:Qadianis Hopes Dashed
  Non - Arabic Articles Swahili

: Qadianis Hopes Dashed
: webmaster

Matumaini ya Makadiani Yatoweka

 

(Na Dkt. Saiyd Rashid)

 

Assalaam Alaykum

 

Makadiani hawafahamiki kwa Waislamu wengi; wao ni wafuasi wa nabii wa uwongo, Mirza Ghulam ambaye alishirikiana na utawala wa Mwingereza kudhoofisha Uislamu Bara hindi mwishoni mwa karne ya 19, na mwanzoni mwa karne ya 20.

 

Makadiani hujifanya Waislamu lakini si mara, si mara mbili, Kiongozi wao aliwatangaza wafuasi wote wa Muhammad (saw) kuwa ni Makafiri. Kwa maafikiano ya Wanazuoni ulimwenguni na Pakistan, wasifu wa Makadiani umeainishwa wazi kuwa si wa Kiislamu.

 

Wakitumai kunufaika kutokana na kuibuka kwa Musharraf na kusitishwa kwa Katiba ya Pakistan kwa Agizo la Katiba ya Mpito la Musharraf, PCO-(Provisional Constituotion Order) ambayo imefutilia mbali muundo wa Kiislamu wa Taifa la Pakistan, Makadiani wamefanya jitihada nyingine ya kutaka wakubalike kama Waislamu. Alhamdulillah wameshindwa.

 

Tunaijumuisha hapa makala inayoelezea baadhi ya dini ambazo si sehemu ya Uislamu. Kwa ufafanuzi kamili juu ya Makadiani na kwa ajili ya kupata mtazamo wa Uislamu juu ya Mwisho wa Utume wa Muhammad (saw), ipate makala hii ya Allama Maududi katika mtandao huu:

 

http://www.usc.edu/dept/MSA/fundamentals/prophet/finalprophet.html. Tafadhali kumbuka kuwa makala mbili zinafuata:

-Serikali yasema Makadiani si Waislamu

-Kulitusi Neno Uislamu

 

(1) Chanzo cha taarifa:The Dawn 25 February 2000 Friday 18 Ziqa’ad 1420

http://www.dawn.com/2000/text/nat7.htm

 

Serikali yasema Makadiani si Waislamu

ISLAMABAD, Februari 24

 

Watu wanaonasibiana na kundi la Makadiani au kundi la Lahori (ambao hujiita Ahmadiya) bado wanaendelea kuhesabiwa kuwa si Waislamu, hayo aliyasema msemaji wa Wizara ya Sheria mjini hapa siku ya Alhamisi.

 

Alisema kuwa vipengele husika vikiwemo vile vya kifungu cha 3 cha Ibara ya 260 ya Katiba havina mgongano na Agizo la Oktoba 14, 1999 na Agizo Na.1 la Katiba ya Mpito Mwaka 1999.

 

Vipengele hivi na vile vya Kifungu cha 3 cha Ibara ya 260 ya Katiba bado vinaendelea kufanya kazi. Msemaji huyo ameondosha hisia iliyojengwa na baadhi ya watu kwamba baada ya kuja kwa tamko la hali ya hatari la Oktoba 14, 1999 ambapo Katiba imesitishwa na matokeo yake zimeibuka shaka zisizo sahihi kuhusiana na utekelezaji wa vipengele vya Kiislamu katika Katiba na vipengele vinavyohusu Makadiani vilivyojumuishwa katika kifungu cha 3 cha Ibara ya 260.

 

Msemaji huyo alifafanua kuwa Ibara ya 2 ya Katiba ya Mpito Na.1 ya 1999 inabainisha kuwa bila kujali kusitishwa kwa vipengele vya katiba, Pakistan itaendeshwa aghalabu kwa kufuata Katiba.

 

Ufafanuzi unasema: “Vipengele husika vya Kiislamu ikiwa ni pamoja na vipengele vya kifungu cha 3 cha Ibara 260 ya Katiba havina mgongano na Agizo la Oktoba 14, 1999 na Katiba ya Mpito Na.1 ya 1999.

