:AlFatwa 30
  Non - Arabic Articles Swahili

: AlFatwa 30
: webmaster

Bismillah Al-Rahman Al-Rahiim

Harakati za Kiislamu dhidi ya Ahmadiyya

Al-Fatwa International Na.30

Muwasisi: Sayid Abdul Hafiiz Shah

Mhariri: Said Rashid Ali

Watukufu wasomaji

Assalaam Alaikum Warahmatullah Wabarakatuhu

Tunaomba radhi kwa kukawiya kukuleteeni toleo hili jipya la Al-Fatwa. Hili ni toleo linalojumuisha sehemu mbili zilizopita.

Sheikh Said Abdul Hafiiz Shah afariki duniya

Tunahuzuni kutangaza kifo cha Sheikh Sayid Abdul Hafiiz Shah (90) kilichotokeya Julai 2- Inna lillahi wa inna ilaihi rajiuun. Alikuwa kiongozi mashuhuri wa dini kule Sindh Yeye ndiye muwanzilishi wa harakati dhidi ya Ahmadiya na jarida la Al-Fatwa International. Kwa kipindi cha miyaka arobaini iliyopita alikuwa anaishi katika Wilaya ya Thatta nje ya kijiji kidogo cha Gujjo. Sheikh alikuwa akihubiri ujumbe wa amani na upendo ndani ya Sindh. Akaanzisha taasisi ya AlHafiiz Zakiriin Tanziim kwa lengo hilo. Katika maisha yake alikuwa na ujumbe huu; kwamba Waislamu wasahau tofauti zao ndogo ndogo na waungane kwa Kalima Tayyiba kama walivyokuwa Masahaba. Hakuwa Pir kwa maana ya asili ya neno hilo, badala yake aliiasisi taasisi ya Pir- Muriid kwa sababu ndogo tu kwamba kwa mtazamo wake wale warithi wa Masufi wakubwa wana kila sifa isipokuwa hawakurithi imani kutoka kwa viongozi wao waliotanguliya na kwa hali hiyo wameigeuza taasisi hii kuwa ya kibiyashara.

Akasema: Mimi nafundisha lile nilijuwalo bila kuwafunganisha wanafunzi wangu na Piri-Muriidi, na najifunza lile nisilolijuwa. Dhikiri (kumkumbuka Allah) ndiyo ilikuwa ada yake ya maisha na kujenga mapenzi kwa Allah na Mtume Muhammad (saw) katika nyoyo za wanafunzi wake na kwa kwa viumbe wa MwenyeziMungu ndilo lilikuwa lengo lake kuu. Alikuwa mtu wa aina yake katika kuheshimu maadili ya kibinadamu na kutowa haki za wengine. Alikuwa akisema: Allah ni Mrehemevu sana.

Kasoro zozote katika kutimiza haki Zake Yeye atazisamehe lakini wengi watatiwa mkononi siku ya Hukumu kwa sababu ya hiyana katika kutowa haki za wengine. Katika siku hiyo ya Kiyama ambapo kila mtu atashughulika na nafsi yake, nani atakuwa tayari kuwasamehe wengine? Sheikh alikuwa mtu wa peke yake kuhusu Akl-i-Halal na Sidq-i-Maqaal (kula vile tu vilivyo hali na kusema ukweli tu) na alikuwa akizingatiya misingi ya ibada zote. Alikuwa akiishi maisha ya kawaida kabisa. Watu kutoka sehemu za mbali walikuwa wakimtembeleya wakiwa na shida zao naye akawakaribisha kwa bashasha na kuwatatuliya shida zao. Bila ya kujali tabaka, rangi, imani wala hadhi ya kijamii, watu wote hao walikuwa wakipewa heshima kubwa kiyasi kwamba alikuwa akiwaandaliya chakula kwa mikono yake mwenyewe na jambo hili alilidumisha katika maisha yake yote.

Mara nyingi kulikuwa na wageni wanane au kumi katika jamvi lake la kuliya chakula. Kutokana na tabiya yake ya ucheshi, ukarimu, na maongezi yake mazuri na yenye faida, idadi kubwa ya vijana wakawa wanafunzi wake, vijana hao wakampenda mno kuliko hata walivyowapenda wazazi wao. Sheikh alikuwa akiupa mazingatiyo maalum ustawi wa kiroho wa vijana hao. Kwa hiyo, alikuwa hatowi hotuba ndevu bali mwenendo wake wa maisha ya kila siku ulikuwa mfano na chimbuko la uwongofu mkubwa kwao. Mnamo mwaka 1988 pale Mirza Tahir Ahmad Qadiani, Khalifa wa na kiongozi wa nne wa Jumuiya ya Ahmadiya alipotowa chagizo la Mubahila ambalo katika anuwani yake liliwaita Waislamu wote kuwa ni Warongo na Makafiri, Sheikh alighadhibika.

Akasema: SubHanAllah! Hii hawezekani eti Umma mzima wa Waislamu, wafuwasi wakweli wa Mtume wa kweli wa Allah, Muhammad (saw) waitwe makafiri na umma wa Mzushi ndio uitwe umma wa Waumini! Kuanziya hapo hadi mwisho wa uhai wake, Sheikh akawa anauwandama ukadiyani katika kona zote za duniya kwa maandiko na hotuba zake. Alichapisha vitabu vingi na makala nyingi, akasafiri katika nchi mbali mbali kuleta mwamko miyongoni mwa Waislamu dhidi ya udanganyifu wa Mirza Ghulam Ahmad Qadiani kwa kutumiya jina la Uislamu. Kwa Rehema za Allah, nashukuru kwamba mtu mdogo sana kama mimi nikapata fursa ya kumsaidiya Sheikh katika harakati zake. Namuwomba Allah azidi kunipa msaada ili niweze kuendeleza kampeni hii ya uwamsho. Amiin. Wakati wa kampeni yake ya miyaka mingi, Sheikh Abdul Hafiidh Shaha alimchagiza Mirza Tahir mara kadhaa afanye naye duwa ya kuapizana (Mubahila) lakini Tahir mara zote akakwepa kuikubali.

