:Mirza Ghulam and his god
  Non - Arabic Articles Swahili

: Mirza Ghulam and his god
: webmaster

BISMILLAH RAHMANIIR RAHIIM

 

Anti Ahmadiyya Movement in Islam

 

MIRZA NA MUNGU WAKE

Ni nani alikuwa Mungu wa mirza wa qadiyyan?

[NA DK Sayid Rashid Ally]

 

watukufu waislamu

Asalam Aleykum

Kwa mujibu wa imani ya kiislamu MwenyeziMungu ndiye muumba wa ulimwengu na kila kitu kilichopo ndani yake ndiye muweza wa yote mfalme na muhimiliwa kila kilichopo ulimwenguni na nje ya ulimwengu.

Yeye ni mmoja  na mpweke hana mshirika yeye ni mwingi wa rehema .mjuzi wa yote wa milele na milele na mola wa walimwengu wote,Mfalme wa siku ya malipo.

Hakika yake ameepukana na aina zote za mapungufu,dosari na kasoro.hashikwi na usingizi na wala alali hakuzaa wala hakuzaliwa na hakuna aliyefanana naye.

MwenyeziMungu ameleta mitume na manabii(amani na rehema ziwe juu yao)amewashushia wahyi ili wawaongoze wanadamu katika njia sahihi nako ni kumpwekesha mwenyezimungu.na katika hao mitume na manabii wa mwisho wao katika ule mlolomgo mrefu wa manabii si mwingine ila ni Mustafa Muhammad[s.a.w]ndiye aliyeleta ujumbe wa mwisho kabisa katika kitabu cha QURAN ili kiwaongoze wanadamu katika maisha ya o ya kila siku mpaka siku ya mwisho. Lakini Mirza Ghulam Ahmad mzaliwa wa qadiyyan ambaye ndiye muanzilishi wa dini ya ahmadiyya[qadiyyan]yeye alikuwa na dhana ya ajabu sana juu ya Mungu.japo kuwa alidai kuwa yeye ni muislamu mtazamo wake juu ya Mungu sio ule unaobainishwa na uislamu.hivyo mtu unastaajabu kwani Mirza Ghulam alidai yeye anapata ufunuo toka kwa mungu hizo funuo anazodai kushushiwa na huyo Mungu wake ni za ajabu na zenye fedheha kubwa ndani yake kiasi kwamba moja kwa moja mtu unaamini kabisa bila kipingamizi kuwa hizo funuo zake si za kutoka kwa mungu bali funuo hizo zaMirza alikuwa anafunuliwa na shetani na kwa hiyo Mirza hakuwa muislamu bali ni kafiri wa wazi wazi InshaAllah katika makala hii tutaonesha funuo hizo anazodai kufunuliwa Mirza toka katika vitabu vyake mwenyewe Mirza tutataja kitabu ,kurasa na jalada ambamo zimo funuo hizo mtajionea kweli funuo hizi ni kutoka kwa mungu au shetani?

 

MIRZA ADAI MUNGU NI KAMA CHUI

Mirza anasema

‘qayuum-ul-alamiin’ni moja ya majina au sifa za mwenyemungu ni mwenye

mikono na miguu mingi isiyoweza kuhesabika na kila mguu ni mrefu kiasi

ambacho hauwezi kuhesabika na mungu ana upana usio na mwisho na

urefu usio na ukomo na yuko kama chui na pia ana nyaya zilizosambaa

sehemu zote za dunia’ Taz.Roohan khazain juzuu ya 3uk.90

 

MIRZA ADAI KATUKUZWA NA MUNGU

Mirza anadai kapata ufunuo kwa kiarabu mungu anamwambia

‘Nahmaduka[nakutukuza wewe]’Tazama Haqiiqatul-wahyi,Roohan khazain juz.22 uk 97

 

MIRZA ADAI MUNGU KASHUKA CHINI KWA AJILI YAKE

Katika ufunuo huu Mirza anadai mungu kamwambia hivi

‘nimeshuka chini kwa ajili yako’Taz.HaqiqatulRoohan Khazain juz.22uk.97

 

MIRZA ADAI MUNGU ATASHUKA QADIYANI

Mirza anasema kuwa kapata ufunuo mungu anamwambia kuwa atashuka kijijini alikozaliwa Mirza yaani kijiji cha qadiyyani Mirza anasema:-

‘punde nimepata wahyi kuwa mungu atashuka kule qadiyyan kulingana na

ahadi yake’Taz.tadhkirah collection of inspiration uk 452 toleo la 2 akiendelea zaidi na madai yake upotovu Mirza hapa anadai mungu atashuka kama mtoto Mirza anasema kapata ufunuo unamwambia “Tunakupa habari njema za mtoto  ambaye kwaye haki itadhihirika kama vile mungu ameshuka chini”Haqiiqatull wahyi,Roohan khazainJuz.2 uk 99

