:Open Letter to Mirza Masroor
  Non - Arabic Articles Swahili

: Open Letter to Mirza Masroor
: webmaster
Bismillahir Rahmanir Rahiim

Anti Ahmadiyya Movement

Barua ya wazi kwa Mirza Masroor Ahmad khalifa wa 5

wa Mirza Ghulam Ahmad Qadiani na Amir wa Jumuiyya ya Ahmadiyya

[By Dk sayed Rashid Ali]

Bwana Mirza Masroor Ahamad Qadiani Saheb Salaam ala mani taba’a al huda

Natumai tayari umekwishapata barua yangu ya wazi iliyotangulia ambayo ilitolewa katika tolea la kiurdu la AlFatwa internation[no29] bado ninasubiri jibu kutoka upande wako kwa kuzingatia barua yangu hiyo ningependa kukuomba unipe majibu ya masuala yafutayo mapema uwezavyo;

1] katika mubahilla baina ya Illiar Suttar na Mirza Tahir Ahmad Qadiani kiongozi wa zamani wa jumuiyya ya Ahmadiyya ni nani alishinda changamoto hiyo ya mubahila? Mirza Tahir au Illias Suttar nataka kujua msimamo rasmi wa jumuiyya ya Ahmadiyya katika kadhia hii;

kwa kukumbusha tu mtangulizi wako Mrza Tahir wakati wa Jalsa salana ya mwaka 1999 alitangaza hadharani kukubali kwake kuwa mmoja wa washiriki katika changamoto ya mubahila iliyotolewa kwa bwana Illias Sutar na Murabi wa jumuiyya ya Ahmadiyya mjini Karachi Mohamed Usman Qadiyyan tarehe 20/5/1999 ni upi msimamo rasmi wa jumiyya yako kuhusiana na matokeo ya mubahila hii. Nani aliyepigwa laana na Allah kutokana na mubahila huu?

2]Ni sera ya Jumuiyya kuwa mtu muongo hufa mkweli angali hai.Mirza Tahir alifariki dunia tarehe 19/4/2003 wakati ambapo Syed Abdul Hafiz Shah kiongozi wa harakati za kiislamu dhidi ya Ahamadiyya ambaye mara kwa mara kadhaa alimpa changamoto ya mubahila Mirza Tahir, alifariki dunia tarehe2/7/2003 Mwezi mmoja na siku 13 baada ya kifo cha Mirza Tahir sasa je uko tayari kutangaza hadharani kuwa Mirza Tahir alikuwa mrongo? Na kwa sababu hiyo pia utangaze hadharani kuwa Mirza Ghulam Qadiyyan naye pia alikuwa ni mrongo!!!

3] Je wewe unafikiri nini juu ya ya idadi ya watu wanaoingia katika ukadiani? Je hudhani kuwa Mirza Tahir alikuwa akidanganya ulimwengu juu ya ongezeko la watu wanaojiunga katika Ahmadiyya? Au je zile takwimu zilizokuwa zikitolewa katika Jalsa Salana tokea mwaka 1993zilikuwa ni sahihi kweli?

Kwa kukumbusha tena ifutayo ni idadi ya watu waliotangazwa kuingia katika ukadiyyani na Mirza Tahir katika kipindi cha mika 10 tokea mwaka 1993 ni kama if

uatavyo..

 

Mwaka                                       Idadi 1993                                        243,008 1994                                        421,753 1995                                        847,753 1996                                     1,602,721 1997                                     3,004,585 1998                                     5,004,591 1999                                     10,820,226 2000                                     41,308,975 2001                                     80,106,721[idadi iliyotolewa katika Jalsa ya Ujerumani mwezi August 2001] 2002                                     20,654,000

 

 

 

jumla kwa miaka 10 ni 160,875,605[tazama Al Fazl interanational uk 4 juz.no.33,tarehe 16-22/8/2002]

4] katika Jalsa Salana ya 2003 kule uigereza[UK] wewe umetangaza idadi ya waahamadiyya [ makadianai] wapya kuwa 800,000 tokea Jalsa salana iliyopita 2002.ukilitazama jedwali, kwa ufasaha utaona kuwa makadiani wapya wa hivi sasa ni chini ta asilimia moja 1% ya idadi ya 2001 ni nini sasa kiini cha punguo hili kwa mtazamo wako?

5] Je unazo takwimu rasmi za hivi karibuni za watu walioingia katika ukadiani tokea 1993.Je ni wangapi kati yao wanaoendelea kuwa wafuasi wa Ahmadiyya [ukadiani] na wangapi wametoka katika jumuiyya tokea wakati huo?

6] Je una jibu gani rasmi kuhusiana na hatua ya sheikh Raheal Ahmad aliyekuwa kiongozi wa juu wa jumuiyya ya Ahmadiyya kule ujerumani[German] na bwana Abu Bakr wa Marekani[USA] ambao kwa sasa wametoka katika jumuiyya?

7]Je wewe uko tayari kufanya mubahila[maapizano]au munazira na mimi juu ya suala hili kwamba mimi natangaza wazi hadharani kuwa Mirza Ghulam Ahmad Qadiani alikuwa ni mrongo katika madai yake ya unabii,umasih,umahd …! Niko tayari kuja London mahali na wakati unaotaka wewe kwa ajili ya maapizano mubahila/munazira na wewe mbele ya hadhara.pengine hii itakuwa fursa nzuri kwako kuwathibitishia wafuasi wako ukweli wa Mirza Ghulam Qadiani ambaye wewe unadai kuwa khalifa wake.

natarahia jibu lako haraka kwa suala hilo tafadhali sana usifanye hila kulikwepa jambo hili. Iwapo utaamua kukacha kurejesha jibu itakuwa ni hatia kwa upande wako,ukiwa kama kiongozi wa harakati za Ahmadiyya usiwe mwoga toka hadharani tufanye mubahila ukikataa mubahila basi nafsi yako itawajibika siku ya hukumu kwa kuongoza kumuiyya ya upotovu kwa kudanganya na kupoteza wafuasi wanaokuamini tunakusihi toka tuapizane kama ninyi Ahmadiyya ni wakweli ukikataa kujibu hapa duaniani basi utajibu siku ya kiama

wassalam kwa wote wanaofuata hidaya

Dr.Syed Rashid Ali Anti Ahamadiyya Movement in Islam P.O Box 11560 Dibba Al-Fujairah United Arab Emirates rasyed@emirates.net.ae Swahili Homepage Main Homepage

:   admin       (   )
: 0 /5 ( 0 )

: 26-11-2009

: 2078