 

Vipengele hivi na vile vya kifungu Na. 3 cha Ibara ya 260 bado vinaendelea kufanya kazi ambapo nafasi ya watu wanaonasibiana na kundi la Makadiani au kundi la Lahori (ambao hujiita Ahmadiya) inabaki vilevile bila kubadilika kwamba watu wanaonasibiana na makundi haya wanaendelea kubaki kuwa si Waislamu.-APP

 

(2) Chanzo cha Taarifa:MSA at University of Southern California

 

------------------------------------------------------------------

 

Qur’an na Sunna ndivyo vyanzo pekee vya imani za msingi za wale wanaojiita Waislamu.

 

Imani hizo ni zipi? Ya muhimu zaidi ni kuwa hakuna mungu ila Allah. Hii ni nusu ya kwanza ya shahada ya kila Muislamu, nusu ya pili ni kuwa Muhammad ni Mtume wa MwenyeziMungu.

 

Kuna nguzo nyingine chache ambazo Muislamu anatakiwa kuzikubali, lakini maelezo zaidi yanapatikana mahala pengine katika tovuti hii. Aidha yanapatikana maelezo juu ya mitazamo potofu ya jumla inayoshikiliwa na Waislamu na wasio-Waislamu.

 

Ukurasa huu umetengwa kwa ajili ya wale wanaoendelea kuyatumia vibaya majina “Uislamu” na “Muislamu” ama kwa makusudi au kwa ujinga. Katika ukurasa huu, tunajaribu kubainisha kwa kifupi ni makundi mangapi ya “kidini” ulimwenguni yanayotumia jina Uislamu ambayo, kwa kweli, yanakiuka waziwazi kabisa mafundisho ya msingi yaliyomo katika Qur’an na Sunna.

 

Makundi yafuatayo ndiyo yanayotajwa hivi sasa:

 

.Kundi linalojiita Nation of Islam (Taifa la Kiislamu)

.Kundi linalojiita The Nation of Gods and Earths (5% Nation of Islam)

.Jumuiya ya Ahmadiya/Kadiani

.Jumuiya inayojiita, The International Comminity of Submitters (Jumuuiya ya Wanyenyekevu Ulimwenguni).

 

 

Kundi la Nation of Islam

 

Wafuasi wa Taifa la Kiislamu (kwa nukuu zote kutoka kwenye Tovuti yao Kuu au kutoka katika machapisho yao), huamini:

 

...Mungu mmoja (Allah) na kwamba Allah alijitokeza kwa Nafsi ya Master W. Fard Muhammad, Mwezi Julai, 1930; huyo ndiye ‘Masihi’ wa Wakristo aliyesubiriwa kwa muda mrefu, na ndiye ‘Mahd’ wa Waislamu...” Hata hivyo, Qur’an, katika Sura ya 4, aya ya 36, inasema, “Muabuduni MwenyeziMungu wala msimshirikishe na chochote...” Na kwa mujibu wa Hadith iliyosimuliwa na Masruq katika Sahih Bukhari, Aisha kasema: “Mtu yeyote akikwambieni kuwa Muhammad kamuona MwenyeziMungu, huyo ni mwongo, kwani MwenyeziMungu anasema: “Macho hayamfikii (kumuona) bali Yeye ndiye anaeyafikia macho.” (6:103).

 

Zaidi ya hivyo, Wafuasi wa Taifa la Kiislamu wanaamini “kufufuliwa kwa wafu-sio kufufuliwa kimwili-bali kufufuliwa kiakili. Pia tunaamini kuwa wale wanaoitwa ‘Wanegro’ ndio zaidi wanaotaka ufufuo wa kiakili; ndiyo kusema kuwa, wao ndio watakaoanza kufufuliwa.”

 

Lakini Qur’an, katika sura ya 20, aya ya 55, inasema: “Katika hii (ardhi) Tumekuumbeni na humo Tutakurudisheni, na kutoka humo Tutakutoeni mara nyingine.” Kwa kulibainisha zaidi hili, Qur’an pia inasema: “Waliokufuru wanadai kuwa hawatafufuliwa. Sema: “Kwa nini? Kwa haki ya Mola wangu nyinyi lazima mtafufuliwa: Kisha lazima mtajulishwa mliyoyatenda . Na hayo ni sahali (rahisi) kwa MwenyeziMungu.” (64:7).