Uhai na kifo viko mikononi mwa Allah, muda wa mtu kuondoka duniyani unapofika, hakuna wa kuweza kuuzuwiya. Lakini hapa ni muhimu kuzingatiya kuwa Mirza Ghulam Ahmad Qadiani na wafuwasi wake mara zote walikuwa wakiamini kuwa MUWONGO HUFA WAKATI MKWELI ANGALI HAI. AlHamdulillah, Thumma AlHamdulillah, Mirza Tahir Ahmad Qadiani alikufa Tarehe 19-4-2003, wakati Sheikh Abdul Hafiidh Shah bado akiwa hai. Tunamuwomba Allah amnyanyuwe katika daraja Sheikh Abdul Hafiiz Shah na atuwongoze kufuwata mafundisho yake. Amiin. Ewe Allah Rehema Zako ziwe juu ya Kipenzi Chako Mtume Muhammad (saw).

Habari kutoka Ujerumani Sheikh Rahiil Ahmad asilimu

Sheikh Rahiil Ahmad alizaliwa katika uhamadiya. Familiya yake ilikuwa ya kiahmadiya kweli kweli na alikuwa mfuwasi mkereketwa wa Mirza Ghulam Ahmad Qadiani. Yeye binafsi alikuwa mchapakazi kweli kweli katika Jumuiya, akiwa ameshika nyadhifa kadhaa katika jumuiya ya Ujerumani. Kwa Rehema za Allah mnamo mwezi Agosti, mwaka 2003 yeye pamoja na familiya yake waliikana Ahmadiya na kusilimu. Juu ya jambo hili alisema hivi:

“Mimi nilizaliwa nikiwa Kadiani (Ahmadiya) na baada ya kuusoma na kuutafakari ukadiani kwa miyaka kadhaa, nimefikiya hitimisho kuwa Genge la jumuiya ya Ahmadiya (kadiani) si dhehebu la Kiislamu bali ni shirika linalokusanya mapesa kwa jina la dini.

Mimi nimeshika nyadhifa kadhaa katika jumuiya kwa muda mrefu, na kwa sababu hii mambo mengi nimeyajuwa, na hivyo nikaona ni bora zaidi kuachana na jumuiya hii na kuvunja uhusiyano wangu na mfumo wa unyonyaji kwa jina la dini na nimeingiya katika dini ya kweli ya Mtume Muhammad (saw).”

(Daily Ummat, Karachi, Agosti 27, 2003)

Akihutubiya mkutano wa Khatme Nabuwwat kule Rabwah [Ghanab Nagar) mnamo Septemba 6, 2003, alisema hivi:

Ndugu zangu! Tunu hii ya mimi na familiya yangu kusilimu si matokeo ya jitihada zangu, na wala hatuna mchango wowote katika jambo hili. Bali Huu ndio ukweli wa milele wa Qur’an kwamba MwenyeziMungu humuonesha njiya ya uwongofu (hidaya) yule Amtakaye. Na wale wasiotaka kutafuta uwongofu basi Yeye huwaacha wapotee katika giza (la ukafiri). MwenyeziMungu amenineemesha neema Zake lakini hii ni neema kubwa ambayo ameitowa kwa mtu kama mimi niliyezaliwa nyumbani 4 mwa makadiyani na ambaye nilikuwa kizazi cha tatu au cha nne cha Qadiyani na ambaye nilizoweya mazingira halisi ya kikadiyani, (naam ndugu zangu! Katika ukadiyani mtoto halelewi bali hupagazwa), mimi ambaye nilipata elimu yangu kule Rabwah na ambaye katika maisha yangu yote nilishika nyadhifa katika Jumuiya hiyo, katika umri huu wa miyaka 56, Allah Aliyetakasika amenitowa gizani na kunileta katika nuru ya Uislamu. Neema za Allah hazikuishiya hapo, bali pamoja nami Kawaleta piya watu tisa wa familiya yangu katika taa iliyowashwa na Mtume Muhammad (saw) AlHamdulillah. (Khatme Nabuwwat Conference, Chanab Nagar (Rabwa)

Septemba 6, 2003).

Akiwahutubiya Waislamu alisema:

Lakini nataka mzingatiye jambo moja kwamba ishini na kadiyani wa kawaida kwa upendo, msimkashifu kwani mwenzetu huyo masikini kapagawishwa; muombeeni, ongeeni naye kwa hikima.

Badala ya kuzungumziya mada ya kifo cha Nabii Isa (as) au Khatma Nabuwwat, muonesheni wasifu wa Mirza Sahib na tabiya yake, jambo ambalo ndilo muhimu sana. Waulizeni jamaa zenu wa kadiyani wanamtazamaje Mirza Sahib?

Watakwambiyeni kuwa wanamkubali kuwa yeye ni Masihi Muwuud, nabii au muhaddith. Kisha waombeni mzungumziye wasifu wa Mirza Sahib na waulizeni jawabu lao litakuwa nini kama ikithibitika kwa maandiko yake, maneno yake na mazungumzo yake, na maandiko ya wafuwasi wake na watoto wake kuwa Mirza hawezi kuwa na hadhi hiyo? Waombeni wabainishe wasifu wa Mirza, kisha basi hakuna cha kuongeya nao zaidi. Mtu yeyote tu wa kawaida anaeweza kuzungumziya jambo hili. Mimi nakuhakikishiyeni kuwa hawatakaa mbele yenu. Maisha ya (Mirza Sahib) yamefunikwa na maturubai mazito, lakini wanazuwoni wakweli wamefanya jitihada kubwa kuyaanika hadharani maisha hayo yanayofichwa. Miwani yoyote waliyovaa machoni, ukizungumza nao kwa hikima namna hiyo, InshaAllah mazungumzo hayo yatakuwa na athari. Baada ya miyaka kadhaa ya utafiti wangu, nimefikiya hitimisho hili kuwa Jumuiya ya Ahmadiya si ya Kiislamu kabisa. Wala si dhehebu ndani ya Uislamu.

