عرض المقال :Part 1..Finality of Prophethood by Maudodi
  الصفحة الرئيسية » مـقـالات الموقـــع » كشف البلية بفضح الأحمدية » Non - Arabic Articles » Swahili

اسم المقال : Part 1..Finality of Prophethood by Maudodi
كاتب المقال: webmaster
Din Al- Ansafi aliyefariki duniya mwaka 710 Hijiriya, katika tafsiri yake, Madark-ut-Tanzil, ameandika hivi: “Na yeye Muhammad ndiye ambaye ameumaliziya mlolongo wa Mitume.. Kwa maneno mengine, yeye ni mwisho wa Manabii wote. Mwenyezi Mungu hatateuwa tena Nabii baada yake. Kuhusu Nabii Isa (a.s) inaweza kusemwa kuwa yeye ni miongoni mwa wale walioteuliwa kuwa Manabii kabla ya zama za Muhammad (s.a.w). Na pale Nabii Isa atakapokuja tena, atakuwa mfuwasi wa shariyah ya Muhammad (s.a.w) na atakuwa miyongoni mwa waumini wa kawaida”.(uk.471) Alamaa Alau-din Bughdadi aliyefariki duniya mwaka 725 Hijiriya, katika tafsiri yake iitwayo Khazin, ameandika hivi: “Wa khatam–un-Nabiyyin”, kwa maneno mengine, Mwenyezi Mungu amekamilisha utume kwa Muhammad. Baada yake hadi mwisho wa duniya, hakuna tena unabii wala hakuna mshirika wake katika unabii..”Wa KanAllahu Bikulli Shaiin Alima” Mwenyezi Mungu anajuwa kuwa hakuna Nabii atakayekuja baada yake. (uk 471-472). Alamaa Ibn Kathir aliyefariki duniya mwaka 774Hijiriya, katika tafsiri yake mashuhuri sana iitwayo Tafsir Ibn Kathir , ameandika hivi: “Ndiyo kusema aya hii ni uthibitisho wa wazi wa ukweli kuwa “hakuna Nabii atakayekuja baada ya Muhammad (s.a.w) na inaposemwa kwamba hakuna Nabii atakayekuja baada yake basi ndio hitimisho la jumla kuwa hakuna Mtume atakayemfuatiya kwani ofisi ya utume ina mvumo zaidi ya ofisi ya Nabii. Kila Mtume ni Nabii lakini si Manabii wote ni Mitume. Yeyote anayezusha dai la Unabii baada ya Muhammad ni Muwongo, Mvurugaji, Mzushi, mtovu wa maadili, na mpotoshaji hata akiwa na mauzauza au mazingaombwe. Yeyote yule atakayezusha dai hilo anaingiya katika kundi hili (Taz. Juzuu ya 3 uk.493-494). Allamaa Jalal-Ud-Din Suyut aliyefariki duniya mwaka 911Hijiriya, katika Tafsiri yake iitwayo Jalalain, ameandika hivi: ”MwenyeziMungu ajuwa fika ukweli kuwa hakuna Nabii atakayekuja baada ya Muhammad na pale Isa (a.s) atakapokuja tena duniyani ataishi kwa kufuwata shariya ya Muhammad” (uk.768) Alamaa Ibn Nujaim aliyefariki duniya mwaka 970 Hijiriya, katika kitabu chake mashuhuri cha kanuni za fiqh kiitwacho Al Ashbah wan-Nazair, Kitab -us-Siyyar: bab: al Radda, ameandika hivi: “Mtu asiyemuitakidi Muhammad kama Mtume wa mwisho wa Allaha si Muislamu kwani kuamini Unabii wa Muhamad kuwa ni wa mwisho ni moja kati ya vipengele vya msingi vya imani ambavyo Muislamu lazima avielewe na kuviamini (uk 179). Mulla Ali Qari aliyefariki duniya mwaka 1016 Hijiriya , katika tafsiri yake, Fiqh Akbar ameandika hivi; “Kuzusha dai la Unabii baada ya kipindi cha Mtume wetu Muhammad (s.a.w) ni ukafiri mkubwa , hili ni tamko la pamoja la ummah wa Kiislamu (uk. 202). Sheikh Ismail Haq aliyefariki duniya mwaka 1137Hijiriya akisherehesha aya husika ameandika hivi katika tafsiri yake Ruh-ul -Bayan.” Asim hulisoma neno Khatam kwa fat-ha juu ya herufi te ambayo maana yake ni kifaa cha kupigiya muhuri na kufunga kama vile “Printer” mashine ya kupigiya chapa. Maana ya neno hilo ni kwamba, Mtume mtukufu alikuwa mwisho wa Manabii na MwenyeziMungu ameifunga kabisa ofisi ya unabii kupitiya utume wake. Katika lugha ya Kiajemi (kipersia) maana kama hiyo inaelezwa kwa istilahi “Mohar Paighambran”, Komeo au kifungio cha Manabii, yaani kuja kwa Muhammad kumefunga mlango wa unabii na hivyo ule mlolongo wa Manabii umeishiya kwake. Wasomaji wengine wanalitamka neno Khatim kwa qasra chini