 

Mbali ya tofauti hizo mbili, Wafuasi wa Taifa la Kiislamu pia wanaamini mambo mengine yaliyo kinyume na Uislamu kama ilivyoainishwa katika Qur’an na Sunna, kama vile, “na (Sisi Waislamu weusi tunaamini) ukweli wa Biblia isipokuwa tunaamini kuwa imebadilishwa na lazima itafsiriwe upya ili watu wasinaswe na mambo ya uzushi yaliyoongezwa humo.”

 

Tatizo la imani hii: Mtume wa kweli wa Uislamu aliwaagiza Waislamu kutoikubali wala kuikataa Biblia. Kwa kweli, hakukuwa na maelezo ya kuitafsiri upya.

 

Wafuasi hao wa Taifa la Kiislamu wanasema, “sisi tunaojitangaza kuwa ni Waislamu wema, hatupaswi kushiriki katika vita zinazochukua maisha ya watu. Hatuamini kuwa taifa hili linapaswa kutushurutisha kushiriki katika vita hivyo, kwani hatuna cha kupata kutoka katika jambo hilo mpaka Amerika ikubali kutupa nchi inayohitajika ambapo tuweza kuwa na cha kupigania.”

 

Tatizo la imani hii: Qur’an na Sunna ziko bayana kabisa juu ya wajibu wa kwenda vitani pale mazingira yanapolazimu.

 

Kundi la Gods and Earths (asilimia 5, Taifa la Kiislamu)

 

Ni dhahiri Kundi la Gods and Earth (aslimia 5, Taifa la Kiislamu) ni tawi la lile linaloitwa Taifa la Kiislamu. Kama lilivyo kundi lake mama, imani za kundi hili zinalitambulisha kundi hili waziwazi kuwa liko nje ya wigo wa Uislamu. Kwa kubainisha hili, tunanukuu kutoka (kwenye tovuti yao kuu):

 

.Mtu wa asili ni Mtu mweusi wa Kiasia, ndiye mtengenezaji, ndiye mmiliki, ndiye mtu bora wa sayari ya Dunia, ndiye Baba wa ustaarabu, ndiye Mungu wa Ulimwengu...Mtu mweusi ni mungu na jina lake ni Allah. Mkono, Mguu, Mguu, Mkono, Kichwa.

 

Huku ni kupingana waziwazi na moja ya imani za msingi za Uislamu nayo ni kwamba MwenyeziMungu ndiye Muumba na vyote vilivyosalia (wakiwemo wanadamu-watu weusi wa kiasia au wengine) vimeumbwa, kwa hiyo ni vigumu kimantiki kwa mtu kuwa Allah.

 

Nukuu ya pili hapo juu ni mfano hai wa mwenendo wa kundi la “Nation of Gods and Earths” kutunga imani ambazo, kwa kiasi kikubwa, ni za kuchanganyikiwa. Baadhi ya mifano ya imani hizo ambazo hazihusiani na Uislamu ni “Hisabati na Herufi Kuu”, mtu muovu aitwaye Yakobo, nabii aitwaye W.D. Fard, na imani kuwa watu weusi ndio bora kwa namna fulani.

 

Mtume wa kweli wa Uislamu aliikataa imani hii ya mwisho ya ubaguzi katika hotuba ya kuaga:

 

Enyi watu! Kwa hakika Mungu wenu ni Mmoja na babaenu ni mmoja. Nyote mnatokana na nasaba ya Adam, na Adam aliumbwa kwa udongo. Hakuna ubora kwa Mwarabu juu ya asiyekuwa Mwarabu, wala asiyekuwa Mwarabu juu ya Mwarabu; wala mweupe juu ya mweusi, wala mweusi juu ya mweupe isipokuwa kwa taqwa. Kwa hakika mbora zaidi miongoni mwenu ni yule amchaye Mungu zaidi.”

Kwa ajili ya kulifichua kwa undani zaidi kundi hili pamoja na kundi mama (Taifa la Kiislamu), msomaji mwenye shauku huenda akapenda kuchunguza tawasifu ya Marehemu Malik Al-shabaz (Malcom x).