Bali ni dini mpya ambayo imepandikizwa katika kiwiliwili cha Uislamu mithili ya papasi. Mtume wa Uislamu ni Muhammad (saw) na mwasisi wa Ahmadiya ni Mirza Ghalam Sahib.

Baada ya kumkubali Muhammad Mustafa (saw), yeyote yule anaweza kuwa Muislamu lakini kwa kumkubali Mirza Sahib mtu atakuwa Ahmadiya au 5 Kadiani tu kwa sababu Uislamu ni dini ya Allah na ukadiyani ni dini iliyobuniwa na binadamu.

Hapana shaka kuwa Makadiani hutamka kalima ‘la ilaha illAllah Muhammadur Rasuulullah ‘, lakini mwisho wanamtaja Mirza Sahib. Mtu yeyote yule atakayekanusha, basi mwambiye asome kitabu kiitwacho Kalimatul Fasl cha Mirza Bashiir s/o Mirza Sahib. Lakini Waislamu wanapotamka Kalima, Wallahi, hakuna kingine kinachoongezwa. Ni kalima tukufu kabisa. Mtume (saw) aliyacha nyuma yake jeshi la Masahaba wakubwa wakati ambapo Mirza Sahib ameacha nyuma yake jumuiya ya wanafiki. Ni mnafiki tu ndiye atakayebaki katika Jumuiya ya Ahmadiya.

Kwa mujibu wa Mirza Mahmud mwenyewe, asilimiya 99 ya wahamadiya ni wanafiki. Jumuiya ya Ahmadiya ni jumuiya ya kukusanya fedha kwa jina la dini, fedha zenyewe si michango bali ni JAGA TAX ( fedha za fidiya)

Akiwahutubiya Makadiyani Sheikh Rahiil Ahmad alisema:

Sasa nataka kuwauliza swali rafiki zangu Makadiyani ambao wapo hapa na kupitiya kwao swali hili liwafikiye rafiki zangu wengine kwamba, sawa kwa ajili ya mjadala tukubali kuwa Mirza Ghulam Sahib alikuwa nabii. ?Je Allah kayakubali maombi ya manabii kwa ajili ya nyimati zao au hapana? Na katika duwa hizo je hakuna maombi ya kushushwa watu wachaMungu wenye uwezo wa kuongoza? Sasa basi ama maombi ya Mirza Sahib yalikubaliwa au kama hakuomba duwa ya kushushwa watu wema katika umati wake.

Vinginevyo inatiya shaka juu ya unabii wa Mirza Sahiib, kwani kulingana na madai ya jumuiya hiyo idadi yao ni 200, 000,000 (ijapokuwa takwimu hizo zina walakini lakini hebu tujaaliye tu idadi yao ni hiyo), je miongoni mwa hawa hakuna hata mmoja ambaye angepanda katika daraja la Taqwa (uchaMungu), uwadilifu na uwongozi ambaye wangeweza kumchaguwa kuwa Khalifa?

Je ni familiya ya Mirza Sahib tu yenye taqwa na uwezo wa kuongoza? Ikiwa mmekaa katika Jumuiya kwa zaidi ya miyaka miya moja na hamkuweza kumpata hata mtu mmoja mchaMungu nje ya familiya ya Mirza Ghulam Ahmad Sahib basi wakati umefika sasa wa kutafakari mnapata nini katika Jumuiya hii isiyo na nguvu?

Njooni! Njooni katika Uislamu hata leo mtakuta mamiya kwa maelfu ya watu wachaMungu. Hebu nyie wenyewe yasomeni maisha ya Mirza, tazameni vitabu vyake, someni simulizi zake, tazameni maandiko ya wafuwasi wake, tazameni maandiko ya wanawe.

Si yale maandiko wanayoyaonesha bali yale maandiko waliyoyaandika huko nyuma ambayo sasa wanayaficha nyinyi msiyaone.

Mkiyasoma maandiko hayo, basi kama nilivyofanya mimi, na nyinyi mtafikiya hitimisho hilo hilo kuwa Mirza hawezi kuwa nabii wala muhaddith. Namuwomba Allah Atuweke sote katika nuru ya Imaan na akujaaliyeni uwongofu mje katika utume halisi wa Muhammad (saw). (khutuba ya Sheikh Rahiil Ahmad wa Ujerumani katika Mkutano wa Khatme Nabuwwat mjini Rabwa Pakistan, Septemba 6, 2003).

Kutoka kwa Sheikh Rahii Ahmad katika Jumuiya si tukio dogo. Wahamadiya wamepata hofu kubwa sana kwani huyu alikuwa mwanajumuiya wa ngazi ya juu na ana nasaba na familiya kongwe ya Ahmadiya ya Rabwa. Tukiyo hilo lilitokeya sambamba na ziyara ya Khalifa mpya wa Jumuiya hiyo, Mirza Masruur Ahmad nchini Ujerumani. Wakuu wa Jumuiya akiwemo Khalifa wanajuwa uzito wa tukio hili. Si ajabu hivi sasa Jumuiya inaandaa mpango wa mauwaji dhidi ya Rahiil Ahmad.

Mshairi wa Ahmadiya, Muzaffar Ahmad naye asilimu Ujerumani

Taathira za kuhama kwa Sheikh Ahmad katika Jumuiya hiyo bado hazijapunguwa kwani Ahmadiya mwingine wa ngazi ya juu pamoja na familiya yake wametoka Ahmadiya na kuingiya katika Uislamu mnamo Septemba 19, 2003.

Muzaffar Ahmad (36) anatokeya Peshawer Pakistan na amekuwa akiishi Ujerumani kwa miyaka mingi. Kwa kutambuwa kazi yake katika Jumuiya aliwahi kupewa medali ya dhahabu na kusifika kwa kupewa jina; ‘Mshairi wa Ahmadiya’. Aidha amekuwa akifanya kazi kama mjumbe wa Baitul-ul-Maal ya Jumuiya.