 

MIRZA ADAI MUNGU WA KWELI KAMTUMA YEYE QADIYYAN

Mirza anasema:-

“Mungu wa kweli ni yule aliyemtuma mtume wake kule Qadiyyan’

Taz. Dafa Alba Roohan khazain juz.18 uk.231

Hii maana yake ni kuwa Mirza anajithibitisha kuwa yeye ni nabii wa kweli na mungu aliyemtuma yeye ndiye Mungu wa kweli lakini kwa vile Mirza ni mzushi mkubwa kabisa na ni wakala wa shetani  na huyo anayeitwa mungu wake anayemshushia wahyi si chochote bali ni sheitwani!!! Tutaona zaidi uko mbeleni katika sehemu inayofuata itadhihirishia zaidi kuwa huyu anayemtuma Mirza ni sheitwani aliyemlaghai Mirza na kufanikiwa kuingia naye motoni.

 

MIRZA ADAI ULIMI WA MUNGU UNA UGONJWA FULANI

Wapendwa katika imani Quran tukufu na hadith sahihi za Mtume zinatuthibishia kuwa baada ya kuja nabii mtukufu Muhammad [s.a.w]unabii umekoma na wahyi pia umekoma hata hivyo Mirza yeye bado anafanya ugagalizi na kudai kuwa yeye ni nabii wa mungu na mpokezi wa wahyi kutoka kwa mungu miongoni mwa madai chungu mzima aliyoyatoa  kuhalalishia upotovu wake ili kuhalisha madai yake ya unabii hapa mirza anadai ikuwa ulimi wa Mungu una ugonjwa fulani Mirza anasema

 

‘Je mtu mwenye akili timamu anaweza kukubali kuwa eti katika zama

hizi mungu anasikiliza lakini hazungumzi kitu sasa basi swali linakuja

kwa nini hazungumzi je amepata ugonjwa kwenye ulimi wake?”

Taz.Zamima braheen ahmadiyya sehemu ya 5,Roohan khazain juz 21uk321

Mirza anaendelea kusema hapa sasa anasema yeye kaambiwa na mungu kuwa ametoka katika katika kiti chake cha ufalme mirza anasema kaambiwa na Mungu wake[sheitwani] hivi

“wewe kwangu unatoka katika kiti changu cha ufalme”

Taz.Haqiiqatu-l-wahyi,Roohan khazain juz.22uk89

 

MIRZA ADAI YEYE NI MUNGU

Mirza hapa sasa anazidi kututhibitisha wahyi wake ni washetani sasa hapa anadai kuwa ni mungu mirza anasema

“Nimeona katika ndoto yangu kuwa mimi ni mungu na nikaamini

kuwa ni kweli” Taz.kitabul-bariyah,Roohan khazain juz.3uk.103

 

MIRZA ADAI MUNGU KAINGIA KATIKA MWILI WAKE NA WAMESHIRIKIANA KUUMBA

Mirza anasema

“Mungu aliingia mwilini mwangu….na katika hali hiyo nikawa nasema tunataka

Pepo mpya na ardhi mpya na mbingu mpya kwa hiyo nikaanza kuumba mbingu

Na ardhi katika umbile dogo ndani kukiwa hamna utaratibu wa vitu tofauti

Kisha kwa matakwa ya mungu nikaumba mfumo wa vitu mbalimbali ni

Mimi nikawa ninajiona kumbe nina uwezo wa kuumba hivyo nikaumba

Mbingu na dunia nikasema tumeipamba mbingu na dunia kwa mataa

Kisha nikasema kuwa sasa tutaumba mtu kutokana na udongo wa ardhi”                              Taz.  Kitabul bariyyah,Roohan khazain juz.3uk.104-105

Mirza anaendelea kudaiyeye na mungu kitu kimoja anasema kaambiwa hivi na mungu wake

“Wewe kwangu ni kama kitu kimoja na dhati moja”Taz.haqiiqatul wahyi,Roohan khazain juz.22 uk 89

 

MIRZA ADAI KAGEUZWA NI MKE WA MUNGU

Mirza anasema

“kama vile maryamu roho ya Issa ilipulizwa mwilini mwake na mimi

pia nikawa mja mzito na baada ya miezi mingi kutokana na ufunuo

uliomo katika barahheen Ahmadiyya sura ya 4uk 556 nikageuzwa kutoka

maryam na kuwa Issa bin Maryam’Taz,kishtee-e-nooh,Roohan khazainjuz.19uk50

 

 