ya neno te ambayo maana yake ni kusema kuwa Muhammad alikuwa Mtume aliyefunga milango ya unabii. Katika lugha ya kiajemi (kipersia) maana hiyo inaelezwa kwa istilahi Mohar konindai Paighambran komeo la Manabii, kwa hiyo, kwa namna zote mbili,neno khatam linabeba maana ile ile moja.. Kwa hiyo Maulamaa wa Umati Muhammad watarithi tu hadhi ya utakatifu wa kiroho kutoka kwake lakini urithi wa hadhi ya unabii haupo tena, kwani Muhammad amefunga kabisa ofisi ya unabii kwa zama zote zijazo... Kuja tena kwa nabii Isa (a.s) baada ya Muhammad hakupingani na mwisho wa unabii kwa Muhammad. Maneno Khatam-un-Nabiyyin yanabainisha wazi kuwa hakuna mtu mwingine atakayeteuliwa kuwa Nabii baada ya Muhammad (s.a.w). Nabii Isa (a.s) alikwishateuliwa kuwa Nabii kabla ya Muhammad na yeye Isa atakuja kuwa mfuwasi wa shariya ya Muhammad (s.a.w). Nabii Isa (a.s) atasali swala kwa kuelekeza uso upande wa Qibla alikoelekeya Muhammad (s.a.w). Nabii Isa (as) atakuwa miyongoni mwa Waumini Waislamu. Yeye hatapokeya wahyi wowote kutoka kwa MwenyeziMungu wala hatoleta sheriya mpya; ataishi kama mfuwasi wa Muhammad (s.a.w). Dhehebu la suni (Ahl-Sunnat wal Jama’a (Suni) wanaitakidi kuwa hakuna Nabii atakayekuja baada ya Mtume mtukufu (s.a.w) kwa sababu MwenyeziMungu amesema “Wa-lakin rasul Allahi wa Khatama-un-Nabiyyin”..., na Mtume amesema: La Nabiya Ba’d (hakutakuwa na Nabii baada yangu). Hivyo , yeyote anayesema kuwa kuna Nabii atakayemfuatiya Muhammad (s.a.w) atakuwa Murtad kwa sababu amekanusha kipengele cha msingi cha imani. Halikadhalika yeyote anayeutiliya shaka mwisho wa unabii wa Muhammad naye piya atatangazwa kuwa ni kafiri, kwani maelezo yote hayo yamepambanua haki na batili na dai lolote la Utume baada ya Muhammad ni batili kabisa” Katika Fatawa-i-Alamgiri iliyokusanywa na wanazuwoni wa Barahindi kwa agizo la Aurangzed Alamgir, katika karne ya 12 Hijiriya, imeandikwa hivi: “Mtu asiyemuitakidi Muhammad kama Mtume wa mwisho wa MwenyeziMungu, si Muislamu na, na kama mtu huyo anadai kuwa yeye ni mtume au nabii, atatangazwa kuwa ni murtad”. (Juz. 2, uk.263). Allama Shoukani aliyefariki duniya mwaka 1255Hijiriya, katika tafsiri yake, Fath-ul-Qadiir ameandika hivi: Watu wengi wamelisoma neno Khatam kwa Qasra chini ya te lakini “Asim hulisoma neno hilo hilo kwa fat-ha juu ya te. Kisomo cha kwanza kina maana kuwa Muhammad alikamilisha mlolongo wa Mitume yaani kwa maneno mengine Mtume Mtukufu alikuja mwishoni kabisa mwa Mitume wote. Kisomo cha pili kina maana kuwa Mtume mtukufu alikuwa komeo ambalo kwalo ofisi ya unabii ilifungwa kabisa; na kuja kwake kukaleta rehema kwa kundi la Mitume wa Allah. Allama Alusi aliyefariki duniya 1270Hijiriya, katika tafsiri yake, Ruh-ul-Ma’ani, ameandika; neno nabii ni la jumla, lakini neno “Mtume” lina uzito mahususi. Ndiyo kusema pale Nabii anapoitwa “komeo la Manabii basi ni lazima piya awe “komeo la mitume”. Maana ya ile nafasi ya Mtume mtukufu ya kuwa ‘Mwisho wa Manabii na Mitume wote ni kwamba kwa kwa kupandishwa kwake katika hadhi ya Unabii katika duniya hii, basi hadhi hiyo ndiyo basi imekoma na hakuna mtu anayeweza kuifikiya hadhi hiyo hivi leo.” (Juz. 22 uk.32). “Yeyote anayejidai kupokeya wahai kutoka kutoka kwa Allah kama nabii baada ya kuondoka Muhammad, atatangazwa kuwa ni kafiri. Hakuna tofauti ya rai miongoni mwa Wanazuoni juu ya jambo hili.”.(Juz. 22, uk. 38). Uthibitisho wa Kitabu cha MwenyeziMungu kuwa Muhammad ni Mwisho wa Mitume uko wazi. Hadith zimelifafanuwa bayana hili na Umma umeafikiyana juu ya hili. Ndiyo kusema anayetowa dai la kupinga msimamo huu atatangazwa kuwa ni murtadi (Taz. Juz. 22, uk. 39).