Alitangaza rasmi kuukana uhamadiya na kusilimu katika Msikiti wa Tauhiid, Offenbach, Ujerumani mikononi mwa Sheikh Mushtaq-ur-Rahman. Kuhusiyana na hili, taarifa zinasema kuwa Amiir wa Jumuiya ya Husun, Muniir Ahmad na Amiir wa Taifa, Abdullah Wagushauser piya wamefahamishwa kwa maandishi.

Baada ya kufanya hivyo, Bw. Muzaffar Ahmad na familiya yake sasa wanapata vitisho vya kuuwawa kutoka Jumuiya ya Ahmadiya. Piya Muzaffar ameandika baruwa kwa Amiir wa Mkowa, Columbus Khan kuhusiyana na jambo hili ambapo ameeleza kuwa anapata vitisho vya kuuliwa na kwamba jambo hili likome.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, katika baruwa yake hiyo kwa Amiir wa Mkowa, ameeleza kuwa ‘mimi sina haja ya kufichuwa hadharani jitihada za Jumuiya kufunguwa mashitaka mahakamani wala jitihada zako binafsi katika 7 mahakama ya sheriya wala mimi sitaki kuisababishiya Jumuiya maumivu ya kudumu kwa kuutobowa undani wake.

Hata hivyo, kama Jumuiya haiachi mwenendo wake muwovu wa kidajali na sera yake ya kijinga na ya kizamani dhidi yangu basi tutakutana huko huko mahakamani (Daily Ummat, Karachi 19 Septemba). Mnamo Septemba 20, 2003, Muzaffar Ahmad alihutubiya watu waliokusanyika kwa ajili ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Tauhiid. Akasema:

“Siku ya leo ni siku ya baraka kwa familiya yangu yote. Tunatoka katika mabonde ya mateso ya ukafiri, udanganyifu na ghiliba na kuingiya katika njiya nyoofu yenye nuru ya Uislamu.

Habari za hila zamakadiyani, uwovu na ufedhuli wao zimeeneya kwa zaidi ya miyaka miya moja. Kwangu mimi sababu za kusilimu kwangu ni: Nyuma ya uwamuzi huu kulikuwa na miyaka saba ya kusoma usiku na mchana vitabu, maelezo binafsi, mwenendo wa ndani wa Jumuiya, kujitenga mbali na Sunna za Mtume (saw), mwenendo wa Jumuiya usiokuwa wa kawaida na unaopingana na Uislamu, imani chungu tele za kipagani, jitihada za Jumuiya kusambaza maandiko yenye mabadiliko na utatanishi juu ya maana ya Qur’an, na maamuzi ya Umma wa Kiislamu yaliyofikiwa Mwezi Aprili na Septemba mwaka 1974 ambayo yaliwatowa makadiyani nje ya dini ya Uislamu.

Kwa upande mwingine madai ya Mirza Sahib yanaanziya pale alipokuwa ‘pandikizi’ la Waingereza hadi katika dai la uungu. Kwa kifupi jina lingine la Kufuru ni Ukadiyani. Kwa sababu hiyo, mimi pamoja na familiya yangu nzima tunazikana imani zote hizo mbaya na tunatangaza kurudi katika Uislamu. (Utenzi wa Kiudu: Hum aisay saada diloon kee niyaz mandee say Butoon nay Kee hein jahaan mein khudaeeyaan kiya kiya) Kwa sababu ya ukarimu wa watu wenye nyoyo laini kama sisi.

Masanamu yamefanya mambo mengi ya kiungu duniyani kote. Mwishowe akawashukuru sheikh Mushtaq-ur-Rahman, Sheikh Mohammed Ahmed, Iftikhar Ahmed na Sheikh Raheal Ahman kwa mwongozo wao na akaelezeya dhamira yake ya kufanya harakati katika njiya ya Uislamu (Daily Ummat, Karachi Septemba 19 2003)

Mirza Abu Bakar Salahuddin (TOMBMASTER) wa Marekani aikana Ahmadiya na kujiunga na Ubahai

Wakati Jumuiya ya Ahmadiya ikiwa bado haijaondokwa na fadhaa ya kuondoka kwa Sheikh Rahii Ahmad, Ahmadiya mwingine wa ngazi ya juu ambaye ni Muamerika mweusi wa Marekani, Mirza Abu Bakar Salahuddin ameikana Ahmadiya na kuingiya katika Ubahai. Ingawaje alikuwa amechukuwa hatuwa hii mwezi Julai, 2003 lakini taarifa zilicheleweshwa kutangazwa kwa sababu Jumuiya ilikuwa inajaribu kumrejesha.

Mirza Abu Bakar amekuwa akiishi Marekani kwa miyaka 27 iliyopita. Alikuwa ni kiongozi wa Jumuiya ya Ahmadiya ya Marekani na ni msimamizi wa tovuti za Ahmadiya na ameandika vitabu vitatu. Yeye ndiye aliyekuwa akitowa nguvu ya mahubiri ya Ahmadiya kwa njiya ya mtandao wa intaneti na akaifanya iwe jumuiya yenye mafanikio. Bw. Abu Bakar ameandika vitabu vingi kuiunga mkono Ahmadiya lakini alikuwa mashuhuri zaidi kutokana na tovuti yake “Tomb of Jesus” na ndiyo maana ya jina Tomb Master.