Jumuiya ya Ahmadiyya/Kadiani

 

Jumuiya ya Ahmadiyya ambayo ilichimbukia Barahindi kwa ufadhili wa wakoloni wa Kiingereza, inaunga mkono imani ambazo haziachi shaka juu ya kuritadi kwao. Miongoni mwa imani zao potofu ni kule kuukana kwao mwisho wa utume wa Muhammad (saw), nguzo ambayo imethibitishwa na Qur’an na Hadith pamoja na Shura ya Maswahaba na Wanzuoni.

 

Qur’an inasema:

 

“Muhammad si baba wa yoyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mungu na Mwisho wa Mitume, Na MwenyeziMungu ni Mjuzi wa kila kitu.” (33:40).

 

Mtume wa kweli wa Uislamu, Muhammad, kasema:

“Banu Israili waliongozwa na Manabii. Pale nabii mmoja alipotawafu, akafuata mwingine. Lakini hakuna nabii atakayekuja baada yangu; ni Makhalifa tu watakaonifuatia”. (Sahih Bukhari)

 

Ahmadiya ni wafuasi wa mtu mmoja, Mirza Ghulam Ahmad wa kule Qadiani ambaye alizusha dai la unabii na akatumia Hadith za uzushi na kupindisha maana ya baadhi ya Aya za Qur’an ili kujithibitisha yeye mwenyewe. Hata hivyo, Mtume wa kweli wa Uislamu alitahadharisha waziwazi juu ya hatari hii:

 

“Saa haitafika...mpaka takribani “madajjal” (wadanganyifu) thelathini watokee, kila mmoja akidai yeye ni mtume kutoka kwa Allah.” (Sahih Bukhari, Sahih Muslim).

 

Muda mfupi baada ya kutawafu Mtume Muhammad, mtu mmoja aliyeitwa Musailama, mzushi wa dai la unabii, alipigwa vita yeye na wafuasi wake kwa uasi wao. Ni muhimu kuzingatia kuwa huyu Musaillama hakuukana utume wa Muhammad (saw) na wala wafuasi wake hawakuukana.

 

Ni muhinmu pia kuzingatia kuwa ilikuwa ni taarifa potofu iliyolipelekea kabila la Banu Hunaifa kuyakubali madai ya uzushi ya Musaillama. Licha ya hivyo, shura ya Maswahaba ikawatangaza kuwa ni waasi na vita ikaanzishwa dhidi yao. Huu ni uthibitisho unaotosha kuwatangaza Ahmadiya kuwa si Waislamu. Kwa ufafanuzi kamili wa mada hii, rejea makala hii:

 

http://www.usc.edu/dept/MSA/fundamentals/prophet/finalprophet.html

 

Mfano mwingine wa Ahmadiyya kukanusha Qur’an na Hadith ni lile dai lao kuwa Yesu alikufa, na kwamba Mirza Ghulam Ahmad alikuwa mwili wa Yesu.. Kwa kweli, kwa mujibu wa EncyclopaediaBritannica 1985, Mirza Ghulam Ahmad sio tu alidai kuwa yeye ni Yesu bali yeye ni Mtume Muhammad, Mahdi na mungu wa Wahindu, Krishna.

 

Yafaa kurejea katika msingi wa Uislamu ambao ni Upweke wa MwenyeziMungu (Tauhiid): dhana yoyote ya mwanadamu kugeuka kuwa mungu, mbali ya mungu wa Wahindu ambaye ni mmoja kati ya wengi, ni potofu kwa mujibu wa Qur’an.

 

Juu ya hili, Uislamu hauna suluhu, ndiyo kusema, dhambi hii ya Ahmadiya ndiyo ishara ya kwanza kabisa ya kujitoa kwao katika Uislamu. Mwishowe, Ahmadiyya pia wakaikana Jihad, hatua ambayo ilikuwa ni mbinu iliyobuniwa ili kuondosha upinzani wa Waislamu dhidi ya utawala wa Kikoloni wa Waingereza. Kwa ufafanuzi wa kina zaidi juu ya Ahmadiyya, rejea tovuti ya “Anti Ahmadiyya Movement in Islam.”

