wale waongo wafanyao mubahila na wakwelibasi waongo wanakufa wakati wakweli wangali hai"Mirza Ghulam aliandika haya katika gazeti la Al hakam la tarehe 10/10/1907 kuwa

" waongo hufa wakati wakweli wangali hai" ndiyo hivyo Mirza Tahir kafa wakati Illias Sutar angali hai.

Wapendwa wasomaji.

Sasa khalifa mpya wa makadiyyani khalifa wao wa 5 khalifa huyu anaitwa Mirza Masroor Ahmad Qadiani khalifa huyu mpya ni kitukuu cha Mirza Ghulam Qadiani ni jambo la kuchekesha kuwa uongozi jumuiyya ya Ahmadiyya unakwenda kifamilia [kiukoo] kwa mara nyingine tena mtu kutoka ukoo wa Mirza Qadiyyani amechaguliwa kuongoza jumuiyya hii kwa niaba ya Anti-Ahamadiyya movement.namsihi kwa dhati kwamba ajifunze kutokana na lile fundisho la adhabu ya Mwenyezi Mungu aliyoipata mwezie aliyetangulia.

Inaonekana Mirza Masroor amechukua hadhari ya adhabu ya Mungu kwani amewapiga maru*****u makadiani kufanya midahalo na waislamu au kujishughulisha na aina yoyote ile ya Mubahila[khabrain akhbaar,Islamabad Pakistan]

Ewe mpendwa bwana Masroor Ahmad Qadiani Sahib!

Haitoshi tu kuzuia mubahilla na waislamu kama umesikia ujumbe wa Mwenyezi Mungu uliotolewa kupitia mubahila hii basi unapaswa kumkana Mirza Ghulam Ahmad Qadiani kuwa ni mrongona tunakuomba usilimu.achana na ukafiri huo ukadiyyani kumbuka mubahila iliomuangamiza Mirza Tahir ulitokana na changamoto aliyoitoa yeye mwenyewe mwaka1988 ambayo kimsingi ilimuhusu Mirza GhulamQadiani kama alikuwa mrongo au mkweli hatimaye ushindi wa mubahila ule umedhirisha nani mkweli katika madai yake imethibiti Mirza ni mrongo kwani aliyesimama kumtetea katika mubahila [maapizano] Mirza Tahir ameshindwa baada ya kuangamia kwa kupata ugonjwa kiharusi na hatimaye kufa. Nakusihi ukane ukadiyyani na kusilimu nazidi kukusitiza na kukushauri waombe wafuai wote wa jumuiyya ya Ahmadiyya nao wafanye hivyo kwa kusilimu.IshaAllah kama utafanya hivyo utafaulu hapa duniani na akhera ukikataa kufanya basi natoa changamoto ya mubahila[maapizano]kwako kuthibitisha kuwa Mirza Ghulam Qadiani alikuwa muongo katika madai yake yote. Natumai kuwa tofauti na mtangulizi wako wewe utakuwa na moyo wa ujasiri kujitokeza hadharani kwa ajili ya maapizano[mubahila] kuthibitisha kuwa Mirza Ghulam Qadiani ambaye wewe ni khalifa wake alikuwa nabii au la tunatangaza hadharani Mirza alikuwa ni mrongo mkubwa wala hakuwa Nabii wa mungu kama kweli unathibitisha yeye alikuwa ni mkweli basi tunakuomba toka hadharani tuapizane kwa kuikubali changamoto hii utakuwa kwa upande mmoja utaimarisha nafasi yako katika jumuiya na kuzidisha imani kwa wafuasi wako na dunia kwa ujumla tunataka utoke tufanye mubahila ulimwengu ujue je nani mkweli na je kweli Mirza alikuwa na nabii au la.

Salam za amani ziwe juu ya wale wanaofuata hidayah

Dr. Syed Rashid Ali P O Box 11560 Dibba Al-Fujariah United Arab Emirates rasyed@emirates.net.ae http://alhafeez.org/rashid/
:   admin       (   )
: 0 /5 ( 0 )

: 26-11-2009

: 2055