Katika tovuti hii amejaribu kuthibitisha kwa maandiko yake kuwa Isa (bin Mayramu amekufa na kuzikwa Kashmir. Mwanzoni pale alipotaka kuitangaza tovuti yake alijaribu kuficha mahusiyano yake na Ahmadiya lakini muda si muda ikadhihirika kuwa yeye ni Ahmadiya mkereketwa. Alikuwa na uhusiyano wa karibu na Mirza Tahir Ahmad, Khalifa wa nne wa Ahmadiya ambaye alimmwagiya sifa nyingi kwa jitihada zake na kumbashiriya maisha yenye nuru. Lakini wapi! Mirza Tahir kwa mara nyingine tena akaonekana muwongo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya Makadiyani, katika kujienguwa kwake katika ukadiyani Bw. Salahuddin alieleza kuwa haamini tena Ukadiyani, anauona ubahai kama ndio uwokovu, hivyo, akajivuwa madaraka yote na kukana imani zote za kikadiyani. Aidha aliandika hivi:

Mimi sijihusishi tena na suwala la kufa au kutundikwa kwa Yesu msalabani. Naitakidi Ubahai ndiyo njiya sahihi. Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, Salahuddin ameandika zaidi kuwa yeye haamini Uislamu na wala haioni imani yoyote ya Kiislamu kuwa ni sahihi (Daily Ummat, Karachi, 3 Septemba 2003) Hapa nataka wasomaji wazingatiye kuwa Bw. Abu Bakar aliingiya katika Ukadiyani akidhani kuwa ni Uislamu. Lakini alipokosa kutimiziwa hitajio lake la kiroho alililokuwa akilitafuta sio tu aliachana na uhamadiya bali piya akajitenga kabisa na Uislamu. Kama kweli bwana huyu anautafuta ukweli, InshaAllah iko siku MwenyeziMungu atamuongoza katika Uislamu halisi.

Mauwaji ya Panditi Lekhram

(Habari hii inaedeleya kutoka Al-Fatwa lililopita)

Wapendwa wasomaji! Katika toleo lililopita la Al-Fatwa International (Na 29),

tulikuwa tumeezeya habari fulani zilizothibitisha jinsi Jumuiya ya Ahmadiya

ambayo imeibuwa kauli mbiu ya “Upendo kwa Wote, Hapana Chuki kwa

Yeyote” (“Love for All, Hatred for None”), inavyowatendeya wapinzani wao.

Katika toleo hili, tutaangaliya jinsi mwasisi wa Jumuiya hiyo, Mirza Ghulam Ahmad Qadiani alivyokuwa akiwatendea wapinzani wake. Kwa mnasaba 9 huwo, sehemu ya habari juu ya Lekhram ilitolewa katika toleo lililopita la Al-Fatwa. Sehemu iliyobaki inasimuliwa hapa.

Mirza alianza safari yake ya kidini kama mtumishi wa Mungu na mtu wa midahalo. Tangiya mwanzo alianza kuichokoza jamii ya Wahindu ,Hindu Arya Samaj kwa hotuba zake wakati alipokuwa Lahore. Baada ya kurejeya Qadiani, mara kwa mara katika matangazo, akawa anawachagiza kufanya naye midahalo.

Lengo la kufanya hivyo halikuwa kueneza Uislamu bali lilikuwa ni kujijengeya sifa na umaarufu. Matangazo yote hayo bado yapo katika machapisho ya Jumuiya ya Ahmadiya, Makao Makuu London.

Brahiin-i-Ahmadiyya na madai yake ya kuwa Mteule wa Mungu

Mnamo mwaka 1880,Mirza Ghulam alidai kuwa yeye kateuliwa na Mungu kuandika Brahiin-i-Ahmadiya katika juzuu 50 ili kuthibitisha usahihi wa Uislamu. Wakati huwo huwo akawachagiza wasio Waislamu kuandika andiko la kukanusha kitabu hicho Kinyume na kanuni nzuri za Uislamu za kufanya midahalo ya kistaarabu katika mas’ala ya dini, katika kitabu hiki Mirza Ghulam ametumiya lugha ya shari katika kuwalinganiya wasio-Waislamu.

Lugha hiyo ilikuwa ya maudhi mno kiyasi ambacho hakuna Mkristo au Mhindu ambaye angeweza kuzuwiya hasira zake baada ya kusoma kitabu hicho. Kitabu hiki kikapanda mbegu ya chuki na uhasama wa kudumu dhidi ya Uislamu na Waislamu katika nyoyo za Wakristo na Wahindu. Hili lilithibitika kwa Pandit Lekhram ambaye aliandika andiko la kujibu kitabu hicho kwa jina la Takziib Brahiin-i-Ahmadiya. Kitabu hiki hakikuwa na chochote isipokuwa kashfa na matusi.

Kilijaa kashfa na shutuma dhidi ya watu wachaMungu na watukufu hasahasa kaporomosha matusi dhidi ya Mitume wa Allah. Lekhram kadhihirisha hasa uwaduwi uliomo katika nafsi yake. Hayo, moja kwa moja, yalikuwa ni matokeo ya kitabu cha Mirza, Brahii-i-Ahmadiya ambacho baada ya kuchapishwa kwake, vikachapishwa vitabu vingi ambavyo vilikuwa vya kashfa ya wazi dhidi ya Mtume (saw) ambapo Mirza anabeba lawama zote kwa majibu hayo. Badala ya kuandika jibu la kisomi kwa andiko la Lekhram, Mirza akaanza kutangaza uwezo wake wa kuonesha miujiza. Katika toleo lililopita la Al-Fatwa nilinukuu matukio mengi ya kuonesha jinsi Lekhram alivyomtega Mirza ili atekeleze ahadi yake ya kuonesha miujiza.

Ni dhahiri kuwa Mirza Ghulam, Mzushi, hakuwa na uwezo wa kufanya miujiza iliyodaiwa. Kwanza, alijaribu kumtuliza Lekhram kwa maruhani yake lakini Lekhram hakutulizika kwa mbinu hizo.

Mnamo mwaka 1886 Mirza Ghulam akaandika kitabu alichokiita “Surma Chasme Arya ambapo aliialika Jumuiya ya Hindu Arya Samaj (ambayo Lekhram ndiye alikuwa kiongozi wake) kwa ajili ya duwa ya kuapizana (mubahila) na kuweka muda wa mwaka mmoja wa kudhihirika kwa athari za Mubahila.