Hizi ni fafanuzi za waja waongofu, Mafuqaha, Wanazuwoni wa Hadith na Mufasiruna wa kila nyanja ya Uislamu tokeya Bara Hindi hadi Morocco na Hispania (Andulus), na tokeya Uturuki hadi Yemen. Tumeonesha miyaka yao ya kuzaliwa na kufa katika kila tukiyo ili msomaji kwanza atambuwe kuwa orodha hii inajumuisha Wanazuoni mashuhuri wa kila karne ya historiya ta Uislamu iliyoanziya baina ya karne ya kwanza na ya kumi na tatu.

Tungeliweza hata kuongeza fafanuzi za Madaktari weledi wa Uislamu wa karne ya kumi na nne; lakini tumewaacha Maulamaa wa karne ya kumi na nne kwa makusudio maalum kwa sababu mtu fulani angeweza kusema kuwa labda Wanazuwoni hawa walikuwa wamefafanuwa maana ya Khatam-i-Nabuwat kama “komeo la Mitume” ili kukanusha dai la Mitume wapya wa zama hizi.

Hivyo, haiwezi kusemwa kuwa Maulamaa wa karne zilizopita walikuwa na chuki dhidi ya watu wa zama za leo wanaodai kuwa ni Mitume. Maandiko piya yanadhihirisha bila shaka yeyote kuwa tokeya karne ya kwanza hadi leo hii ulimwengu wa Waislamu, kwa ujumla, umelichukuliya neno Khatam-un-Nabiyyin kwa maana ya “Mwisho wa Mitume wote”.