 

Kundi la Jumuiya ya Wanyenyekevu: The International Community of Submitters

 

Wanyenyekevu, the submitters ni wafuasi wa hayati Rashad Khalifa, mtu aliyedai kuwa ni Mtume wa Allah. Dai hili, lenyewe tu linatosha kuwaondoa wanyenyekevu katika Uislamu kama inavyosema Qur’an:

 

“Muhammad si baba wa yoyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mungu na Mwisho wa Mitume, Na MwenyeziMungu ni Mjuzi wa kila kitu.” (33:40).

 

Mtume wa kweli wa Uislamu, Muhammad (saw) alisema:

 

“Kabila la Banu Israili liliongozwa na Manabii. Alipotawafu Nabii mmoja, akafuatia mwingine. Lakini hakuna Nabii atakayekuja baada yangu, ni Makhalifa tu watakaonifuatia.” (Sahih Bukhari)

 

Upotevu mwingi wa Rashad Khaklifa waweza kuonekana katika hali ya kupumbazika kwake na utabiri wa namba, pumbao ambalo limewapotosha watu chungu mzima katika kipindi chote cha historia.

 

Khalifa alidai kuwa Qur’an ilikuwa na kanuni ya kimahesabu iliyojizunguusha kwa nambari 19. Alikwenda umbali wa kuondoa aya mbili za Qur’an eti kwa sababu kwa mujibu wa maelezo yake yeye, “Neno ‘God...’ haliwi kigawe cha namba 19 na “jumla ya namba za aya zote ambazo neno Mungu linajitokeza ni...19x6217...Iwapo aya iliyokosewa 9:129 ikijumuishwa, basi kanuni hiyo hutoweka.” Kwa kuikana aya moja ya Qur’an, Wanyenyekevu wanajitumbukiza wenyewe kwenye hukumu ya aya nyingine.

 

“Je! Mnaamini baadhi ya Kitabu na kukataa baadhi? Basi hakuna malipo kwa mwenye kufanya haya katika nyinyi ila ni fedheha katika maisha ya dunia; na Siku ya Kiama watapelekwa katika adhabu kali...”(2:85).

 

Ni jambo muhimu kuzingatia kuwa Khalifa huyu alikuwa ni mtabiri wa namba ambaye aliitendea uadilifu taaluma yake potofu, akatabiri Mwisho wa dunia. Lakini MwenyeziMungu Anasema hivi:

 

“Wanakuuliza juu ya Saa hiyo (yaani Kiama) kutokea kwake kutakuwa lini? Sema: “Ilimu yake iko kwa Mola wangu (tu). Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haitakufikieni ila kwa ghafla.” Wanakuuliza kama kwamba wewe uliitafuta. Sema: “Ilimu yake iko kwa MwenyeziMungu.” Lakini watu wengi hawajui.” (7:187).

 

Wanyenyekevu pia wanakataa Sunna ya Mtume Muhammad (saw)-sio baadhi tu, bali yote. Kwa mtazamo wa wanyenyekevu, Sunna siyo chanzo cha Uislamu. Matatizo ambayo jambo hili linayaleta ni mazito kwani kwa kufanya hivyo, wanyenyekevu wamekhalifu wajibu wao wa

 

Kuswali Sala za faradhi, nguzo ya pili ya Uislamu

Kutoa Zaka, nguzo ya tatu ya Uislamu

Kufunga Swaum, nguzo ya nne ya Uislamu

Kufanya Hija, nguzo ya tano ya Uislamu

 

Kwa nguzo nne kati ya tano za Uislamu kuondolewa, wanyenyekevu wana nafasi finyu ya kulitia nguvu dai lao kuwa wao ni “Waislamu”

 

Mtume wa kweli wa Uislamu (saw) aliwatahadharisha Waislamu juu ya mtego huu. Kasimulia Abu Rafi:

 

Mtume (saw) kasema: Nisimuone mmoja wenu akiegamia kochi wakati anaposikia jambo fulani kuhusu mimi ambalo mimi nimeliamrisha au kulikataza (yaani katika Sunna) halafu akasema: “Sisi hilo hatulijui. Tulichokikuta katika Kitabu cha Allah (Qur’an) ndicho ambacho sisi tumekifuata.” Kitabu cha 40, Namba 4588 cha Sunan Abu Dawud

:   admin       (   )
: 0 /5 ( 0 )

: 26-11-2009

: 1944