....”na kisha muda wa kusubiri hukumu ya Mungu ni mwaka mmoja.Ikiwa baada ya mwaka mmoja mwandishi wa kipeperushi hapatilizwi kwa adhabu ya Mungu na mateso au kama haimshukii mpinzani, kwa hali zote mbili, huyu roho mnyenyekevu (Mirza) atalipa fidiya ya Rupiya 500/= (Surma Chasme Arya, Roohani Khazain juz.2 uk.252) Kwa mara nyingine tena Mirza akaichagiza Hindu Arya Samaj kwamba hakuna yeyote awezaye kukijibu kitabu chake:

“Kitabu hiki, nacho ni Surma Chasme juu ya Mdahalo na Lala Murlidhar, Drawing Master, Hoshiarpur ambacho kinabainisha wazi imani potofu ya Ved, kimeandikwa kwa imani na kwa dai kuwa hakuna Arya anayeweza kuandika andiko la kukikanusha. (Advertisement of Reward Rs.500, Roohani Khazain juz. 12 uk. 320)

Lakini kinyume na madai ya Mirza Ghulam, Hindu Arya wakaandika majibu ya kitabu hicho, ambapo kuhusiyana na majibu hayo Mirza Ghulam akaandika hivi katika maandiko yake:

“na zaidi ya hivyo kijitabu hicho ambacho kinaitwa ‘Surma Chashme Arya Kee Haqiiqat Aur Fun Furaib Ghulam Ahmad’ (Ukweli wa Surma Chashme Arya na Mchezo wa ghiliba wa Ghulam Ahmad) ni muhimu kukiangalia pamoja na kitabu changu.” (Shuhna-i-Haq, Roohani Khazain juz.2 Uk.328 tanbihi)

Baada ya kuchapisha mwaliko huu wa Mubahila, Pandit Lekhram akajitokeza kukabiliyana na Mirza Ghulam. Akiikubali changamoto yake ya Mubahila mwaka 1888, Lekhram akachapisha ‘Mubahila-nama’. Kulingana na sharti lililokubaliwa, hadi mwaka 1889, Lekhram awe amepatilizwa kwa adhabu ya Mungu. Lakini hakuna chochote kilichotokeya. Wote wawili walibakiya salama salmini. Ndipo Mirza alipoanza majigambo ya kuonesha ishara ya mbinguni. Lakini piya akashindwa kufanya jambo hilo!!! “Janab Mirza Saheb. Namaste...Sababu ya kusafiri kote huku kutoka Peshawar kuja Qadiani ni hii tu na niko hapa kwa matumaini kuwa nitakiri baada ya kuona miujiza yako, matukio yenye nguvu za Kiungu na funuwo na ishara kutoka mbinguni na kabla ya kujadili utaratibu mwingine wowote jambo hili litimizwe katika hadhara ya watu wenye heshima zao...hapa lazima ikumbukwe kuwa kukaa nyumbani na kuonesha ishara mbele ya waumini ni jambo jingine na kuthibitisha ishara mbele ya hadhara ya watu wenye 11 heshima na elimu ni jambo jingine.Natumaini kuwa utaniheshimu kwa kunipa jibu. Usitowe visingiziyo...ninakuwomba tena na tena kuwa kama unayo chembe ya ukweli, nioneshe (ishara ya mbinguni) vinginevyo kwa ridhaa ya Mungu jizuwiye (kutowa madai ya aina hiyo)....” (Baruwa ya Lekhram kwa Mirza Ghulam, Roohani Khazain juz 12 uk. 113)

Imesainiwa.

Lakini wapi, Mirza Ghulam hakuweza kuonesha ishara ya Kiungu kutoka mbinguni. Lekhram akaendeleaya kumuandikiya baruwa Mirza. Hatimaye baada ya maandikiyano yaliyochukuwa miyaka mingi (tangu 1885 hadi 1893) wakakubaliyana kwa makubaliyano yafuwatayo ambayo yalichapishwa na Mirza Ghulam katika kitabu chake:

“Makubaliyano hayo ambayo yalifikiwa kati yangu na Lekhram kuhusiyana na uoneshaji wa ‘ISHARA’ kwa andiko ambalo Lekhram kaandika kwa mikono yake....mukhtasari wa makubaliyano haya marefu ni kuwa kama utabiri fulani utatolewa kwa Lekhram halafu usitokee kweli basi huwo utakuwa ushahidi wa ukweli wa dini ya Uhindu na utakuwa wajibu kwa mtu aliyetowa utabiri huo (Mirza Ghulam) kuingiya katika dini ya Arya AU la, basi atowe Rupiya 360/= kwa Lekhram ambazo zihifadhiwe kabisa dukani kwa Bw. Shrampat, mkaazi wa Qadiani. Na kama huyo mtu anayetowa utabiri ataonekana kuwa mkweli basi hiyo itachukuliwa kama ni ishara ya ukweli wa Uislamu na utakuwa wajibu kwa Pandit Lekhram kusilimu.” (Istafta, Roohani Khazain juz. 12 uk.117)

Kutokana na maelezo ya hapo juu inadhihirika wazi wazi kama mchana kweupe kuwa kila utabiri uliokuwa ukitolewa, pale ulipowadiya muda wa kutimizwa, Lekhrama angekuwa hai, angeshuhudiya huko kutimiya kwa utabiri, ingelikuwa wajibu kwake kusilimu baada ya kuthibitika kwa utabiri, kwani bila kuwa hai kusingekuwa na suwala la kuwona ishara ya uweza wa Mungu kutoka mbinguni na muujiza wa Mirza Ghulam wala isingewezekana kuikubali imani ya Kiislamu kama ilikuwa afe wakati wa kutimiya utabiri huwo.

Chini ya makubaliyano haya utabiri ufuwatao ulitolewa na Mirza Ghulam

Utabiri wa Adhabu ya Kiungu

“Sasa kwa chapisho la utabiri huu nataka kuweka wazi kwa Waislamu, Arya (Wahindu) na Wakristo wote na imani nyingine kuwa ikiwa ndani ya MIAKA SITA kuanziya tarehe ya leo ambayo ni Februari 20 1893, adhabu hiyo ambayo si mapatilizo madogo na ni Khaariq-i-Aaadat ( si ya kawaida au ni ya Kiungu...Rashid) {yaani siyo moja ya magonjwa au maradhi ya kawaida na madogo tu ambayo wakati mwingine mtu hupona na wakati mwingine hufa} bali yenyewe ina hofu ya Mungu ndani yake {yaani ina ishara za ghadhabu ya Mungu}, (ikiwa adhabu hiyo) haitamshukiya mtu basi eleweni kuwa mimi sitoki kwa Mungu na wala sina mawasiliyano yoyote na Roho Wake {kwamba bishara ndiyo msingi wa kuuhukumiya ukweli na uwongo wangu}. (Roohani Khazain juz.12 uk.118).