Waislamu wa vipindi vyote wamekuwa na imani moja kuwa ofisi ya utume imefungwa baada ya kuja kwa Mtume mtukufu (s.a.w). Hapajawahi hata kidogo kuwa na tofauti ya rai miongoni mwa Waislamu kwamba mtu yeyote anayediriki kujinadiya utume na wale wanaoamini dai la utume, wote hao wamejitowa nje ya wigo wa Uislamu.

Sasa ni juu ya watu wote wenye akili timamu kukata hukumu kuwa kutokana na ushahidi wote huu mzito; maana ya wazi ya kamusi ya kirai “Khatam-un-Nabiyyin”, tafsiri ya aya ya Qur’an kwa mawanda yake sahihi, ufafanuzi wa Mtume mwenyewe, muwafaka juu ya utume kuishiya kwa Muhammad uliofikiwa na Shura ya Umma mzima wa Waislamu ulimwenguni tokea Maswahaba wa Mtume mtukufu hadi waislamu wa leo.

Ni mwanya gani tena uliobaki wa kupachikiya tafsiri nyingine na ni hoja gani wanayoweza kuitowa kwa ajili ya kumfunguliya mlango wa utume mzushi yeyote yule.

Isitoshe watu hawa wanawezaje kutambuliwa kama Waislamu kwa sababu siyo tu wametowa rai yao kwa ajili ya kufunguwa mlango wa utume bali piya wamempandisha mtu katika daraja la Mitume wa Mungu na wamekuwa wafuwasi wa Muwovu huyo? Kwa mnasaba huu mambo haya matatu ni ni muhimu kuyazingatiya.

Je Mungu ni Adui wa Imani yetu?

Kwanza kabisa, Utume ni jambo nyeti. Kwa mujibu wa Mtume mtukufu utume ni kipengele cha msingi cha Imani, na kwamba yule anayeamini utume ndiyo muumini na yule asiyeamini ni Kafiri. Kama mtu hamuwamini Mtume, basi huyo ni Murtadi. Vile vile kama ataamini dai la mtu anayedai utume, mtu huyu huwa kafiri.

Katika jambo hilo nyeti na muhimu Mungu Muweza wa yote, kwa hakika, hawezi hata kidogo kudhaniwa kuwa ameteleza. Kama kumgelikuwa na Mtume baada ya kipindi cha Muhammad MwenyeziMungu angeliutangaza bayana uwezekano wa kuja nabii mwingine.

Katu Mtume wa Allah asingelitawafu bila kuwabashiriya watu wake kuwa Mitume wengine wangekujs baada yake na kwamba wafuwasi wake lazima wawaamini Mitume hao wa baadae.

Je Mungu na Utume Wake walikuwa na niya yeyote ya kudhoofisha imani yetu kwa kutuficha uwezekano wa kufunguka mlango wa unabii na kuja nabii mwingine baada ya kipindi cha Muhammad na hivyo kutuwacha sisi katika utatanishi kwamba kama tusipoamini unabii wa nabii mpya basi tutatoka katika Uislamu?

Zaidi ya hivyo, piya tungeliwekwa gizani na Mungu na Mtume Wake juu ya jambo hili, lakini kinyume chake walitowa maelezo na uthibitisho ambao Umma, kwa miyaka elfu moja miya tatu (sasa miyanne) iliyopita haujayapa maana nyingine na hadi leo bado una mtazamo ule ule kuwa hakuna nabii atakayekuja baada ya Muhammad. Je Mungu na Mtume Wake kweli wangeliweza kuicheza shere imani yetu?