 

kwa hiyo wapenzi wasomaji mnajionea vituko hivyo vya Mirza yaani anabadilika kutoka katika mirza bin chiragh bibi na kuwa Maryam alafu anakuwa mja mzito wa miezi kumi na baadaye  anajizaa mwenyewe na kuwa Issa na kisha anadai kuwa yeye ndiye Issa bin maryam masih aliyeahidiwa

MIRZA ADAI KAPATA HEDHI NA KUWA   MWANA WA MUNGU

Wasomaji nadhani mtaona tunatumia maneno makali lakini ndio hivyo maana mirza mwenyewe ndio katamka hivyo nasi anatufanya tufikie hapo kwani nia yetu ni kumdhihirisha waziwazi watu wote waone upotovu wake na yote hayo tunayanukuu kutoka katika vitabu vyake kama yalivyo ninyi wenyewe mtapima na kumuona alivyokuwa punguani sasa hapa anadai kapata hedhi Mirza anasema kuwa mungu wake kamwambia hivi

    “Babuillah bukhsh anataka kuona damu yako ya mwezi au japo apate taarifa juu

       yako lakini mungu atakuonesha fadhila zake ambazo zitadumu daima na         mwilini mwako   kuna hedhi bali mtoto ndiye anaendelea kukuwa mtoto huyo ni kama mwana wa mungu”Taz.tatumma haqiqatul wahyi, Roohan khazain juz.22 uk 581

tukiendelea zaidi na uchambuzi wetu hapa sasa Mirza anadai mungu kawa kama mwanaume na yeye ni kama mwanamke

    “wakati Fulani Hazrat Masih muwuud alieleza hali hii kuwa wahyi kuwa ulimshukia katika hali ambapo mungu alikuwa kama mwanamme na yeye kama mwanamke na mungu akaonesha ulijali wake kwake”[kwa wanaoelewa dokezo hili linatosha]Taz.islam qurbqn track no 34by Qazi yar mohammed qadiyyan ASTAGHFIRULLAH wasomaji tokea kuja kwa wanadamu hakuna hata mmoja ambaye amethubutu kutoa madai kama hayo hata wale manabii wa urongo je tujiulize

ni mungu gani huyo anayeweza kumgeuza nabii wake kuwa mkewe bila shaka huyo anayemzungumza Mirza si mungu bali ni shetwani na nabii wake ndioMirza

 

MIRZA ADAI TENA SASA YEYE NI MWANA WA MUNGU

 

Mirza anasema kaambiwa hivi katika ufunuo na huyo mungu wake [sheitwani]

   

 “Wewe [Mirza]kwangu mimi ni kama mwanangu kuanzia zama hizi,wakristo wapumbavu waliokuwa wamemfanya yesu ni mungu kwa hiyo busara ya mungu ikataka maneno mengine zaidi yatumike kwa mtu mnyenyekevu ili macho ya wakristo yafumbuke na wayaelewe hayo maneno ambayo kwayo wamemfanya Yesu ni mungu na katika umma huu ni mtu mmoja tu ambaye kwa maneno hayo yametunika”Taz.Haqiqatull wahyi, Roohan khazain Juz.22 uk.89

 

MIRZA ADAI MUNGU ATAKUJA KAMA MWIZI

Mirza anaendelea kueleza upotovu wake sasa anasema “mungu yule ambaye katika milki yake mna kila chembe mtu atakimbilia wapi kumkwepa yeye anasema kuwa atakuja kimyakimya kama vile mithili ya mwizi”Taz.tajliyat e llahiyah,Roohan khazain Juz.20uk396

 

MIRZA ADAI MUNGU AKIRI KUFANYA MAKOSA

Katika mojawapo ya funuo zinazomjia Mirza mungu wake Mirza anakiri kufanya makosa ufunuo unasema hivi “Akhtee wa Aseeb[mimi nitafanya makosa na nitarekebisha]Taz.Haqiiqatullwahyi ,Roohan khazain juz.22uk106 mirza anaendelea kuufafanua ufunuo huu kwa maneno yake haya anasema “maana ya wazi ya ufunuo huu ni kuwa mimi pia nitafanya makosa na wakati mwingine nitarekebisha yaani ninachotaka mimi nitakitekelezatu na wakati mwingine sitakitekeleza”Taz.Roohan khazain Juz.22 uk 106 footnote

MIRZA ADAI MUNGU ANAFUNGA NA KUFUNGUA SWAUMU

Katika wahyi huu mungu anamuarifu Mirza mungu huyo wa mirza anasema

    “Na mimi nitafunga na kufungua saumu”Taz.Haqiiqatull wahyi,Roohan khazainJuz.22 uk 107

 