Tanbihi: maneno ndani ya mabano haya “{}” ni sehemu ya maneno halisi.

Katika kitabu hicho hicho Mirza Ghulam anaielezeya tena nukta yake:

“Sasa ninakiri tena kuwa...kama akipata homa tu ya kawaida au akipata tu maumivu fulani au akipata Kipindupindu na kisha akapona basi hiyo haitahesabiwa kama ni ishara na bila shaka itakuwa ni ulaghai na uwongo. “ (Roohani Khazain juz. 12 uk. 17).

“Siku ya leo ambayo ni Jumanne Februari 20 1893 wakati nilipofanya taamuli kupata muda wa adhabu hii ya Mungu, Mungu alinifunuliya kuwa tokeya tarehe ya leo ambayo ni Februari 20 1893 ndani ya miyaka sita mtu huyu atapatilizwa kwa adhabu kali kutokana na ulimi wake mchafu, hiyo ni kama adhabu ya kashfa dhidi ya Mtume (saw), ataadhibiwa kwa adhabu kali. Sasa kwa kuchapisha utabiri huu nataka kuwadhihirishiya Waislamu, Wa-Arya (Wahindu) na Wakristo wote na watu wa imani nyingine kuwa kama ikiwa ndani ya kipindi cha MIYAKA SITA tokeya tarehe ya leo adhabu ya Mungu isipomshukiya mtu huyu ambayo ni kubwa zaidi ya mapatilizo ya kawaida (iliyo kinyume na maumbile au ya Kiungu...Rashid-Khaariq-i-Aqadat) na isipokuwa na hofu ya Mungu basi eleweni kuwa mimi sitoki kwa Mungu na wala sina mawasiliyano na Roho Wake. Na kama nikidhihirika kuwa muwongo katikautabiri huu, basi niko tayari adhabu yoyote ile na niko tayari kujitiwa kitanzi na kunyongwa Na isitoshe licha ya kukiri kwangu, hii piya ni wazi kuwa kubainika kuwa ni muwongo katika utabiri ni fedheha mbaya zaidi kwa mtu yeyote yule.

(Roohani Khazain juz. 12 uk. 15)

Khaariq-i-Aadat- Kinyume na Maumbile au ya Kiungu

Hapa ni muhimu kuzingatiya kuwa kwa mujibu wa maelezo ya Mirza Ghulam, aina ya adhabu inatakiwa iwe Khariq-i-Aadat. Je Mirza Ghulam anaielewa vipi hasa istilahi hii? Hebu ngoja tuone:

“Kitu ambacho hakina mfano wa kulinganisha nacho, kwa maneno mengine hii piya inaitwa Khaariq-i-Aaadat”. (Roohani Khazain juz, 2 uk. 19) “Khaariq-i-Aaadat hutumika kuelezeya kitu kisicho na mfano katika duniya hii.”

(Haqiiqatul Wahi, Roohani Khazain juz. 22 uk. 204)

Kwa kifupi:

Hitimisho ambalo linaweza kufikiwa kutokana na nukuu za hapo juu kutoka katika kitabu cha Mirza Ghulam ni kama ifuwatavyo:

1.Bishara kuhusiyana na Lekhram ilikuwa itoke kwa Mungu, na muda wake uliowekwa ulikuwa ni miyaka sita.

2.Adhabu itakuwa katika sura ya Khaariq-i-Aaadat ambayo haina mfano wake katika duniya hii.

3.Ilikuwa lazima kwa Lekhram kuwa hai hadi itimiye bishara ili aishuhudiye na kusilimu.

4. Iwapo bishara hatatimiya basi Mirza Ghulam Ahmad Qadiani atatangazwa kuwa ni MUWONGO na atastahili adhabu na kwa matakwa yake mwenyewe, atanyongwa.

5.Iwapo utabiri hautatimiya basi ama Mirza ataingiya katika dini ya Uhindu au atalipa fidiya ya Rupiya 369 kwa Lekhram Kwa mujibu wa bishara yake, ndani ya

miyaka sita yaani hadi kufikiya Februari 20 1899 Lekhram awe amepata adhabu hiyo ya Mungu ambayo haina mfano na ambayo ingetiya hofu ya Mungu katika moyo wake, matokeo yake Mirza Ghulam angemtaka bwana huyo asilimu na yeye Lekhram alikwishakubaliyana na hilo. Lakini jambo hilo halikutokeya . Badala yake Lekhram aliongopewa na kuuliwa.

Ushahidi wa kimazingira

Katika mauwaji yoyote ya kupangwa, mara nyingi ni vigumu kupata ushahidi wa nguvu katika kumtambuwa muuwaji au kuwatambuwa waliopanga mauwaji.