Jaaliya kwa muda tu mlango wa ofisi ya unabii unafunguliwa na Mtume mwingine anajitokeza, sisi, bila shaka, tutamkataa. Kwa kukataa huku, Mungu anaweza kutuhukumu siku ya hukumu; lakini nasi tutawasilisha mbele yake rekodi yote ya maneno na hukumu zake.

Ushahidi huu (SubhanAllah) utathibitisha kuwa Kitabu cha Allah na Sunna ya Mtume Wake zilituchuza na hivyo kutomwamini Mtume mpya na kwa hivyo ametuhukumu kwa ukafiri. Hatuna wasiwasi kuwa baada ya kuitafakari rekodi hii Mwenyezi Mungu ataona yaswihi kutuadhibu kwa kufuru dhidi ya Mtume mpya.

Lakini kama mlango wa utume unafungwa ambapo hakuna Mtume atakayekuja baada ya Muhammad, lakini pamoja na ukweli huu bado mtu analisadiki dai la Mtume mpya, mtu huyo afikirie vizuri kweli kweli ni rekodi gani atakayoiwasilisha mbele ya Mungu katika kujiteteya kwake ili kuepukana na adhabu ya kufuru na kupata nusra?

Mtu huyo anapaswa kupitiya rekodi yake ya kujiteteya kabla ya kufikishwa mbele ya mahakama kuu ya MwenyeziMungu. Ailinganishe rekodi yake na ile tuliyoiwasilisha sisi na kisha ajihukumu mwenyewe iwapo rekodi anayoitegemeya kwa utetezi wake inaswihi kwa mtu mwenye akili timamu na je anaweza kusimama mahakamani kuhimili hatari ya kukabiliyana na shitaka la kufuru na kuadhibiwa kwa shitaka hilo kwa ile aina ya utetezi alionao mikononi mwake?”

Je twahitaji Mtume mpya hivi sasa?

Nukta ya pili, inayohitaji mazingatiyo ni kwamba unabii sio daraja analoweza kupata mtu yeyote anayejiona anastahili kulipata kwa kujitupa kwake katika sala na mambo ya UchaMungu. Wala si kitu kilicho sawa na zawadi au tuzo ya utumishi bora. Unabii ni madaraka ambapo Allah humteuwa mtu fulani katika madaraka hayo kutimiza hitajiyo fulani.

MwenyeziMungu hatumi Mitume kwa mfuwatano wa harakaharaka iwapo hakuna hitajio au pale ambapo hitajio limetimizwa. Tunapoirejeleya Qur’an ili kuona masharti ambayo kwayo Mitume wameletwa ulimwenguni, tunaona kuwa kuna masharti manne ambayo kwao Manabii walitumwa duniyani:

Mosi, kulikuwa na haja ya Mtume kupelekwa katika Taifa fulani ambako hapo kabla hakuna mtume aliyepata kupelekwa na ujumbe ulioletwa na Mtume wa Taifa jingine usingeweza kuwafikiya watu wa Taifa hilo.

Pili, kulikuwa na haja ya kumteuwa Mtume kwa sababu ujumbe wa Mtume wa awali ulikuwa umesahauliwa na watu, au mafundisho ya Mitume waliopita yamevurugwa na hivyo ikawa vigumu kufuwata ujumbe ulioletwa na Mtume husika.

Tatu, watu hawakupokeya sharia kamili ya Allah kupitiya Mtume aliyetanguliya. Hivyo Mitume waliofuwata walitumwa ili kutimiza jukumu la kukamilisha dini ya Allah

Nne, kulikuwa na haja ya Mtume wa pili kushirikiana na Mtume wa kwanza kutimiza jukumu la ofisi moja

Ni dhahiri kuwa hakuna hitajio lolote kati ya mahitajiyo hayo ambalo limesaliya baada ya kipindi cha Mtume Muhammad.