MIRZA ADAI MBINGU ZIKO PAMOJA NA YEYE

Ufunuo wake unamwambia “Oh Mirza mbingu na dunia ziko pamoja nawe kama zilivyo pamoja nami”Taz.Haqiiqatull wahyi,Roohan khazainjuz.22uk78

 

 MIRZA ADAI QUR AN NI MANENO TOKA MDOMONI MWAKE

Mirza anasema ‘Qur an ni maneno ya Mungu na tamko la kinywa changu” Taz.Haqiiqatull wahyi Roohan khazain Juz.22uk87

Wapendwa wasomaji

Ni dhahiri kuwa Mirza alikuwa na dhana potofu kabisa juu ya Mungu ambayo haipo katika mafundisho ya uislamu Qur an na hadith pana tafsiri mbili za dhana hii

1.Mirza Ghulam alikuwa ni mwendawazimu,punguani na kwa kweli alisumbuliwa na uwendawazimu alikuwa na matatizo ya kiakili utafiti wa  kisaikolojia na maandiko yake unabainisha mengi kwa hiyo tunapata uthibitisho wa wazi Mirza alikuwa na wazimu kamili pasina shaka katika mjadala huu mfano mmoja tunastahiki kuutaja

“Hazrat saheb[Mirza Ghulam]walizaliwa wawili kulwa na doto pacha wake yaani mwenzie Mirza alikuwa mwanamke jina lake alikuwa anaitwaJanat Janat alifariki dunia baada siku chache baadaya kifo hicho cha ndugu yake wa kike Mirza alisema maneno haya “Mungu ameniondolea mbali jinsia ya uke” Taz. Hayatul un nabi Juzuu ya 1uk 50 mwana saikolojia yoyote yule atakuthibitishia kuwa mtu kamili ni lazima jinsia zote mbili za ume na uke ni lazima kauli hii wa Mirza inabainisha kuwa kwa tatizo la kijinsia lilikita katika kichwa cha Mirza tatizo hili ikichanganya na udhahifu wake wa kijinsia,ulevi wake wa pombe na kuanguka kwa familia yake kiuchumi na uchu wake wa kupenda madaraka na pesa kama alivyokiri yeye mwenyewe katika maandiko yake mengi hatimaye vikamtia uchizi .nukta nyingine muhimu ni kuwa upunguani wa hisia katika kichwa Mirza yumkini ndio sababu ya ufunuo wake kubadilisha jinsia yake mara anajiita yeye bibi maryamu na akapata mimba ya ujauzito wa yesu na mara anazini na mungu wake[sheitwani]

 

MIRZA ALIKUWA ANACHEZEWA NA SHETANI

Kwa hakika pasina shaka katika kipindi Fulani cha uhai wake Mirza alikuwa akifanya mambo ya ukuhani na ilithibi kwamba wale wenyeuzoefu na mambo hayo ya ukuhani basi muda mfupi baadaye hupata njozi,ndoto na sasa kama mtu anafanya hayo chini ya uangalizi wa  mcha mungu basi  anaweza kumdhibiti  lakini Mirza hakuwa chini ya uthibiti wa wacha mungu matokeo yake ndio hivyo akawa chini ya usimazi wa

Sheitwani aliyalaaniwa kwani kuhusiana na masuala ya ndoto au njozi watu wengi hawajui kuwa ni wakati gani ndoto au njozi zaweza kusadikika na matashi ya mtu mara nyingi yaweza kumpelekea adhani kuwa anaongea na mungu wakati si hivyo

Kumbuka kuwa sheitwani ni adui yetu wa wazi kabisa kwetu wanadamu anataka kuwaangamiza wanadamu kwa njia mbalimbali kwa mfano yaweza funuo za mtu kama mirza zikamjia kama ni za kweli kumbe zinatoka kwa shetani kwa sababu shetani ni mrongo mkubwa wakati mwingi hujenga urongo mkubwa unaofanana na kweli il akujenge imani umuamini  matokeo yake anakuangamiza yote hayo Mirza anafahamu hivyo na amekubali Taz.Haqiqatul wahyi,Rooham khazain juz.22uk3 lakini Mirza alijisahau hakujitambua kabisa matokeo yake akautupa uislamu na kukufuru kwa kufuata funuo za urongo za shetani

 

  Mwenyezi mungu atukinge na sheitwani aliyelaaniwa Ameen

   Salamu za amani ziwe juu ya wale wanaofuta uongofu

   Wabillah Tawfiiq

Dr. Syed Rashid Ali P. O Box 11560 Dibba Al-Fujairah United Arab Emirates rasyed@emirates.net.ae http://alhafeez.org/rashid/

:   admin       (   )
: 0 /5 ( 0 )

: 26-11-2009

: 2140