Kwa hali hiyo, wapelelezi hutegemeya ushahidi wa kimazingira kufunguwa kesi. Katika upelelezi wowote wa tuhuma za mauwaji motisha na maslahi ni mambo yanayowekwa mbele. Hebu tuwone kilichotokeya katika kesi ya mauwaji ya Lekhram na ushahidi gani wa kimazingira tulionao. Baada ya kutangaza utabiri kama kawaida yake Mirza Ghulam alitambuwa kuwa alitangaza tu jambo hilo lakini kutimiya kwake ni bahati nasibu, kwa maana kuwa alielewa fika kuwa msaada wa Allah haupo kwake. Kilichokuwa kinaendeleya katika undani wake anakijuwa Allah tu, lakini kuna ushahidi fulani wa kimazingira hapa ambao unatowa mwangaza juu ya kile ambacho Mirza Ghulam alikuwa anakipanga:

“Umri wa Lekhram kwa hivi sasa, sana sana ni miyaka 30 na ni kijana mbichi mwenye umbo lenye nguvu na afya nzuri. Na huyu mtu mnyenyekevu ni mkubwa kidogo kwa miyaka zaidi ya hamsini na ni mdhaifu na mgonjwa mgonjwa wakati wote anasumbuliwa na aina mbalimbali za magonjwa. Licha ya hivyo, itadhihirika katika shindano hili ni kipi kinachotoka kwa binadamu na kipi kinachotoka kwa Mungu.” (Siraj-i-Muniir, Roohani Khazain vol. 12 p. 17)

Baada ya muda fulani Mirza Ghulam akatowa utabiri mwingine:

“Siku ya leo ambayo ni Aprili 12 1893/14 Ramadhan 1310 AH, asubuhi wakati nilipolala niliona kuwa nimekaa ndani ya jumba kubwa ambamo walikuwemo rafiki zangu, hapo hapo kijana mwenye nguvu na haiba ya kuhuzunisha kama vile damu inamvuja usoni akaja na kusimama mbele yangu. Mimi nikaangaliya juu na kubaini kuwa ni kiumbe wa aina mpya kana kwamba si binadamu bali ni miongoni mwa malaika wa adhabu na kitisho chake kiliingiya katika nyoyo. Na wakati mimi nikitazama akaniuliza Lekhram yuko wapi. Na akachukuwa jina la mtu mwingine kwamba naye yuko wapi Hapo nikagunduwa kuwa mtu huyo katumwa kuja kumuadhibu Lekhram na huyo 14 mtu mwingine, lakini sikumbuki huyo mtu mwingine ni nani, ndiyo bila shaka nakumbuka kuwa mtu huyo mwingine alikuwa miongoni mwa wale ambao nilishawachagiza. Na hii ilikuwa Jumatatu saa kumi alfajiri.” (Siraj-i-Muniir, Roohani Khazain vol. 12 uk. 19)

wa basharnii rbbi mubashirun sa t’arefo yaum al-eid wa aleid aqrab....Tafsiri

yake ni..na huku akinipa habari njema za ishara Mungu akasema kuwa muda si mrefu utaitambuwa siku ya Eid..na Mungu akaniahidi na kuniitikiya duwa yangu kuhusiyana na fisadi mmoja aduwi wa Mungu na Mtume, ambaye ni Lekhram Peshawari na akaniambiya kuwa atakufa tu”. (Siraj-i-Muniir, Roohani Khazain vol. 12 uk. 119)

SubHanAllah!! Huyo anayeitwa Mungu wa Mirza Ghulam hakuheshimu makubaliyano baina ya Mtume na mpinzani wake, ingawaje makubaliyano hayo na utabiri ulitolewa baada tu ya ‘mungu’ kuufunuwa kwa mtume wake!!!

Lekhram auliwa kwa jambiya – Je hili ndilo jambo lisilo la kawaida hili?

Mnamo Machi 6 mwaka 1897 Lekhram aliuliwa kwa jambiya lililomtumbuwa tumbo. Murabi wa Ahmadiya/Qadiyani na wahubiri wakasema kuwa Lekhram aliuliwa na Malaika na kwa hiyo utabiri wa huyo anayeitwa Masihi aliyeahidiwa umetimiya.

Wapendwa wasomaji! Usomeni tena kwa makini utabiri huu wa Mirza Ghulam Ahmad, someni tena kwa makini makubaliyano kati ya Mirza Ghulam na Lekhram.

“Siku ya leo ambayo ni Jumanne Februari 1893, wakati nilipofanya taamuli kupata muda wa Adhabu hii ya Mungu, Mungu akanifunuliya kuwa tokeya tarehe ya leo ambayo ni Februari 20 1893 nadani ya kipindi cha miyaka sita mtu huyu atapatilizwa kwa adhabu kali kutokana na ulimi wake mchafu, hiyo ikiwa kama ni adhabu ya kashfa dhidi ya Mtume mtukufu (saw), ataadhibiwa kwa adhabu kali. Sasa basi kwa kuchapisha utabiri huu nataka kuwadhihirishiya Waislamu, Waarya (Wahindu) na Wakristo wote na watu wa imani nyingine kwamba kama ikiwa ndani ya MIAKA SITA tokeya tarehe ya leo, adhabu hii ya Mungu haitamshukiya mtu huyu ambayo ni kubwa kuliko mapatilizo madogo madogo na ni Khaariq-i-Aaadat (iliyo kinyume na maumbile au ya Kiungu...Rashid) na kama isipokuwa na hofu ya Mungu ndani yake, basi eleweni kuwa mimi sitoki kwa Mungu na wala sina mawasiliyano na Roho Wake. Na ikiwa mimi nitaonekana muwongo katika utabiri huu, basi niko tayari kupata adhabu yoyote ile, niko tayari kutiwa kitanzi shingoni na kunyongwa. Na licha ya kukiri kwangu huku na hii ni dhahiri piya kuwa kuonekana muwongo katika utabiri ni fedheha mbaya sana kwa mtu yeyote yule.” (Roohani Khazain vol. 12 uk. 15).

Je hapa kuna ishara yoyote ya mbali kuwa Lekhram atauliwa? Utabiri unahusu kuonesha jambo lisilo la kimaumbile/la Kiungu/si la kawaida, ni muujiza usio na mfano, ishara kutoka mbinguni na hauhusu kifo cha Lekhram.

Je kifo cha Lekhram kilitokana na jambo fulani lililo kinyume na maumbile na

lisilo na mfano? Kumtumbuwa mtu hadi kufa ni tukiyo la kawaida. Muuwaji

anaweza kukodiwa kirahisi kwa malipo fulani. Sasa kipi ambacho kilikuwa si

cha kawaida wala kisicho na mfano katika mauwaji haya? Wakati ambapo

[1] [ 2]

:   admin       (   )
: 3 /5 ( 1 )

: 26-11-2009

: 4112