Qur’an tukufu inasema kuwa Nabii Muhammad katumwa kama mjumbe wa kufikisha mawaidha kwa Walimwengu wote. Historiya ya utamaduni ulimwenguni inathibitisha ukweli kuwa kabla ya kipindi cha Mtume Muhammad (saw), masharti hayo mara kwa mara yalijuzu ulimwenguni kwa ajili ya kusambaza ujumbe katika Mataifa yote.

Lakini kwa sasa Mataifa hayahitaji tena Mitume tofauti baada ya kipindi cha Mtume Muhammad. Qur’an tukufu na Hadith na sira ya Muhammad vinathibitisha ukweli kuwa ujumbe wa MwenyeziMungu ulioletwa ulimwenguni na Mtume mtukufu uko vilevile katika muundo wake halisi na asiliya. Ujumbe wa Mtume haujakumbwa na heka heka za uharibifu na upotoshaji.

Hakuna hata neno moja lililoongezwa au kufutwa katika Qur’an tukufu, kitabu alichokileta Mtume duniyani kutoka kwa MwenyeziMungu, wala hakuna yoyote awezaye kutiya nyongeza au kupunguza chochote kutoka humo hadi siku ya kufufuliwa.

Ujumbe ambao Mtume mtukufu ameufikisha kwa maneno na vitendo umesambazwa kwetu katika muundo wake uleule kamili, halisi na asiliya kiasi ambacho tunahisi kama vile tunaishi katika mazingira na zama za Mtume Mtukufu.

Kwa hiyo sharti la pili la kuletwa Mitume ulimwenguni limetimizwa.

Tatu, Qur’an inathibitisha waziwazi kuwa MwenyeziMungu amekamilisha utume kupitiya utume wa Nabii Muhammad. Ndiyo kusema hakuna tena nafasi kwa Mtume mpya kuja kukamilisha kazi ya Mungu.

Kuhusiyana na sharti la nne, iwapo mwenza kweli angehitajika, basi angeteuliwa katika zama za Mtume Muhammad ili kushirikiyana jukumu zito la kipindi chake. Kwa vile hapakuwa na Mwenza aliyeteuliwa sharti hili nalo piya limetimizwa.

Hivyo basi tuangaliye huku na kule kupata sharti la tano ambalo kwalo Mtume mpya labda anaweza kuhitajika baada ya Muhammad. Ikiwa mtu anatowa hoja kuwa watu wametumbukiya katika uovu, hivyo kuna haja ya kuja Mtume mpya kuwarekebisha watu waovu, sisi tutamuuliza hivi;

lini Mtume aliwahi kuja kuanzisha mageuzi tu ambapo tunahitaji Mtume mwingine wa kutekeleza kazi ya mageuzi? Mtume huteuliwa ili awe mpokeaji wa wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na wahyi wa Mwenyezi Mungu hushushwa kwa lengo la kusambaza ujumbe mpya au kusahihisha makosa ambayo yametumbukizwa katika dini baada ya ujumbe wa awali.

Kwa vile Qur’an na Sunna ya Mtume vimehifadhiwa katika muundo wake uleule wa asili na timilifu na kwa vile kazi ya Mungu imekamilishwa na Muhammadi basi hitajio lolote liwalo la kusambaza wahyi wa Mungu hivi sasa limetimizwa ambapo hitajiyo lililopo ni lile la Mujitahidi wa kuondosha maovu ya wanadamu, lakini hakuna nafasi kwa Mitume wengine.

Part 2..Finality of Prophethood by Maudodi

الصفحات[ 1] [2]
اضيف بواسطة :   admin       رتبته (   الادارة )
التقييم: 0 /5 ( 0 صوت )

تاريخ الاضافة: 26-11-2009

الزوار: 4281


المقالات المتشابهة
المقال السابقة
Shatam
المقالات المتشابهة
المقال التالية
Part 2..Finality of Prophethood by Maudodi
جديد قسم مـقـالات الموقـــع
القائمة الرئيسية
البحث
البحث في
القائمة البريدية

اشتراك

الغاء الاشتراك